Mchango wa rais kwa CHADEMA ni kujipendekeza?

Feedback

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2011
Posts
7,988
Reaction score
4,515
Gazeti la Mwananchi limeandika kuwa rais Kikwete ametoa mchango wa sh. mil.10 kwenye harambee iliyoandaliwa na Chadema kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu katika Jimbo la Nyamagana ambalo linawakilishwa bungeni na Ezekiel Wenje mbunge kupitia tiketi ya Chadema.

Katika harambee hiyo iliyofanyika juzi jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe, jumla ya Sh47 milioni zilikusanywa.

Wadau hii inatoa ujumbe gani toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.
 
Ikiwa alichanga kama rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hakuna matatizo kwani ni rais wa watu wote bila kujali itikadi wala vyama vya siasa. Ikiwa alichanga kama mwananchi mkereketwa wa maendeleao pia hakuna tatizo kwani hazuiliwi kufanya hivyo. Ila ikiwa alichanga kama mwenyekiti wa CCM kuna walakini.
 
Anatimiza wajibu! Hakujipeleka ikulu kwenda kula bata na kuoa hovyohovyo. Ni kutumikia na kuwapelekea maendeleo wananchi wakiwemo wa Nyamagana. Kwahiyo ametimiza wajibu wake.
 
Ikiwa alichanga kama rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hakuna matatizo kwani ni rais wa watu wote bila kujali itikadi wala vyama vya siasa. Ikiwa alichanga kama mwananchi mkereketwa wa maendeleao pia hakuna tatizo kwani hazuiliwi kufanya hivyo. Ila ikiwa alichanga kama mwenyekiti wa CCM kuna walakini.
Nasikia alipigiwa simu na Zitto ili achange.
 
Ni jambo jema, lakini nadhani kwa kuwa Zito ni rafiki yake na kuwa Zito ndo alikuwa mgeni rasmi, alimuomba rais achangie.

Tunaporudi kwenye suala la maendeleo, tuache ushabiki wa Kisiasa kwani wanaonufaika ni Watanzania na sio CHADEMA, CCM au CUF pekee.

Peoples' Power!!!!!!!, Kidumu Chama Cha Mapinduzi (a.k.a Mafisadi/Magamba), Hakiii Sawaaaa.
 
Gazeti la Mwananchi limeandika kuwa rais Kikwete ametoa mchango wa sh. mil.10 kwenye harambee iliyoandaliwa na Chadema kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu katika Jimbo la Nyamagana ambalo linawakilishwa bungeni na Ezekiel Wenje mbunge kupitia tiketi ya Chadema.

Katika harambee hiyo iliyofanyika juzi jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe, jumla ya Sh47 milioni zilikusanywa.

Wadau hii inatoa ujumbe gani toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.

Watu kweli hamna wema, asingetoa mngesema anawabagua, ametoa mnasema amejipendekeza sasa kwenu jema ni lipi ? na ww umeisha sema ni RAIS, kama hivyo ndivyo, ni Rais wa watu wote bila kujali itikadi zao wakiwemo chadema ndio Rais wao
 
siasa sio uadui ila kwa hili JK anajipendekeza tu

Duh, I can see how JK alivyoharibu nchini kwake. Unaweza kuta kafanya kwa nia njema tu, but ndo hivo tena different definitions zitaletwa..! Pole sana JK, nobody trusts u anymor.:mod::mod:
 
Rais ni wa watanzania wote na Mkereketwa wa maendeleo kwa hiyo alichanga kwa ajili ya maendeleo ya Elimu katika Jimbo la Nyamagana na sio kwa ajili ya CDM, na hii inaonyesha kuwa anatofautisha ukereketwa vyama vya siasa na maendeleo ya nchi.
 
Duh amehaidi hizo milioni 10, ahadi zake amesha anza kuzitekeleza? au ndio......
 
Gazeti la Mwananchi limeandika kuwa rais Kikwete ametoa mchango wa sh. mil.10 kwenye harambee iliyoandaliwa na Chadema kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu katika Jimbo la Nyamagana ambalo linawakilishwa bungeni na Ezekiel Wenje mbunge kupitia tiketi ya Chadema.

Katika harambee hiyo iliyofanyika juzi jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe, jumla ya Sh47 milioni zilikusanywa.

Wadau hii inatoa ujumbe gani toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.

Kama swali la kipimajoto cha itv vile!
 
Adui akikuzidi nguvu patana naye!
Kikwete ameshaona CHADEMA ni maji marefu kwake hivo hana ujanja inabidi apatane nao.
 
teh teh teh ! teh teh teh! mi naangalia tu kama alifanya kama rais basi hongera yake lakini onyo makada wa CCM wasije kulichukulia hili kama mtaji wao wa kisiasa tutawakosoa mara moja lakini vilevile JK mjanja huyo mtu wa pwani keshausoma mchezo kuwa CHADEMA ndiyo watakuwa chama tawala 2015 hivyo anajiandalia mazingira mazuri ya kuheshimika na chama tawala kipya atakapostaafu.
 
Jifunze kuandika wewe. Rais amechngia ujenzi wa shule Nyamagana sio CDM. Halafu ukisema amejipendekeza, kwani Nyamagana Rais wao ni nani? au ni Slaa? Usitake kuwachonganisha wananchi na Rais wao.
 
Rais Haitajiki kutoa pesa mfukoni kwake, hizo ni fedha ambazo amezipata kutoka kwenye kodi zetu,
hivyo mchango hauna tija yoyote ile, tunachokitaka kutoka kwake ni uongozi bora na imara, utakao
simamia maendeleo ya elimu tanzania.

tumempa mamlaka na nguvu kubwa sana za kutekeleza wajibu huo tunataka azifanyie kazi
 
Ikiwa alichanga kama rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hakuna matatizo kwani ni rais wa watu wote bila kujali itikadi wala vyama vya siasa. Ikiwa alichanga kama mwananchi mkereketwa wa maendeleao pia hakuna tatizo kwani hazuiliwi kufanya hivyo. Ila ikiwa alichanga kama mwenyekiti wa CCM kuna walakini.

Bado hakuna walakini wowote kwakua mfuko huo utawanufaisha wana CDM na wasio wana CDM. Kwenye ishu za maendeleo tuweke siasa pembeni
 
Back
Top Bottom