Dr.Magufuli alipolizungumzia suala hili wakati wa kampeni nilidhani anatania.
Lakini amerudia tena ahadi ya kuanzisha MAHAKAMA YA MAFISADI bungeni na kusisitiza kwamba ameazimia kutimiza ahadi hiyo.
Kwa msingi huo basi, kinachofuatia sasa ni serikali kupeleka mswada wa uanzishwaji mahakama ya mafisadi bungeni. Baada ya wabunge kujadili na kupitisha mswada huo, Raisi atausaini kuwa sheria.
Sasa hivi tayari tunayo sheria ya UHUJUMU UCHUMI ambayo basically ndiyo sheria ya ku-deal na mafisadi.
Kwa mtizamo wangu, ili sheria ya kuanzisha mahakama ya mafisadi iwe tofauti na sheria tulizonazo sasa hivi, itabidi iwe na maboresho niliyoyataja hapo juu, na zaidi iwe na chombo chenye MENO cha kuchunguza makosa na rushwa, uhujumu uchumi, na ufisadi, pamoja na kushtaki.
Mapendekezo yangu ni matatu:
Kwanza, PCCP iwe HURU kuchunguza na kupeleka mashtaka mahakamani bila kuingiliwa;
Pili, kinga ya Rais iondolewe ili asitokee fisadi yeyote yule akasingizia kwamba alielekezwa na rais;
Tatu, PCCB iwe na uwezo wa kuchunguza na kushtaki makosa na ufisadi hata uliofanyika kabla ya kuundwa kwa mahakama hii mpya.
cc
Pasco,
Mzee Mwanakijiji,
Mag3,
MsemajiUkweli,
Nyenyere,
Nyani Ngabu,
The Boss,
Nguruvi3