Mchango wa rais kwa CHADEMA ni kujipendekeza?

Nasikia alipigiwa simu na Zitto ili achange.


Majimbo ya Nyamagana, Arusha mjini, Kawe na kule kwa Lissu yanatafutwa na CCM kwa udi na uvumba. Kianzio.... timu ya mukama na Nape walianza heka heka zao za mikutano ya wazi Singida. Huu ni mpango wa kumwaga 'sumu' kwa Lissu maana wanataka kumtoa bungeni at any cost!.

Walio karibu na Wenje, Lissu, Halima Mdee na Lema wajitahidi sana kuziba mapungufu mara yanapotekea (kama yapo). Moja ya mbinu wanayotumia hasa kwa Lissu ni kuwahadaa wananchi kuwa mbunge wao anawatelekeza maana haonekani jimboni mara mara. Tadhali chadema pamoja na kazi kubwa mnayofanya ya kueneza elimu ya uraia msisahau kutembelea majimbo yenu ya uchaguzi mara kwa mara.
 
Kuna jamaa mmoja ali comment kuwa J.K. anaikubali CHADEMA moyoni lakini anashindwa kusema wazi wazi. Nimekubaliana naye maana naona sasa Bwana mkubwa ameshindwa kuvumilia sasa ameanza kuonyesha kwa matendo. Huu ndio uungwa mtu akifanya mazuri hata awe anatoka chama gani CCM msiwe na hofu kuiga. Mkuu wenu ameonyesha njia natumaini mtafuata nyao. Hongera J.K.
Sidhani kama Mh. Kikwete anatatizo. tatizo liko kwenu, jiangalieni na acheni chuki za maji taka. Hao wa nyamagana hata kama hawakuchagua (baadhi) bado Kikwete ni Rais wao kwa hiyo sioni tatizo pia.
 
Hapa mi nasema aksante jk kwa kumega kiasi kiende kwa Nyamagana. Ila ukumbuke pia ahadi hewa ulizotoa bado tunazikumbuka. Usisubiri mpaka 2015.
 
Huu ni ukomavu si kujipendekeza!
KWA NIABA YA JF CONTRIBUTORS NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MCHANGO WAKE!!
ni mategemeo yangu siku ikitokea harambee ya ccm chadema watafanya vivyo hivyo,
Anyhow Ndesamburo alishawahi kutoa harambee ya aina hiyo hiyo kwa ccm
 
Hatakiwi kuchangia cash mane bali kuhakikisha anasimamia idara na wizara husika ktk maendeleo. Alivofanya si sahihi kwani hana huo uwezo wa kuchangia kwa watz wote. Ndo maana wachangiaji wengine wanasema anajipendekeza. Yeye asimamie maendeleo badala ya kuyalinda mafisadi halafu atumie kodi zetu eti anachangia! Huu ni wizi na matumizi mabaya ya kodi zetu! Aaaaaaaaagh!
 
Hatakiwi kuchangia cash mane bali kuhakikisha anasimamia idara na wizara husika ktk maendeleo. Alivofanya si sahihi kwani hana huo uwezo wa kuchangia kwa watz wote. Ndo maana wachangiaji wengine wanasema anajipendekeza. Yeye asimamie maendeleo badala ya kuyalinda mafisadi halafu atumie kodi zetu eti anachangia! Huu ni wizi na matumizi mabaya ya kodi zetu! Aaaaaaaaagh!
regam

You are right mchango wa JK cash money hauna manufaa yeyote zaidi ya kujionyesha, mchango anaotakiwa kutoa ni wa kusimamia majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani mafisadi wanaochota mabilioni na kuyatekeza ambayo yangewekezwa kwenye elimu badala ya yeye kuchangia mil.10.
 
Rais Haitajiki kutoa pesa mfukoni kwake, hizo ni fedha ambazo amezipata kutoka kwenye kodi zetu,
hivyo mchango hauna tija yoyote ile, tunachokitaka kutoka kwake ni uongozi bora na imara, utakao
simamia maendeleo ya elimu tanzania.

tumempa mamlaka na nguvu kubwa sana za kutekeleza wajibu huo tunataka azifanyie kazi
We lazima ni mjumbe
 
Back
Top Bottom