SoC01 Mchango wa Jamii katika kuboresha Elimu Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Semu Msongole

Member
Jul 19, 2021
16
421
Katika taifa letu la Tanzania, watanzania tumejijengea utaratibu wa kushirikiana katika maswala mbalimbali ndani ya jamii zetu kama kuchangiana harusi, kutoa rambi rambi kwenye misiba na kujenga makanisa pamoja na misikiti. Haya yote yanafanyika na yanafanikiwa kutokana na nguvu ya umoja na mshikamano iliyopo katika jamii zetu.

Nguvu hii hii tunayoitumia huku kwenye maswala mengine ya kijamii tukiielekezea kwenye kuboresha elimu na kusomesha wanafunzi waliopo katika jamii zetu tutafika mbali kama taifa. Kuna changamoto nyingi sana katika sekta ya elimu baadhi zikiwa ni changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na chuo kikuu, vitabu vya kusomea mashuleni, usafiri wa wanafunzi na hulka ya kusoma au kwenda shule.

Changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na vyuo vikuu

Kwa kupitia dini zetu na kwa uhamasijaji wa viongozi wa dini zetu tunaweza tukashirikiana katika kusaidia wale wanafunzi ambao tunasali nao katika makanisa na misikiti yetu, wanafunzi hawa wanaweza kuwa wadogo zetu, majirani zetu, wanakwaya wetu, vijana wetu makanisani na wanajumuiya wenzetu. Kama tunaweza kuchangishana katika ujenzi wa makanisa, kurekodi video na audio za kwaya zetu, sherehe mbalimbali za kidini basi hili nalo pia linawezekana.

Kama kila kanisa na msikiti wakiamua kusomesha wale wanafunzi ambao ni waumini wao tu naamini kuwa hakutakuwa tena na wanafunzi watakaoshindwa kwenda kusoma kwa kukosa ada. Kihesabu zaidi ni kwamba kanisa moja likiwa na wanafunzi watano wanaotarajia kwenda sekondari (A level) ambako ada ni 70,000/= Tsh ukijumlisha na michango ya shule inafika 120,000/= Tsh kwa mwanafunzi mmoja wakiwa watano jumla inakuwa 600,000/= Tsh kwa miaka yote miwili inakuwa ni 1,200,000/= Tsh kwa kushirikiana hivi na kufanikisha jambo hili kanisa linakuwa limeokoa maisha ya vijana hawa na kuwapa nafasi ya kufanikiwa kielimu.

Changamoto ya vitabu vya kusoma mashuleni

Katika swala la vitabu vya kusomea mashuleni wazazi na jamii kwa ujumla tumekuwa tukiilaumu serikali kwa kutonunua na kupeleka vitabu vya masomo mashuleni tunasahau kuwa hata sisi binafsi kama jamii tunao uwezo wa kufanikisha hili swala kwa urahisi sana. Katika shule zetu huwa kuna wanafunzi wanaotoka katika familia zenye hali tofauti ya kiuchumi, kama mzazi unauwezo wa kumnunulia mtoto wako simu ya laki 3 basi unaouwezo wa kununua vitabu 20 vya 15,000/=Tsh.

Sawa unaweza usipongezwe wala kushukuriwa kama utakavyotarajia lakini fahamu kuwa kuna maisha ya mwanafunzi mmoja au wawili hapo shuleni utakuwa umeyaokoa cha muhimu ni kuzingatia umuhimu wa msaada utakao toa katika shule anayosoma mwanao au hata mtoto wa jirani yako, wakifanya hivi wazazi watano kutakuwa na vitabu 100 ikiendelea kwa miaka miwili au mitatu hiyo shule haitakuwa tena na shida ya vitabu na kama jamii mnakuwa mmechangia kuleta maendeleo ya kielimu.

Changamoto ya usafiri kwa wanafunzi

Tumekuwa tukishuhudia kila siku namna ambavyo wanafunzi huwa wanateseka katika swala la usafiri wa kwenda shule na kurudi nyumbani. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kama tukishirikiana kwa pamoja wazazi na walezi wa hawa wanafunzi au watoto wetu wanaopata shida hii ya usafiri. Kama wazazi wakikubaliana na madereva hata watano tu wa daladala ambao watakuwa wanawabeba wanafunzi hao kwenda shule na kurudi nyumbani bila kuharibu safari zao za kawaida yaani kama ni gari ya gongo la mboto ibebe wanafunzi wanaoelekea huko huko.

