Mkapa ni miongoni mwa viongozi wa ccm ambao wamekuwa wakilitaja jina la mwalimu ili kujipatia manufaa binafsi.
Ukitazama kwa makini utaliona hilo, na ndio maana utaona hakuna serikali yoyote inayoshughulika na MNF, kuanzia kwa mkapa hadi kikwete ili ihakikishe kwamba MNF inafanya kazi ilizokusudia kulifanyia taifa hili kama ilivyoanzishwa na mwalimu Nyerere mwenyewe.
Kama wangekuwa wanamuenzi bila shaka MNF ingekuwa ni taasisi ya kutegemewa kwa ajili ya masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, na ndipo pangekuwa mahali sahihi pa hawa wastaafu kwenda kujumuika na kusaidia kutekeleza kwa ukamilifu malengo na matarajio ya MNF. Na bila shaka hapo ndipo wangepafanya kisima cha busara, na viongozi wetu mbalimbali, wa serikali, vyama vya siasa na taasisi za binafsi wangeweza kunufaika na kuwepo kwa viongozi wakuu wastaafu, ambao wangesaidia kutoa mwongozo wa namna ya kuiendesha nchi kwa tija.
Sasa kwakuwa wamefanya kusudi kuitelekeza MNF basi ni dhahiri kwamba wote wanaolitaja jina la mwalimu ili kufikia malengo yao ni wanafiki sana tena wanafaa kuitwa 'Wanafiki papa".