Wewe na Zitto huwa mnapenda kuutumia ule msemo wa shida mwanamandanda kulala na njaa kupenda! Takwimu za facebook unatuletea kwenye siasa? Hata Mr Bean anawashabiki kibao! I wonder Jamii ya watanzania ambao 85% hawana maji, hawana, umeme, hawawezi kumudu mlo mmoja kwa siku wanawezaje kupata access ya internet... Hivi kweli wewe ni mwandishi ama kanjanja kama wale wa uhuru?...How come unajishushia heshima hivi? Ilborians hakunaga wajinga wa aina yako ... "tulijifunza kujitegemea kwa kila kitu ndiyo maana tunasifika mpaka leo"! sifa ya kujikomba ni wewe na Nchemba tu! Hivi kweli Pasco unawezaje kuipigia debe CCM yenye kufanya ujangili kwa Raia na Wanyama? CCM yenye Kuuza na kuingia mikataba ya kudhulumu mali za Watanzania? CCM iliyoshindwa kuwapatia wananchi maji, elimu, huduma za afya, barabara, reli, ndege, ajira, amani, utulivu na mshikamano?...Mnaendekeza siasa za kuwabagua watu wa kaskazini wakati mmesomea huko, mmefundwa huko, mmeoa huko, mmefundishwa maisha huko? Sasa hivi Kaskazini mnayoibagua kwa misingi ya ukabila na dini tayari Allah S.W.T kawaongezea Uranium, Mafuta na Gesi! mbali na mbuga za Wanyama, Milima mirefu, bandari, maziwa na zaidi ya yote WATU WENYE AKILI...Pasco et kumbukeni kuwa "mchimba kisima siku zote huingia mwenyewe" Dhambi hii ya ubaguzi lazima itawarudi mkiwa hai...mark my word...Nguvu za vyombo vya dola wala Mahakama haitafua dafu mbele ya nguvu ya umma!... Badala ya kutumia nguvu kubwa kupigania maslahi ya waalimu, wafanyakazi, wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyabiashara, kukataa kupandishwa kwa bei ya umeme, kukataa rasilimali zetu zisimilikiwe na wageni 100% . Mnatumia mabilioni kuidhoofisha CDM ambayo inapaa kwa uwezo wa Rabuka... Lazima mtambue kuwa kamwe hamtaweza kugeuza mchana kuwa usiku ... kun faya kun...