Pia njia nyingine ni ya wazazi kuongea na uongozi wa miji waweke utaratibu kuwa kila daladala litumie safari yake moja ya siku kubeba wanafunzi yaani ikipakia wanafunzi tupu asubuhi basi ikifika jioni muda wanatoka shule hatawajibika yeye kuwabeba tena hao wanafunzi watabebwa na daladala nyingine ambayo haikuwapakia asubuhi, kwa taratibu kama hizi tutakuwa tumeboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi.

Changamoto ya hulka ya kusoma au kwenda shule

Wanafunzi wengi siku hizi hawapendi kusoma na hawapendi zaidi kwenda shule hii inaweza kuwa inasababishwa na ukali wa walimu mashuleni lakini pia husababishwa na ukosefu wa dira ya kielimu kwa wanafunzi. Hapa Tanzania mwanafunzi anasoma darasa la kwanza hadi kidato cha nne na msomi pekee anayemfahamu ni mwalimu wake tu basi hali hii hupelekea wanafunzi wengi kuichukia elimu na kuona hakuna maana ya kusoma. Kama jamii tunaweza kutatua changamoto hii na kubadilisha fikra za wanafunzi kwa kuwa mabalozi wa taaluma zetu kutembelea shule na kuongea na wanafunzi wajue kuwa taaluma zipo nyingi na zinahitaji ufaulu wa masomo gani ili uweze kusomea.

Kama wewe ni daktari, mwanasheria, manager, mwandishi wa habari, engineer ukipata muda tembelea shule yeyote iwe ya serikali au ya binafsi uongee na kupiga stori na wanafunzi waruhusu wakuulize maswali mbalimbali kuhusu taaluma yako, waeleze changamoto ulizopitia katika safari yako ya kielimu wajulishe faida ya kuwa na taaluma kama yako. Wanafunzi wengi siku hizi wamekuwa wakitamani kuwa wasanii wa mziki au waigizaji (sio kwamba ni kitu kibaya) hii ni kwasababu hao ndo watu wanaoona wana mafanikio katika jamii lakini mwanafunzi huyo huyo akijua kuwa ukiwa manager wa Vodacom, CRDB bank au kampuni kubwa kubwa familia yako inakuwa na bima ya kutibiwa hadi nje za nchi, unapewa gari la kazi, unalipiwa nyumba unayokaa ukitaka unasomeshwa na kampuni na vingine vingi tu watoto wetu wakijua haya hawatakuwa tena na wasiwasi na maisha yao ya kielimu watasoma tena kwa bidii mpaka na wao wayafikie mafanikio ya kiwango hicho.

Kwa kumalizia naomba kusema kuwa tukishirikiana kama jamii tunaweza kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya elimu Tanzania, sio lazima tusubirie serikali itufanyie kila kitu mtu binafsi kwa kwenda tu shule na kupiga stori na wanafunzi kuhusu kazi yako inatosha kuleta mabadiliko makubwa sana ya kifikra kwa wanafunzi na kuwafanya waongeze bidii katika masomo yao. Pamoja Tunaweza!​
 
Usiache kuuliza swali, kutoa maoni yako na pia usisahau kupiga kura unapomaliza kusoma makala hii na kuvutiwa nayo.

Jinsi ya kupiga kura: Kama unatumia simu ya mkononi basi sehemu ya kupiga kura ipo juu ya hii coment pale inapoishia makala hii chini yake utaona kuna namba zinasoma ukibonyeza ndo unakuwa umepiga kura. Pia kama unatumia kompyuta sehemu ya kura ipo juu mwanzoni mwa makala hii kona ya kulia utaona kuna namba zinasoma pale ukibonyeza unakuwa umeshapiga kura. Asante 🙏
 
Well said bro, napenda kuongezea hapo in this era what i think ili kuhuisha Mustakabali wa Elimu yetu hususani katika aspect ya wito kwa wanafunzi ni Mifumo ya elimu yenyewe ibadilike "its time we create proffesionals not graduates".

