Mch. Peter Msigwa, kwa hili tukio la Mbowe nenda katubu kwa uzushi wako kama kweli wewe ni mtumishi wa Mungu

Maneno yangu ni machache tu kwako na najua upo humu na utaupata ujumbe huu.

Wewe kama mtumishi wa Mungu tena mchungaji kabisa ulichokifanya si haki mbele za Mungu.

Umeeneza uzushi kwamba mh Mbowe alishambuliwa na watu walio mshambulia walikuwa wanatamka maneno "wewe ndio unamsumbua Rais tumekuja kukuvunja ili tuone utafanya vipi kampeni"

Maneno haya umeyatoa wapi??
Ulikuwa na dhamira gani kuongopa namna hii?

Mbowe alikuwa peke ake wakati anashambuliwa kama mlivyo dai sasa wewe haya maneno ulitoa wapi??

Yalirekodiwa na nani hadi wewe ukayasikia??

Mch nenda katubu kwa hili na uwaombe radhi waumini wako kwa hili ulilofanya.

Alafu hizi tabia uziache hazifai kumbuka uliwahi kumsingizia mzee Kinana kuwa ni jangili kwa masilahi yako ya kisiasa na ukakiri mwenyewe kwa ulimi wako leo tena kwanini unafanya kosa lilelile??

Nenda katubu na uombe radhi waumini wako.
Pia alidanganya yupo karantini Dodoma kumbe amekuja Dar kula bata.
 
Back
Top Bottom