Mchawi wa CHADEMA huyu hapa

Mchawi wa CHADEMA huyu hapa

Kuna kipindi M/kiti alijaribu kubalance Ukabila akamleta kijana toka Tarime na kumweka pale makao makuu Kama Msaidizi wake Lakini kwa kutojua Yule kijana akaandika kitabu cha kumbukumbu cha Maisha ya Chacha Wangwe kimya kimya pasipo kujua kuwa Mkiti Kuwa hapendi Msaidizi wake amkumbuke Chacha Wangwe yule kijana Siku alipotaka kukizindua kitabu tu M/kiti akajua ni Siku hiyo hiyo akamfukuza toka makao makuu na kupata Misuko suko ambayo haifai kuhadithia kwani hadi lap top yake iliporwa huyo kijana amehamia NCCR ukitaka akupe story nenda pale NCCR muulizie Yule kijana aliyetunga kitabu cha Maisha ya Chacha Wangwe watakuonyesha muulize maswali yote utapata jawabu.

Hoja nzuri sana.......!!! Tatizo ni Viongozi, hawako tayari kuzipokea changamoto na kuzifanyia kazi.... laiti hoja zilizoandikwa kwenye Waraka ule zingechukuliwa kama changamoto na kubadilisha misimamo na mitizamo yao haya yote yasingetokea... lazima unapoongoza Taasisi yeyote ujue kuwa watu wote hawawazi kama unavyowaza wewe na wanatofautiana kimtazamo na kifikira.... haya yote yote yasingetokea kama Viongozi wa CDM wangelitambua mawazo ya wanaowaongoza na Viongozi waandamizi.... A good Leader predicts and foresees what may happen in future........
 
kwan zito akibaki kuwa mwanachama wa chadema na mbunge wa chadema kuna tatizo gani.......kauli zenu za zito kashinda na uongoz umeshindwa hazina mantiki ...kwan kulikua na mashindano gani?

Hakuna tatizo......!!! hakukukua na mashindano ila kulikuwa na kesi mahakamani kati ya ZZK na CC
 
Nzilo

Hukohuko fb ukiangaliA magroup na page za maana zina watu wachache sana, Lakini Magroup na page za kipuuzi zinawafuasi wengi sana.

Mfano page ya Zitto ina watu 30,000 lakini page ya Mzee wa Utamu ina watu 100,000.

Hope kuna cha kujifunza hapo.

nimekupa like nikaona haitoshi mkuu! nimeamua nikuletee nyingine kwa mkono.
 
Last edited by a moderator:
ipo siku utaufahamu umuhimu na ushawishi wa ZZK siyo sasa..... kipindi chama kitakapokuwa kimepoteza mwelekeo na si muda mrefu.... labda tu hali hiyo CDM wainusuru kwa kutomfukuza uanachama ZZK..... "Maumivu ya kidonda cha mtu ayajua mwenye nacho..."

kama chama kitapoteza muelekeo lakini kikabaki na watu watiifu ni heri kuliko kibaki salama kikiwa na watu aina ya zitto.
 
Kuna tatizo kubwa Chadema, weledi umeenda safari, weledi utakaporudi utakuta chama kiko chali. Sasa angalia wapenzi wa Mbowe na Hoja zao very low. CC ya chama ndio utafikiri walilewa kwanza ndio wakaingia kwenye kikao.

Hakuna mtu mwenye uelewa wa kawaida tu anaweza kukubali mashtaka ya uongo na ya kutunga kama haya. Naamini hata akina Dr. Kitila na Mwigamba wakienda mahakamani watashinda pasi na shaka.

Wanashabikia dhuluma chama kinaanguka. Mbowe na Dr. Slaa wanakiua chama mchanamchana sijui ----------!

Uko sahihi......
 
uongozi wa chadema wajinga wote na kama wameruhusu ujinga huu mambo kwao ni taiti sana wamuombe mungu mwingi wa rehema ili awanusuru.
 
uongozi wa chadema wajinga wote na kama wameruhusu ujinga huu mambo kwao ni taiti sana wamuombe mungu mwingi wa rehema ili awanusuru.

Tena maombi ya Mzee wa Upako.... kwani maombi ya Dr. Slaa hayatoshi...
 
Then what? atafanyakazi na katibu yupi? M/Kiti yupi?...wajumbe wepi? kwanini msiwe wakweli wa nafsi zenu kuwa amefanikiwa kutetea posho zake za ubunge na uenyekiti wa PAC? Mlarushwa mkubwa kama Zitto kuwa M/Kiti wa kamati ya Bunge i.e watch dog committee inayochunguza mashirika ya umma huoni kuwa kuna walakini?...kweli wajinga ndio waliwao...Mahakama ilikuwa haina namna zaidi ya kuitikia wito wa Rais na Mwenyekiti wa CCM... Ukweli huu utasimama mpaka siku ya mwisho wa dunia kuwa Zitto si Msafi na CCM wako nyuma yake kujaribu kudhoofisha upinzani... After all in saltation Zitto atasubutu kumwangalia Mbowe na Viongozi wake kweli...Kijana aliechukuliwa kibohehe secondary alikokuwa anashindwa hata kwenda likizo kwa kukosa nauli leo anauwezo wa kuingia kwenye propaganda chafu ya kumchafua master wake ? Anazuia harakati za kuokoa Tembo, Madini na Gesi mali halali ya Watanzania? ama kweli kizazi cha nyoka itaendelea kuwa kizazi cha nyoka hadi mwisho wa dunia...
Khaa!!!! ZZK hapiganii uanachama bali anapigania haki itendeke. Siyo mnakurupuka tu kama mlivyozoea mkidhani ndiyo utaratibu. Mbowe, Slaa, Lema na vijibwa vyao walaumie kwa kuua demokrasia nchini
 
nimekupa like nikaona haitoshi mkuu! nimeamua nikuletee nyingine kwa mkono.