Hivyo kwa ngazi zote (primary-uni) vitu kama sylabus,ethics,na ufundishaji yapaswa imjenge mtoto kujitambua anataka kua nani angali bado mdgo na apewe support kupitia mfumo wa elimu nasio kumvuruga bila kuelewa what he really what.
 
Yeah hilo swala la syllabus kiukweli na lenyewe linahitaji kufanyiwa kazi.
 
Halafu pia kwenye upande wa ukosefu wa vitabu mashuleni kuna baadhi ya wazazi wameshamaliza kusomesha watoto wao au watoto wapo kwenye hatua nyingine ya kielimu kama chuo au sekondari hivyo basi vile vitabu vya shule ya msingi ulivyowanunulia watoto wako kuliko vibaki nyumbani na kuharibika ni bora ukavigawe mashuleni kwa wanafunzi wenye uhitaji navyo tukifanya hivi kama wazazi kila mwisho wa mwaka au mwanzo wa mwaka tukapeleka vitabu mashuleni itasaidia kuboresha elimu nchini.
 
Usisahau kupiga kura kama ukisoma na kuipenda makala hii pia kama una swali lolote karibu kuuliza, na kama una maoni mengine kuhusu mada hii unaweza kuchangia maoni yako hapa
 
Kabisa yaani bila kusahau naomba kura yako hapo mkuu. Natanguliza shukrani .

Jinsi ya kupiga kura ni kwa kubonyeza hizo namba zinazosoma chini kidogo mwisho wa makala hii.. au kama unatumia kompyuta kuna namba utaona zinasoma juu ya makala hii kona ya kulia ukibonyeza hizo namba ndo unakuwa umeshapiga kura tayari. Asante
Kura yangu nimeshapiga mkuu
 
Katika taifa letu la Tanzania, watanzania tumejijengea utaratibu wa kushirikiana katika maswala mbalimbali ndani ya jamii zetu kama kuchangiana harusi, kutoa rambi rambi kwenye misiba na kujenga makanisa pamoja na misikiti. Haya yote yanafanyika na yanafanikiwa kutokana na nguvu ya umoja na mshikamano iliyopo katika jamii zetu.

Nguvu hii hii tunayoitumia huku kwenye maswala mengine ya kijamii tukiielekezea kwenye kuboresha elimu na kusomesha wanafunzi waliopo katika jamii zetu tutafika mbali kama taifa. Kuna changamoto nyingi sana katika sekta ya elimu baadhi zikiwa ni changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na chuo kikuu, vitabu vya kusomea mashuleni, usafiri wa wanafunzi na hulka ya kusoma au kwenda shule.

Changamoto ya ada kwa wanafunzi wa sekondari (A level) na vyuo vikuu
Kwa kupitia dini zetu na kwa uhamasijaji wa viongozi wa dini zetu tunaweza tukashirikiana katika kusaidia wale wanafunzi ambao tunasali nao katika makanisa na misikiti yetu, wanafunzi hawa wanaweza kuwa wadogo zetu, majirani zetu, wanakwaya wetu, vijana wetu makanisani na wanajumuiya wenzetu. Kama tunaweza kuchangishana katika ujenzi wa makanisa, kurekodi video na audio za kwaya zetu, sherehe mbalimbali za kidini basi hili nalo pia linawezekana. Kama kila kanisa na msikiti wakiamua kusomesha wale wanafunzi ambao ni waumini wao tu naamini kuwa hakutakuwa tena na wanafunzi watakaoshindwa kwenda kusoma kwa kukosa ada. Kihesabu zaidi ni kwamba kanisa moja likiwa na wanafunzi watano wanaotarajia kwenda sekondari (A level) ambako ada ni 70,000/= Tsh ukijumlisha na michango ya shule inafika 120,000/= Tsh kwa mwanafunzi mmoja wakiwa watano jumla inakuwa 600,000/= Tsh kwa miaka yote miwili inakuwa ni 1,200,000/= Tsh kwa kushirikiana hivi na kufanikisha jambo hili kanisa linakuwa limeokoa maisha ya vijana hawa na kuwapa nafasi ya kufanikiwa kielimu.

Changamoto ya vitabu vya kusoma mashuleni
Katika swala la vitabu vya kusomea mashuleni wazazi na jamii kwa ujumla tumekuwa tukiilaumu serikali kwa kutonunua na kupeleka vitabu vya masomo mashuleni tunasahau kuwa hata sisi binafsi kama jamii tunao uwezo wa kufanikisha hili swala kwa urahisi sana. Katika shule zetu huwa kuna wanafunzi wanaotoka katika familia zenye hali tofauti ya kiuchumi, kama mzazi unauwezo wa kumnunulia mtoto wako simu ya laki 3 basi unaouwezo wa kununua vitabu 20 vya 15,000/=Tsh. Sawa unaweza usipongezwe wala kushukuriwa kama utakavyotarajia lakini fahamu kuwa kuna maisha ya mwanafunzi mmoja au wawili hapo shuleni utakuwa umeyaokoa cha muhimu ni kuzingatia umuhimu wa msaada utakao toa katika shule anayosoma mwanao au hata mtoto wa jirani yako, wakifanya hivi wazazi watano kutakuwa na vitabu 100 ikiendelea kwa miaka miwili au mitatu hiyo shule haitakuwa tena na shida ya vitabu na kama jamii mnakuwa mmechangia kuleta maendeleo ya kielimu.

Changamoto ya usafiri kwa wanafunzi
Tumekuwa tukishuhudia kila siku namna ambavyo wanafunzi huwa wanateseka katika swala la usafiri wa kwenda shule na kurudi nyumbani. Tatizo hili linaweza kutatuliwa kama tukishirikiana kwa pamoja wazazi na walezi wa hawa wanafunzi au watoto wetu wanaopata shida hii ya usafiri. Kama wazazi wakikubaliana na madereva hata watano tu wa daladala ambao watakuwa wanawabeba wanafunzi hao kwenda shule na kurudi nyumbani bila kuharibu safari zao za kawaida yaani kama ni gari ya gongo la mboto ibebe wanafunzi wanaoelekea huko huko. Pia njia nyingine ni ya wazazi kuongea na uongozi wa miji waweke utaratibu kuwa kila daladala litumie safari yake moja ya siku kubeba wanafunzi yaani ikipakia wanafunzi tupu asubuhi basi ikifika jioni muda wanatoka shule hatawajibika yeye kuwabeba tena hao wanafunzi watabebwa na daladala nyingine ambayo haikuwapakia asubuhi, kwa taratibu kama hizi tutakuwa tumeboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi.

Changamoto ya hulka ya kusoma au kwenda shule
Wanafunzi wengi siku hizi hawapendi kusoma na hawapendi zaidi kwenda shule hii inaweza kuwa inasababishwa na ukali wa walimu mashuleni lakini pia husababishwa na ukosefu wa dira ya kielimu kwa wanafunzi. Hapa Tanzania mwanafunzi anasoma darasa la kwanza hadi kidato cha nne na msomi pekee anayemfahamu ni mwalimu wake tu basi hali hii hupelekea wanafunzi wengi kuichukia elimu na kuona hakuna maana ya kusoma. Kama jamii tunaweza kutatua changamoto hii na kubadilisha fikra za wanafunzi kwa kuwa mabalozi wa taaluma zetu kutembelea shule na kuongea na wanafunzi wajue kuwa taaluma zipo nyingi na zinahitaji ufaulu wa masomo gani ili uweze kusomea. Kama wewe ni daktari, mwanasheria, manager, mwandishi wa habari, engineer ukipata muda tembelea shule yeyote iwe ya serikali au ya binafsi uongee na kupiga stori na wanafunzi waruhusu wakuulize maswali mbalimbali kuhusu taaluma yako, waeleze changamoto ulizopitia katika safari yako ya kielimu wajulishe faida ya kuwa na taaluma kama yako. Wanafunzi wengi siku hizi wamekuwa wakitamani kuwa wasanii wa mziki au waigizaji (sio kwamba ni kitu kibaya) hii ni kwasababu hao ndo watu wanaoona wana mafanikio katika jamii lakini mwanafunzi huyo huyo akijua kuwa ukiwa manager wa Vodacom, CRDB bank au kampuni kubwa kubwa familia yako inakuwa na bima ya kutibiwa hadi nje za nchi, unapewa gari la kazi, unalipiwa nyumba unayokaa ukitaka unasomeshwa na kampuni na vingine vingi tu watoto wetu wakijua haya hawatakuwa tena na wasiwasi na maisha yao ya kielimu watasoma tena kwa bidii mpaka na wao wayafikie mafanikio ya kiwango hicho.

