Mbowe kwa kujua au kutokujua ameamua kuitumia Ibada ya Sadaka ya Shukrani kama sehemu ya mkutano wake wa siasa

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
FREEMAN MBOWE UMEANZA TENA

Leo jumapili Terehe 20/03/2022 Mwenyekiti wa chadema Ndugu Freeman Mbowe aliungana na familia yake na wafuasi wake kutoa sadaka ya SHUKURANI katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini, ushariki wa Nshara machame

Kuna baadhi ya mambo yamenza kuonekana ambayo hayana dalili nzurii tuendako

1. Mbowe kwa kujua au kutokujua ameamua kulitumia tukio la sadaka ya shukrani kama sehemu ya mkutano wake wa siasa, akiwa na kundi la wanachama wake waliamua kwa makusudi kabisa kuvaa sare za chadema na wengine kuvaa kofia zisizo rasmi kanisani na kufanya ibada ambayo mavazi yao hayakuwa ya uchaji Mungu zaidi ya mavazi ya mikutano ya kisiasa (tazama ushahidi wa picha chini)

Tazama kianbatanisho cha picha za kanisani na nje ya lango kuu la kanisa

Mytake
1. Hivi leo mwenyekiti wa CCM Mhe Rais Samia Suluhu Hassan akisema anakwenda kutoa sadaka ya SHUKURANI msikitini na kuchukua maelfu ya wanachama wa CCM hivi dunia itasema nini?

2. Mbowe asidhani Mhe Rais Samia hajui anachofanya, narudia kusema acha wakati utaongea

USHAURI KWA KANISA KKKT
1. Askofu Mkuu wa kkkt Tanzania Dkt. Shoo ambae pia ni askofu wa dayosisi ya kaskazini ambako tukio hili liketokea leo tunaomba ujitafakari sana na mwenendo wa Mbowe ambae siku zote amekuwa akilitumia kanisa vibaya

-Mkuu wa jimbo la Hai Mchungaji msomi Biniel Maliyo usikubali jimbo lako kutwezwa na kutumiwa na wana siasa hata kama kuna shinikizo kutoka kwa Askofu wako simama katika
nafasi yako mana vyeo huja na kupita ila utukufu wa Mungu upo

- Sijawai kuona Mhe. Mbunge wa Hai Saashisha Mafuwe akienda kanisani na wanachama wa ccm wakiwa wamevaa nguo za kijani leo iweje tukio hili liwezekane kwa chadema ibadani?

2. Mbowe amekuwa akitumia kivuli cha kanisa kufanya siasa za hila mfano alipotoka gerezani alikwenda kanisani KKKT usharika wa Azania front na kuongea maneno ambayo hayakuwa ya kimadhabauni at all

3. Askofu Shoo anapaswa kutambua miongoni mwa waumini wa kkkt wapo pia wa vyama vingine leo ccm wakiamua kwenda kusali na mavazi ya kijani itakuwaje si ni vurugu?

USHAURI KWA MBOWE
Huu ni wakati wako wa kutulia na kutafakari hatima ya maisha yako kisiasa na kifamilia, unapotoka katika changamoto kubwa unashauriwa ujipe muda wa kutulia na kutafakari sana mana ni katika kipindi hiki unaweza kufanya mambo ya ajabu zaidi ukawa kituko zaidi, jipe muda tulia tafakari

USHAURI KWA WASAIDIZI WA RAIS SAMIA
Naomba mumshauri Mhe Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na dhamira yake nzuri ta kutengeneza mazingira wezeshe ya kufanya siasa nchini atambue wako binadamu kamwe hata ukiwatengeneza mazingira mazuri watayaharibu wenyewe kwa makusudi, ni wakati sasa wa Mhe Rais kuwa macho na watu wasiolitakia taifa mema.

Nyuki kamwe hakumbatiwi

Makala na
Mangi kiongozi
Narumu machame
20/03/2022

IMG-20220320-WA0369.jpg


IMG-20220320-WA0370.jpg


IMG-20220320-WA0368.jpg


IMG-20220320-WA0367.jpg
 
Mkuu, mimi nikuulize swali moja tu.

