Mohamed Mchengerwa (Mb) Waziri anayeacha alama na kutekeleza maono ya Rais Samia kwa vitendo

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,160
1,492
Mohamed Omary Mchengerwa, Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo(Mb), ni moja ya Mawaziri vijana wanaohudumu katika Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluh Hassan. Mohamed Omary Mchengerwa, ni kiongozi mchapakazi, mzalendo, mpenda maendeleo na mtu wa haki.

Kwa walio fanya kazi na Mh. Mchengerwa kuanzia akiwa Waziri Ofisi ya Raisi - Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, watamkumbuka kwa namna ambavyo ameacha alama za uongozi (Uongozi sio Utawala), lakini pia Watumishi wataendelea kumkumbuka kwa namna ambavyo aliweza kushughulikia changamoto za muda mrefu za Watumishi, ni kiongozi anayefikika, anasikiliza na anatatua. Watumishi wanakumbuka namna alivyoweza kutatua matatizo yao kupitia ubunifu wa Sema na Waziri. Watumishi wengi walisikitika saana pale ilipompendeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano kumpeleka Mchengerwa akamsaidie katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Ni ukweli usio na shaka kuwa kwa muda mrefu Tanzania iliacha kusikika ulimwenguni katika tasinia ya utamaduni sanaa na michezo, Wizara pamoja na mashirikisho ikiwa ni pamoja na BMT zilikuwa zimelala, kama kuna Wasanii au timu ilijitahidi kuwakilisha Taifa basi asilimia kubwa ilikuwa kwa nguvu zao.

Mh. Mohamed Omary Mchengerwa toka alipoteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwa kweli tumeanza kuona Tanzania ikirudi kwenye ramani, Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kuwa Tanzania inafunguka kimataifa katika njanja zote Mh. Mohamed Omary Mchengerwa anatekeleza kwa vitendo.

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Taasisi zilizo chini yake sasa zimeamka, zinafanya kazi ya kusaidia Wasanii kusonga kimataifa, kuna mifano michache kati ya mafanikio mengi yaliyofikiwa na Wizara hii kutokana na uongozi makini , ubunifu, weledi, kufanya kazi bila kuchoka wa Mh. Mohamed Omary Mchengerwa pamoja nakushirikiana na wadau mbali mbali

1. Kufuzu kwa Timu ya Wanawake chini ya Miaka 17 (Serengeti Girls) kushiriki kombe la dunia mpira wa miguu itakayofanyika nchini India. Vyovyote itakavyosemwa, lakini ukweli ni kwamba toka tupate Uhuru hatujawahi kushiriki kombe la dunia, ni heshima kubwa saaana, Mh. Waziri, Katibu Mkuu na viongozi wote wa Wizara pamoja na Shirikisho la mpira wa miguu mmefanya kazi kubwa saana ambayo imeipa heshima kubwa saana Tanzania. Kwa Tanzania kushiriki kwenye kombe la dunia kutaleta manufaa makubwa ya kiuchumi. Pongezi kubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa namna ambavyo amebeba jukumu la kuhakikisha Tanzania inafunguka kimataifa, hakika Royal tour sasa inaeleweka. Tutafute namna ya kupenyeza filamu yetu ya royal tour katika mashindano haya., nina imani kubwa na viongozi wa Wizara.

2. Ushindi wa Mwanariadha Alphonce Simbu katika mashindano ya Jumuiya ya madola yaliyofanyika hivi karibuni nchini uingereza ni Ishara tosha sasa Mh. Mohamed Omary Mchengerwa umeamua kwa dhati kuwa Tanzania lazima irudi katika ramani Kimataifa, wote tumeshuhudia ukiwa bega kwa bega na Alphonce Simbu kuanzia kwenye maandalizi mpaka kwenye mashindano nchini Uingereza. Ushindi wa medali ya fedha kwa ndugu Alphonce Simbu ni pamoja na juhudi binafsi na kiu yake ya kupata mafanikio, lakini jitihada za Serikali katika kuhakikisha anawakilisha Taifa akiwa katika hali nzuri na kupata mahitaji yake yote bila shaka yamechangia ushindi huu mkubwa. Yawezedkana miaka ya nyuma Tanzania imekosa medali hizi kwa sababu tu akina Alphonce Simbu wengi walishindwa kufanya maanadalizi ya kina au kukosa fedha za kwenda kushiriki. Mh Mohamed Omary Mchengerwa,tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu uendelee kupambana kuhakikisha Tanzania ina rudi kwenye ramani ya Kimataifa hasa kwenye michezo na sanaa, maana mafanikio haya ya muda mfupi ni imani yako ya dhati katika kuhakikisha unamsaidia Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kuifanya Tanzania isiwe msindikizaji kimataifa.

