Mchango Mh Joseph Mbilinyi(Sugu) toka amekuwa Mbunge kwa vijana wanao tegemea sanaa kama ajira

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,214
42,087
Wanajamvi, Wasalaam.

Ni ukweli usiofichika kabisa wasanii na wadau wa sanaa Tanzania walikuwa na mategemeo makubwa baada ya kuona mtu ambaye alikuwa kwenye sanaa ya muziki muda mrefu amekwenda bungeni.

Wengi walitegemea Mh Joseph Mbilinyi (Sugu )angekuwa kiungo kikubwa cha wasanii na wasanii au wasanii na wadau wa sanaa hasa muziki.
Kila mtu anajua fika sanaa ya Tanzania ina matatizo mengi ambayo kwa nafasi yake angeweza kuyatatua haraka hasa hii migogoro ya wasanii kwa wasanii au wadau wa sanaa au muziki na wasanii.Lakini kinacho sikitisha zaidi yeye amekuwa akichochea mivutano hiyo kwa kujionesha yuko upande fulani kwa wakwaruzanao,wakati tulitegemea yeye ndio angekuwa msuluhishi mkuu wa hiyo migogoro hiyo jitokeza na kupata suluhu.

Tunajua fika hakuna mwanadamu aliye kamilika na hata hao anao watetea kwenye hiyo migogoro nao wana matatizo yao pia na unaweza kukuta wao ndio chanzo. Tunajua Mh Mbilinyi aliwai kuwa na migogoro na baadhi ya wadau wasanaa lakini asiwafanye wasanii wote nao wawe na migogoro nao bali alitakiwa aoneshe njia kwa kuhakisha ana waunganisha wasanii.

Pia tulitegemea kuona Mh mbilinyi angekuwa wa kwanza kuanzisha mfuko maalum wa wasanii ambao ungetumika kuwaunganisha na kuwasaidia wasanii wakati wa shida hasa wanapo patwa na misiba waache kuwa omba omba.

Hivi Mh mbilinyi hadi sasa kafanya nini kuokoa sanaa hii?Hivi atakumbukwa kwa lipi? Yani hata hili la kutatua migogoro kati ya wasanii na wadau wa sanaa limemshinda? Kwanini asiitwe waziri kimvuli mzigo?

Nilitegmea Mh Mbilinyi ange shirikiana bega kwa bega na waziri Fenela kutatua matatizo yale yanayo weza kupatiwa ufumbuzi kwa haraka at least wasanii na wadau wafaidike na uwepo wake,kinyume chake ameweka siasa mbele na kuona kila mdau au waziri wana nia mbaya na sanaa, na hili analifanya ili kupandikiza chuki wakati anajua fika chuki haijengi.

Naulize tena Mh mbilinyi amefanya nini kwenye sanaa tangu awe mbunge?Bado najiuliza kwanini amekuwa akiwa katisha tamaa wadau wasanaa na kuonesha wao ni wezi na wana wanyonya wasanii. Yeye hadi leo kafanya nini?

T bnolB54YUjgAAAABJRU5ErkJggg==
 
ugonjwa wako unafahamika sana, bilashaka hutaki kujishughulisa kusoma ama kudadisi,
 
Anawalipua wanapora haki na stahiki za wasanii, anapambana mchwa wanaliibia taifa hili kwa kisingizio cha kuwasaidia wasanii, Hakuna mtu yeyote ambaye amejaribu kufungua mdomo wake kuyasema haya...haya kwa machache ndiyo mh.Sugu amefanya.
 
Naulize tena Mh mbilinyi amefanya nini kwenye sanaa tangu awe mbunge?Bado najiuliza kwanini amekuwa akiwa katisha tamaa wadau wasanaa na kuonesha wao ni wezi na wana wanyonya wasanii. Yeye hadi leo kafanya nini?

Mbilinyi hakuchaguliwa na wasanii bali na wakazi wa Jimbo lake. Atafanya anayoagizwa na wapiga kura wake tu. Kwani John Komba wako sio msanii? Vicky Kamata?
 
Mkianza kuuliazana mmefanya nini, na nyie jiulizeni kwanza, familia zenu mmezifanyia nini, ndugu zenu mmewafanyia nini nk!
 
Mbilinyi hakuchaguliwa na wasanii bali na wakazi wa Jimbo lake. Atafanya anayoagizwa na wapiga kura wake tu. Kwani John Komba wako sio msanii? Vicky Kamata?

Hua unanifurahisha na majibu yako ya chap chap halafu yana ukweli mtupu..hebu msindikizie na picha moja mtoa mada!
 
Alichofanya Mbilinyi ni kurekodi nyimbo zenye maudhui ya matusi na kuzisambaza kwa njia ya mtandao akishirikiana na wahuni wenzie.
 
hebu bandika antivirus mixtapes waungwana wasikilize mbunge akimwaga matusi, na nyie misukule wake mnashangilia. Ujinga sana!

mkuu me ninachojua mchango wa sugu ni matusi tuu
 
Mbilinyi hakuchaguliwa na wasanii bali na wakazi wa Jimbo lake. Atafanya anayoagizwa na wapiga kura wake tu. Kwani John Komba wako sio msanii? Vicky Kamata?
Sasa kwanini hujifanya msemaji wa wasanii?
 
Hebu bandika ANTIVIRUS MIXTAPES waungwana wasikilize Mbunge akimwaga matusi, na nyie misukule wake mnashangilia. Ujinga sana!

hebu bandika wewe kwa audio clip za kikwete ukitaka kula lazima uliwe kwanza.

ushazoea kuliwa kama mboga wewe.
 
wewe unasumbuliwa na mimba changa wahi clinic.

Naulize tena Mh mbilinyi amefanya nini kwenye sanaa tangu awe mbunge?Bado najiuliza kwanini amekuwa akiwa katisha tamaa wadau wasanaa na kuonesha wao ni wezi na wana wanyonya wasanii. Yeye hadi leo kafanya nini?

CC Ben Saanane MSALANI
 
Last edited by a moderator:
Mbunge Mbilinyi alichaguliwa na wanajimbo la Mbeya Mjini na sio wana sanaa,kwa hiyo kipaumbele sio kwa wanasanaa bali ni kwa wale waliompigia kura na huko ndiko kuna mchango wake,wabunge hawachaguliwa kwenda kutetea maslahi ya professional zao au kazi zao bali kuwatetea wale walio wachagua kuingia bungeni
 
Anawalipua wanapora haki na stahiki za wasanii, anapambana mchwa wanaliibia taifa hili kwa kisingizio cha kuwasaidia wasanii, Hakuna mtu yeyote ambaye amejaribu kufungua mdomo wake kuyasema haya...haya kwa machache ndiyo mh.Sugu amefanya.

sugu ni waziri kimbulv sio kivuli. kama unakumbukumbu wasanii wamesota na hati miliki mpaka kwenye msiba wa kanumba zito ndo ameazisha mada bungeni kwamba pamoja na kuagwa na watu wengi na alikuwa na mchango mkubwa kafa maskini na ndo ikapitishwa sheria ya kucop na kupest faini ya ml. 50 sugu alikuwa anatoa macho kama shoga kaguswa makario leo hii anatokwa povu
 
Sugu sio mbunge wa wasanii ni mbunge wa wananchi wa mbeya kwani hakuchaguliwa na wasanii
Haya ni majibu ya kitoto. Kila mtu anajua Sugu ni waziri kimvuli wa wizara inayo wahusu wasani?
Hivi uko mbeya waliko mchagua hakuna wasanii?

Hivi alitumwa kupigana bungeni?
 
Back
Top Bottom