Mchakato Mahakama ya Mafisadi waanza

Mchakato Mahakama ya Mafisadi waanza

Akiianzisha basi aifanye TAKUKURU pia iwe na uwezo wa kushtaki tofauti na sasa wao wanachunguza kisha DPP anaachiwa jukumu la kushtaki.
 
Hivi mafisadi wa Bongo ni wa aina gani hasa mpaka wawekewe mahakama maalumu? Je mahakama zilizopo haziwezi tumika kuendesha kesi zao? Je itabidi pia wateuliwe mahakimu/majaji maalumu kwa ajili ya mahaka hii? Je itabidi wajengewe pia Magereza yao? Yaani nina maswali mengi basi we acha tu!
 
Dar es Salaam. Utekelezaji wa ahadi za Rais John Magufuli unazidi kushika kasi baada ya kuanza kwa mchakato wa kuanzisha mahakama maalumu ya kuwashughulikia mafisadi.

Jaji Kiongozi, Shaban Lila alisema jana kuwa tayari wadau mbalimbali wa haki jinai wameanza kukutana kuangalia namna ya kuanzisha mahakama hiyo kama sehemu ya utekejezaji wa ahadi ya Rais.

Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya kushughulikia mashauri nyeti ya jinai kwa majaji 12 wa Mahakama Kuu ya Tanzania, alisema juzi walikuwa na mazungumzo na Wizara ya Katiba na Sheria kuangalia mfumo wa uendeshaji wa mahakama hiyo.

?Tunaangalia tuianzishe kama mahakama huru au ifanywe ndani ya muundo wetu wa mahakama kwa kuipa kipaumbele maalumu. Lakini tunafikiria zaidi kama ingekuwa ni kitengo maalumu ndani ya Mahakama Kuu kitakachokuwa kikishughulikia mafisadi,? alisema Jaji Lila.

Hata hivyo, Jaji Lila hakutaja muda maalumu utakaotumika kumaliza mchakato wa kuanzisha mahakama hiyo, huku akisema unahusisha wadau wengi na unyeti wake unahitaji maandalizi makubwa.

Jaji huyo bila kutaja takwimu, alieleza kuwa kesi za makosa makubwa ya jinai zinaongezeka nchini ukilinganisha na miaka ya nyuma hasa zile zinazohusu utakatishaji fedha, ugaidi, usafirishaji wa dawa za kulevya, usafirishaji wa nyara za Serikali hasa wanyama hai na mazao yake na ufisadi.

Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose alimpongeza Rais Magufuli kwa kuonyesha msimamo wa kupambana na makosa ya jinai yakiwamo ya dawa ya kulevya, usafirishaji wa nyara za Serikali na utakatishaji fedha.

?Nilikuwa nimeketi bungeni namsikiliza Rais siku alipokuwa akilihutubia Bunge, japo hotuba yake ilikuwa kwa Kiswahili lakini nilipata faraja kubwa nilipomuona akiwa mkali katika masuala hayo,? alisema Balozi Melrose.

Chanzo: Mwananchi

watanzania wote tunajua mafisadi wote wako ccm na hata kama wanasema lowassa ni fisadi sawa yuko mmoja tu alietoka ccm
lakini wengi bado wako ccm na ndio wafadhili wa ccm na wengine ela za escrow zimewaingiza bungeni sasa sijajua atawafunga wenzie au ndo ataishia maneno tu,
 
Hahahaaa hii kitu inanichekesha xana mana ni nzuri ila kuwakamata hao majiz na kuwafunga xaxa ndo itakua mtihani mana ndo hao hao waliomuweka pombe madarakani

Hahahahaaa! Naimagine Jk na Lowassa wakiwa kwenye defender ya polisi....

Ila nahisi km ndoto hivi
 
Mbona Nepi alisema alivyosema mahakama ya mafisadi alimaanisha kuboresha utendaji wa hizi zilizopo?
 
Nina mashaka kama hii mahakama ya mafisadi itaanzishwa,na kama itaanzishwa basi itekelezaji wa majukumu yake utakuwa na mushkeli maana utamtia hatiani huyu na kumuachia huru mwingine kwa makosa yanayofanana.

Kwa kifupi itakuwa na upendeleo kwa kisingizio cha ushahidi haukujitosheleza.
 
Mahakama hii itawahusu walioondoka kwenye chama chetu kama hawakuondoka hao ni watakatifu na haata angekuwa mchafu sana yeye haimuhusu
 
Hahahaaa hii kitu inanichekesha xana mana ni nzuri ila kuwakamata hao majiz na kuwafunga xaxa ndo itakua mtihani mana ndo hao hao waliomuweka pombe madarakani

Hizo xasa, xana pelekeka fesibuku bwana..hii mitoto bana!
 
Hizo xasa, xana pelekeka fesibuku bwana..hii mitoto bana!

Kwa bahati nzur mm hua sio muongeaji sana kma wa kike ww subir uje uone itadili na nan hyo kitu ukitaka tulumbane hpa wte tutakua wa kike xaxa
 
Nahofia isije kuwa mahakama isiyo na meno kama Takukuru. Pia iende sambamba na upitishwaji wa katiba mpya ili iwaondelee marais haki ya kutoshtakiwa wakiwa madarakani na wakiwa wamestaafu ili watu km Ben Mkapa na J. Kikwete wafikishwe mahakamani kwa ufisadi mkubwa walioufanya wakiwa madarakani.
 
pale lumumba hapatabaki mtu ,,,maana yamejaa majamaa pale kazi kuifisadi nchi tu ... mi wamenidhulumu pesa zangu nyingi nikaamua kukimbia

Yale hayahusiki na hii mahakama maana ndy yanayo andaa hii mahakama ila yakihama chama tutayakamata
 

kp25112015.jpg




hahahaha !! kipanya mchokozi sana...
 
Hahahaaa hii kitu inanichekesha xana mana ni nzuri ila kuwakamata hao majiz na kuwafunga xaxa ndo itakua mtihani mana ndo hao hao waliomuweka pombe madarakani

Ukiangalia mapanamapainaweza ikawa ndio hao tatizo ni kwamba wao hawakuanguka signatures wapo waliojifanya vihelehele wa kubebeshwa mizigo kuifikisha sehemu husika hao ndio watakao umia na wakome kubeba vya haramu kwa niaba ya wengine
 
Back
Top Bottom