Ni kweli...!! Nahisi ni kwa sababu wanapenda huo upumbavu wanaoupost... vivyohivyo na kwa Kabwe wanapenda vitu adimu anavyowapa watanzania.... hope umenielewa...
 
Mchawi wa CHADEMA ni UOngozi wa CHADEMA
Metahli ya "mfa maji haachi kutapa" ndo yanatimia.....
sasa mara CCM mara CUF hivi hata kwa akili ya kawaida hatuwezi kuyaona haya matatizo yaliyopo kwenye uongozi wa juu au tunafumba macho na kushabikia ujinga.....
hakuna mchawi nje ya CHADEMA, mchawi yumo ndani ya kamati kuu na baraza la ushauri wa CHADEMA... mi nashauri wakae chini na kujitathimini ndani ya chama na ikiwezekana matatizo yao wayamalize kwa kushirikisha watu wenye busara nje na ndani ya chama na wenye uwezo wakuona mbali na ikiwezekana Viongozi wapate msasa wa elimu ya Sayansi ya siasa (Political Science.....)
Ninachokiona ndani ya CHADEMA ni Poor management of the Organization... Mtaalamu mmoja wa mambo ya Utawala Maxwell katika kitabu chake cha "The 21indispensable laws of a Leader" anashauri kuwa kama Kiongozi (Leader) unatakiwa kujifunza namna ya kuongoza kupitia migongo wa watu wenye ushawishi katika Taasisi yeyote suala hili kwa CHADEMA naona kama halipo....


Umesema ukweli mkuu lakini unadhani ni nani atakaeye kusikiliza maana viongozi wa juu wote wapo kwenye maslahi zaidi na ukabila ni ukweli usiopingika
 
kasome katiba ya Chama

Kwa uelewa wangu mdogo.... lengo la chama chochote duniani kinachokua ni pamoja na kuongeza wanachama ili kiweze kushinda uchaguzi na si kupunguza wanachama.... sijui kama unalielewa hili?
 
Umesema ukweli mkuu lakini unadhani ni nani atakaeye kusikiliza maana viongozi wa juu wote wapo kwenye maslahi zaidi na ukabila ni ukweli usiopingika

Yap...!! changamoto kama hii siyo ya kuipuzia... ni malalamiko ya muda mrefu.. naamini kurugenzi ya habari imeliona hili na na italifanyia kazi na kufikisha habari hii mahali husika...
 
Ben saa 9 kama kweli yeye si TISS basi atakuwa na mchango mkubwa kwenye kuwachonganisha viongozi wa CHADEMA!

Acha visingizio....!! Kwani ndani ya CDM si kuna kitengo cha Intelijensia.... kazi yake ni nini?
 
Kwa uelewa wangu mdogo.... lengo la chama chochote duniani kinachokua ni pamoja na kuongeza wanachama ili kiweze kushinda uchaguzi na si kupunguza wanachama.... sijui kama unalielewa hili?

haina maana yoyote kuwa chama chenye wanachama wapuuzi kama Zitto
 
haina maana yoyote kuwa chama chenye wanachama wapuuzi kama Zitto

You are rigid bro...!!! Jifunze kuukubali ukweli hata kama unaumiza.... coz kumbukumbu zangu zinaonesha kuwa kuna siku Mbowe aliwahi kumkubali Rais na kumuita Mh. Rais kwa mara ya kwanza baada ya kusema hamtambui baada ya uchaguzi wa 2010.... na siku hiyo alisema hivi "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpe..." hivi ni mtanzania gani aliyeshuhudia jitihada za ZZK anaweza kumuita mpuuzi????
 
You are rigid bro...!!! Jifunze kuukubali ukweli hata kama unaumiza.... coz kumbukumbu zangu zinaonesha kuwa kuna siku Mbowe aliwahi kumkubali Rais na kumuita Mh. Rais kwa mara ya kwanza baada ya kusema hamtambui baada ya uchaguzi wa 2010.... na siku hiyo alisema hivi "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpe..." hivi ni mtanzania gani aliyeshuhudia jitihada za ZZK anaweza kumuita mpuuzi????

upuuzi wa Zitto tunaujuwa sisi CHADEMA. wewe ambaye hujawahi hata kuipigia kura CHADEMA huwezi kujuwa lolote. tuacheni tumalizane naye.

kwa sasa tunatekeleza agizo la Katibu Mkuu: 'msishirikiane naye'
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom