Hivi kama kweli Mkapa alikuwa karibu sana na Nyerere - kama anavyotaka watu waamini - alifanya nini katika kuijenga na kuiunga mkono taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa miaka yake kumi alipokuwa Rais? Na hata leo hii amefanya nini - hata kuichangia muda na raslimali zake kuijenga? Maana karibu wengi ambao waliwahi kuwa karibu sana na Nyerere wamekuwa ni wadau wakubwa wa taasisi hiyo.
Isije kuwa ukaribu huu ulikuwepo wakati Nyerere alipokuwa hai tu lakini pia haukuwa ukaribu wa kifikra wa kumfanya akubaliane na malengo na nia za MNF.
Kuhusu Kikwete naelewa kwa nini hayuko karibu na MNF lakini Mkapa kwa kweli sijui.
Alimjengea nyumba nzuri butiama kabla ya hapo alikuwa hana nyumba ya uhakika. Kwani mchango mpaka uupeleke ninyi mnakotaka?