Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,642
- 6,071
Kuhusu mchango wa matibabu ya Mhe. Tundu Lissu
Tunaomba kuwataarifu wanachama, wapenzi na wafuasi wa CHADEMA pamoja na watu wote wenye mapenzi ambao wanawiwa kuchangia kiasi (kitu) chochote kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Tundu Lissu, wawe wavumilivu kidogo hadi kesho ambapo Chama kitatoa utaratibu mzima ikiwa ni pamoja na njia zitakazotumika.
Tumelazimika kuratibu suala la matibabu ya Mhe. Lissu ikiwemo kuchangisha fedha kutoka kwa watu wote wenye mapenzi mema, baada ya Bunge kusema haliwezi kugharamia matibabu yake nje ya nchi, ambako CHADEMA tunaamini atakuwa na usalama wa uhakika wakati akipata matibabu.
Tuendelee kumuombea Mhe. Lissu wakati anaposafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi huku tukisubiri chama kitangaze utaratibu wa wananchi kushiriki katika kuchangia matibabu hayo kesho wakati wa mkutano na waandishi wa habari saa 4 asubuhi.
Makene