Mchakato Mahakama ya Mafisadi waanza

Mchakato Mahakama ya Mafisadi waanza

Wenyewe wanasema muhimu sio unayoyazungumza jukwaani, muhimu ni kukamata dola.
 
Kwenye kampeni, wagombea wangekuwa wanawaskiliza wansnchi wanachotaka na sio kinyume chake
 
Wenyewe wanasema muhimu sio unayoyazungumza jukwaani, muhimu ni kukamata dola.

Nakubaliana nawe mkuu, ndio maana hajapata kuonekana tena akipiga push-ups tokea wakati ule.
 
Dar es Salaam. Utekelezaji wa ahadi za Rais John Magufuli unazidi kushika kasi baada ya kuanza kwa mchakato wa kuanzisha mahakama maalumu ya kuwashughulikia mafisadi.

Jaji Kiongozi, Shaban Lila alisema jana kuwa tayari wadau mbalimbali wa haki jinai wameanza kukutana kuangalia namna ya kuanzisha mahakama hiyo kama sehemu ya utekejezaji wa ahadi ya Rais.

Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya kushughulikia mashauri nyeti ya jinai kwa majaji 12 wa Mahakama Kuu ya Tanzania, alisema juzi walikuwa na mazungumzo na Wizara ya Katiba na Sheria kuangalia mfumo wa uendeshaji wa mahakama hiyo.

?Tunaangalia tuianzishe kama mahakama huru au ifanywe ndani ya muundo wetu wa mahakama kwa kuipa kipaumbele maalumu. Lakini tunafikiria zaidi kama ingekuwa ni kitengo maalumu ndani ya Mahakama Kuu kitakachokuwa kikishughulikia mafisadi,? alisema Jaji Lila.

Hata hivyo, Jaji Lila hakutaja muda maalumu utakaotumika kumaliza mchakato wa kuanzisha mahakama hiyo, huku akisema unahusisha wadau wengi na unyeti wake unahitaji maandalizi makubwa.

Jaji huyo bila kutaja takwimu, alieleza kuwa kesi za makosa makubwa ya jinai zinaongezeka nchini ukilinganisha na miaka ya nyuma hasa zile zinazohusu utakatishaji fedha, ugaidi, usafirishaji wa dawa za kulevya, usafirishaji wa nyara za Serikali hasa wanyama hai na mazao yake na ufisadi.

Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose alimpongeza Rais Magufuli kwa kuonyesha msimamo wa kupambana na makosa ya jinai yakiwamo ya dawa ya kulevya, usafirishaji wa nyara za Serikali na utakatishaji fedha.

?Nilikuwa nimeketi bungeni namsikiliza Rais siku alipokuwa akilihutubia Bunge, japo hotuba yake ilikuwa kwa Kiswahili lakini nilipata faraja kubwa nilipomuona akiwa mkali katika masuala hayo,? alisema Balozi Melrose.

Chanzo: Mwananchi

mark my words.......this is bullshit,
 
Kwanza tujue ni ya mahakama
ya Aibu (shame ) au majipu ?? Kama ni ya mafisadi List of shame Ccm watakuwa 99%

Tutasikia mengi?
 
Back
Top Bottom