3. Kwa wale wenye kutazama mbali na wenye kuitakia mema Nchi yetu, watakubaliana nami kuwa kwa sasa Tanzania saana na michezo imekuwa ni ajira kubwa kwa Vijana, uwekezaji mkubwa unaofanywa na makampuni kama Azam, Sports pesa, Mbet etc ni ishara kuwa makampuni haya yana Imani na Mh. Rais, makampuni haya yana Imani na Wizara kwa namna wanavyosimamia sera. Hii ni imani kubwa kwako Mh. Mchengerwa na timu yako kwa namna mnavyomsaidia Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano kusimamia sera kuhakikisha kuwa sanaa na michezo inatoa ajira kubwa kwa Vijana.

4. Kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya mwaka 2012, asilimia 77 ya watu wa Tanzania ni Vijana, Mh. Mchengerwa, Vijana tunaimani na wewe, endelea kusaidia Vijana wa Kitanzania, vipaji vingi viko mitaani havijafikiwa bado. Endelea kupigania muziki wa Tanzania ambao changamoto kubwa ni kushindwa kufikia soko la kimataifa kutokana na uwekezaji mdogo katika tasinia hii, Umebeba matumaini ya Wanamuziki wa Tanzania. Wakati ulipohudhuria tamasha la Tuzo za BET Music Awards katika usiku mkubwa wa Utamaduni ( THE GREATEST CULTURAL EVENTS- CALIFORNIA LOS ANGELS) ulisema lengo ni kujifunza namna bora ya kuupeleka muziki wa Tanzania katika soko la kimataifa, Tamanio lako ni kuona tunakuwa na Tuzo zinazokaribia na hizo, tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu tamanio na kusudio lako la kupeleka muziki wa Tanzania kwenye soko la Kimataifa lifanikiwe, kama Nigeria wameweza kwa nini sisi tushindwe? Kama Wasanii wa Filamu wa Nigeria wameweza kufika soko la Kimataifa kwanini sisi soko la filamu Tanzania linashuka? Mungu yupamoja nawe kuhakikisha unawasaidia soko hili la filamu la Tanzania kuendelea mbele.

Mwisho, Nikupongeze saana Mh. Mohamed Omary Mchengerwa, Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo(Mb) kwa namna unavyopambana kuwasaidia Vijana na Watanzania kwa ujumla. Kuna kipindi wakati wa uwasilishaji wa makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Prof Kitila Mkumbo tarehe 6 Juni, 2022 alisema Wizara ya Michezoumeipa hadhi na heshima kubwa saana, kwa sasa kila Waziri angetamani kuwa Waziri wa michezo, alimaliza Prof Kitila Mkumbo.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu akubariki kwa kazi kubwa unayofanya Mh. Mohamed Mchengerwa
Mungu mbariki Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluh Hassan.
 
Huku kwenye sanaa ,utamaduni na michezo. Anapwaya,inaonekana sio mtu wa michezo,kule alipotoka ofisi ya rais angalau ,alinishangaza eti anaunda kamati kutafuta vazi na melody ya muziki wa taifa kichekesho.

Nchi ina makabila 120 vazi la taifa labda ngozi za wanyama.

Melody ya muziki wa Taifa haitafutwi huja yenyewe tu kama ilivyo kwa lugha ,huwezi kutengenexa lugha,labda computer programming languages.

Huko ni kutumia ofisi vibaya kutumia fund za nchi kulipana posho za kamati inayotafuta bikra wodi ya wazazi
 
Huku kwenye sanaa ,utamaduni na michezo. Anapwaya,inaonekana sio mtu wa michezo,kule alipotoka ofisi ya rais angalau ,alinishangaza eti anaunda kamati kutafuta vazi na melody ya muziki wa taifa kichekesho...
Mkuu Mdukuzii, huyu jamaa ni Mchapakazi , mpe muda, ni very creative.

Kuhusu Melody wa muziki wa Taifa, ni jambo nzuri kabisa, kuna midundo ukisikia tu lazima utajua kuwa huu ni wa South Africa au huu ni mdundo wa Nigeria etc , ni jambo jema hata Tanzania tukawa na Melody yetu.

inayotutambulisha. Tuiamini kamati iliyoteuliwa.
 