Kwa kumalizia naomba kusema kuwa tukishirikiana kama jamii tunaweza kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya elimu Tanzania, sio lazima tusubirie serikali itufanyie kila kitu mtu binafsi kwa kwenda tu shule na kupiga stori na wanafunzi kuhusu kazi yako inatosha kuleta mabadiliko makubwa sana ya kifikra kwa wanafunzi na kuwafanya waongeze bidii katika masomo yao. Pamoja Tunaweza!​
Umewaza vizuri sana siyo kila mara kutegemea wafadhili kutoka nnje wenye masharti hii nndo maana ya ukombozi wa elimu
 
Elimu ni nini?

Kuna aina ngapi za elimu?

Paragraph yako ya kwanza kabisa hapo juu katika utangulizi nimeipenda sana.

Lakini bahati mbaya leo utu na upendo umetoweka moyoni mwetu pesa ambayo dini au madhehebu yangezitumia kuwagusa wasiojiweza/wahitaji ndo inatumika kuyaneemesha matumbo ya mashehe,mapadri,wachungaji,wainjilisti sanjari na kuwasomeshea watoto wao nje ya nchi kama South Korea, US, Italy, n.k
 
Changamoto ya vitabu vya kusoma mashuleni
Katika swala la vitabu vya kusomea mashuleni wazazi na jamii kwa ujumla tumekuwa tukiilaumu serikali kwa kutonunua na kupeleka vitabu vya masomo mashuleni tunasahau kuwa hata sisi binafsi kama jamii tunao uwezo wa kufanikisha hili swala kwa urahisi sana. Katika shule zetu huwa kuna wanafunzi wanaotoka katika familia zenye hali tofauti ya kiuchumi, kama mzazi unauwezo wa kumnunulia mtoto wako simu ya laki 3 basi unaouwezo wa kununua vitabu 20 vya 15,000/=Tsh. Sawa unaweza usipongezwe wala kushukuriwa kama utakavyotarajia lakini fahamu kuwa kuna maisha ya mwanafunzi mmoja au wawili hapo shuleni utakuwa umeyaokoa cha muhimu ni kuzingatia umuhimu wa msaada utakao toa katika shule anayosoma mwanao au hata mtoto wa jirani yako, wakifanya hivi wazazi watano kutakuwa na vitabu 100 ikiendelea kwa miaka miwili au mitatu hiyo shule haitakuwa tena na shida ya vitabu na kama jamii mnakuwa mmechangia kuleta maendeleo ya kielimu.
Mkuu nakushukuru kwa andiko zuri na tayari nimekupigia kura. Lakini naomba niseme kuwa suala la ukosefu wa vitabu shuleni kwa sasa limebaki histroria. Kipindi cha JK, serikali ilijitahidi kununua vitabu vingi na hadi sasa kuna vitabu tele mashuleni. Tatizo wanafunzi wetu wa siku hizi wameharibiwa na utandawazi pamoja ujuaji mwingi usiokuwa na tija. Wanafunzi wanafuatilia masuala ya kijinga zaidi ya wanavyofuatilia masomo. Ni kama vile wamerogwa. Na wazazi nao ni changamoto. Badala ya mzazi amnunulie mtoto wake kitabu anamnunulia simu ya smartphone.

Mimi pia ni mwandishi wa vitabu vya O-level ijapokuwa sijapabahatika ku-publish vitabu hivi. Nimeandika jumla ya vitabu 12 vya O-level mpaka sasa na vimefikia hatua ya mwisho kabisa ya kwenda kiwandani; ila sijapata mfadhili wa kunisapoti. Tazama sample ya kitabu cha Biology Form IV kwenye attachment. Tunaomba serikali itusaidie sisi wazazalendo ili tuweze kuchapisha vitabu hivi kwa ajili ya watoto wetu.
 
Attachments

  • SAMPLE.pdf
    2.8 MB · Views: 5
Back
Top Bottom