Mkuu Mdukuzii, huyu jamaa ni Mchapakazi , mpe muda, ni very creative.
Kuhusu Melody wa muziki wa Taifa, ni jambo nzuri kabisa, kuna midundo ukisikia tu lazima utajua kuwa huu ni wa South Africa au huu ni mdundo wa Nigeria etc , ni jambo jema hata Tanzania tukawa na Melody yetu inayotutambulisha. Tuiamini kamati iliyoteuliwa.
Mdundo wa taifa haupatikani kwa kamati,huja tu wenyewe automatically,vazi la taifa ndio kabisaaa
 
Sawa ndugu yake mchengerwa
Mkuu Championship mbona unanibatiza mambo ambayo hayapo, mimi sina Undugu na Mheshimiwa Mchengerwa ila napenda kazi zake, namna anavyowasaidia Watanzania, namna anavyotumia muda wake kuhakikisha anawaletea Watanzania mafanikio. Mzee tusapoti Viongozi wa namna hii
 
Mama Samia alipomtoa utumishi nikaona kinachofuata ni mauzauza. Anyway alisimamia vyema sana zoezi la watumishi kupanda madaraja na kulipwa mapunjo yao ya mshahara. Naona kuna mengi yatakuja kwenye tasnia y.a michezo na sanaa. Kila la kheri kwake.
 
Hata mimi nina imani kubwa saana kuna mengi yatakuja kwenye tasnia ya michezo na sanaa, kikubwa ni Wasaanii wachangamke kumtumia. Nakumbuka Watumishi walimtumia vizuri kutatua changamoto zao hasa kwenye mambo ya kupandishwa vyeo, madaraja na kulipwa stahiki zao kama ulivyosema darcity . Wasaanii watambue ikija fursa waitumie kabla haijapita
 
Mohamed Omary Mchengerwa, Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo(Mb), ni moja ya Mawaziri vijana wanaohudumu katika Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluh Hassan. Mohamed Omary Mchengerwa, ni kiongozi mchapakazi, mzalendo, mpenda maendeleo na mtu wa haki.

Kwa walio fanya kazi na Mh. Mchengerwa kuanzia akiwa Waziri Ofisi ya Raisi - Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, watamkumbuka kwa namna ambavyo ameacha alama za uongozi (Uongozi sio Utawala), lakini pia Watumishi wataendelea kumkumbuka kwa namna ambavyo aliweza kushughulikia changamoto za muda mrefu za Watumishi, ni kiongozi anayefikika, anasikiliza na anatatua. Watumishi wanakumbuka namna alivyoweza kutatua matatizo yao kupitia ubunifu wa Sema na Waziri. Watumishi wengi walisikitika saana pale ilipompendeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano kumpeleka Mchengerwa akamsaidie katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Ni ukweli usio na shaka kuwa kwa muda mrefu Tanzania iliacha kusikika ulimwenguni katika tasinia ya utamaduni sanaa na michezo, Wizara pamoja na mashirikisho ikiwa ni pamoja na BMT zilikuwa zimelala, kama kuna Wasanii au timu ilijitahidi kuwakilisha Taifa basi asilimia kubwa ilikuwa kwa nguvu zao.

Mh. Mohamed Omary Mchengerwa toka alipoteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwa kweli tumeanza kuona Tanzania ikirudi kwenye ramani, Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kuwa Tanzania inafunguka kimataifa katika njanja zote Mh. Mohamed Omary Mchengerwa anatekeleza kwa vitendo.

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Taasisi zilizo chini yake sasa zimeamka, zinafanya kazi ya kusaidia Wasanii kusonga kimataifa, kuna mifano michache kati ya mafanikio mengi yaliyofikiwa na Wizara hii kutokana na uongozi makini , ubunifu, weledi, kufanya kazi bila kuchoka wa Mh. Mohamed Omary Mchengerwa pamoja nakushirikiana na wadau mbali mbali

1. Kufuzu kwa Timu ya Wanawake chini ya Miaka 17 (Serengeti Girls) kushiriki kombe la dunia mpira wa miguu itakayofanyika nchini India. Vyovyote itakavyosemwa, lakini ukweli ni kwamba toka tupate Uhuru hatujawahi kushiriki kombe la dunia, ni heshima kubwa saaana, Mh. Waziri, Katibu Mkuu na viongozi wote wa Wizara pamoja na Shirikisho la mpira wa miguu mmefanya kazi kubwa saana ambayo imeipa heshima kubwa saana Tanzania. Kwa Tanzania kushiriki kwenye kombe la dunia kutaleta manufaa makubwa ya kiuchumi. Pongezi kubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa namna ambavyo amebeba jukumu la kuhakikisha Tanzania inafunguka kimataifa, hakika Royal tour sasa inaeleweka. Tutafute namna ya kupenyeza filamu yetu ya royal tour katika mashindano haya., nina imani kubwa na viongozi wa Wizara.

2. Ushindi wa Mwanariadha Alphonce Simbu katika mashindano ya Jumuiya ya madola yaliyofanyika hivi karibuni nchini uingereza ni Ishara tosha sasa Mh. Mohamed Omary Mchengerwa umeamua kwa dhati kuwa Tanzania lazima irudi katika ramani Kimataifa, wote tumeshuhudia ukiwa bega kwa bega na Alphonce Simbu kuanzia kwenye maandalizi mpaka kwenye mashindano nchini Uingereza. Ushindi wa medali ya fedha kwa ndugu Alphonce Simbu ni pamoja na juhudi binafsi na kiu yake ya kupata mafanikio, lakini jitihada za Serikali katika kuhakikisha anawakilisha Taifa akiwa katika hali nzuri na kupata mahitaji yake yote bila shaka yamechangia ushindi huu mkubwa. Yawezedkana miaka ya nyuma Tanzania imekosa medali hizi kwa sababu tu akina Alphonce Simbu wengi walishindwa kufanya maanadalizi ya kina au kukosa fedha za kwenda kushiriki. Mh Mohamed Omary Mchengerwa,tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu uendelee kupambana kuhakikisha Tanzania ina rudi kwenye ramani ya Kimataifa hasa kwenye michezo na sanaa, maana mafanikio haya ya muda mfupi ni imani yako ya dhati katika kuhakikisha unamsaidia Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kuifanya Tanzania isiwe msindikizaji kimataifa.

3. Kwa wale wenye kutazama mbali na wenye kuitakia mema Nchi yetu, watakubaliana nami kuwa kwa sasa Tanzania saana na michezo imekuwa ni ajira kubwa kwa Vijana, uwekezaji mkubwa unaofanywa na makampuni kama Azam, Sports pesa, Mbet etc ni ishara kuwa makampuni haya yana Imani na Mh. Rais, makampuni haya yana Imani na Wizara kwa namna wanavyosimamia sera. Hii ni imani kubwa kwako Mh. Mchengerwa na timu yako kwa namna mnavyomsaidia Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano kusimamia sera kuhakikisha kuwa sanaa na michezo inatoa ajira kubwa kwa Vijana.

4. Kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya mwaka 2012, asilimia 77 ya watu wa Tanzania ni Vijana, Mh. Mchengerwa, Vijana tunaimani na wewe, endelea kusaidia Vijana wa Kitanzania, vipaji vingi viko mitaani havijafikiwa bado. Endelea kupigania muziki wa Tanzania ambao changamoto kubwa ni kushindwa kufikia soko la kimataifa kutokana na uwekezaji mdogo katika tasinia hii, Umebeba matumaini ya Wanamuziki wa Tanzania. Wakati ulipohudhuria tamasha la Tuzo za BET Music Awards katika usiku mkubwa wa Utamaduni ( THE GREATEST CULTURAL EVENTS- CALIFORNIA LOS ANGELS) ulisema lengo ni kujifunza namna bora ya kuupeleka muziki wa Tanzania katika soko la kimataifa, Tamanio lako ni kuona tunakuwa na Tuzo zinazokaribia na hizo, tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu tamanio na kusudio lako la kupeleka muziki wa Tanzania kwenye soko la Kimataifa lifanikiwe, kama Nigeria wameweza kwa nini sisi tushindwe? Kama Wasanii wa Filamu wa Nigeria wameweza kufika soko la Kimataifa kwanini sisi soko la filamu Tanzania linashuka? Mungu yupamoja nawe kuhakikisha unawasaidia soko hili la filamu la Tanzania kuendelea mbele.

Mwisho, Nikupongeze saana Mh. Mohamed Omary Mchengerwa, Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo(Mb) kwa namna unavyopambana kuwasaidia Vijana na Watanzania kwa ujumla. Kuna kipindi wakati wa uwasilishaji wa makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Prof Kitila Mkumbo tarehe 6 Juni, 2022 alisema Wizara ya Michezoumeipa hadhi na heshima kubwa saana, kwa sasa kila Waziri angetamani kuwa Waziri wa michezo, alimaliza Prof Kitila Mkumbo.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu akubariki kwa kazi kubwa unayofanya Mh. Mohamed Mchengerwa
Mungu mbariki Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluh Hassan.
moja yanwatu niliowakubali wakiwa utumishi ni mchengerwa na kama kuna mdau ana namba yake naiomba hata nimpongeze kwa kaz nzr anayoifanya
 
Back
Top Bottom