Kuna sheria yoyote iliyovunjwa hapo.

Ukisema, NDIYO, basi nakusihi usimlilie Mama Mzinguo, wahimize wanaotakiwa kusimamia sheria hiyo wachukue hatua.

Watu kama nyinyi ndio mnaoleta shari ndani ya nchi hii kwa kutozingatia matakwa ya sheria zilizopo, badala yake mnakimbilia Mwenyekiti wa CCM atunge sheria zake kukidhi mahitaji yenu. Ndiyo maana wengi wenu mlimpenda sana yule shetani.
 
Kama anaendelea na Siasa zake za kumdhihaki na kumdhalilisha Magufuli (RIP) hafiki popote labda tu kama anatafuta Ubunge wa Hai lkn kama ni kwa Tanzania nzima, no chance!
 
FREEMAN MBOWE UMEANZA TENA

Leo jumapili Terehe 20/03/2022 Mwenyekiti wa chadema Ndugu Freeman Mbowe aliungana na familia yake na wafuasi wake kutoa sadaka ya SHUKURANI katika kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini...
Taja na sare rasmi za kuvaa kanisani! Unashauri upuuzi Kwa rais!

Kwa kuvaa sare za chama kumevunja sheria ipi ya nchi?

Ndio maana unatoka narumu wasikojitambua!
 
Sisi rutheran tunafikiria sadaka tulizo pata nita kusifu sana sana kama uta mshauri Mama samia alete sadaka yake rutheran,

ila hata msikitini sawa,Mbowe kaenda katika kigango chake kwao kijijini na wala sio tukio kubwa kikanisa shoo niaskofu wa dioceses hiyo kipi kibaya.

Rutheran wanajenga miradi yao kwa asilimia themanini kwa michango ya waumini
 
Kuna watu hawana shukrani, mama asipoangalia atapata tabu na uraisi atauona mgumu sana.

Amuulize mkwere walivyomsumbua kwa vijisababu vya kipuuzi kila siku.

Kuna watu hawahitaji kuchekewa hata sekunde.....watakusumbua mno

Katika hili jpm alinifurahisha sana, ilikuwa anawatwanga mabanzi tu kila wanapotaka kumsumbua na hatimaye akafanya mambo yake kwa uhuru kabisa.

kama kuwaacha huru wapinzani wafanye watakavyo ndiyo maendeleo, basi tungeendelea sana kipindi cha kikwete, lkn ona sasa nyuzi za kumpondea kilwete kila siku.

Kama kupewa uhuru ndiyo kupendwa na kuheshimiwa na kina mbowe na genge lake, basi kikwete wangemheshimu sana lakini hebu kumbuka jinsi walivyomdhalilisha.

Hapo siku si nyingi atawaita na wale misukule‐viongozi wake waliopo kule nje waje waungane na kumsumbua huyu mama yetu.......linakuja hili.

Kuna maaana gani kumchekea mtu anayekuharibia kila ufanyacho, tena kwa makusudi?!!!

Hao jamaa sio; ukicheza na mbwa atakufuata msikitini!!!
 
Kama ww ni mwanaccm mwenzangu utafute hoja za msingi uje nazo kwani zaidi sana unakiabisha Chama changu kwa kutokuwa mvumilivu wa matukio pia una wivu.

Ila kwa Chadema kwa hali ilivyo kwa sasa tutakuwa na kazi ngumu huko mbeleni tukumbuke tuliwajenga wenyewe tuwaache wafanye mikutano kama ni kuchokwa wachokwe na Wananchi sío Chama chetu.

Mwenyekiti mstafu Kikwete alitupa tahadhari mapema lakini hatukumsikia kwa hiyo tuwe na uvumilivu kidogo
 
Kuna watu hawana shukrani, mama asipoangalia atapata tabu na uraisi atauona mgumu sana. Amuulize mkwere walivyomsumbua kwa vijisababu vya kipuuzi kila siku. Kuna watu hawahitaji kuchekewa hata sekunde..
Hoja hujiwa kwa hoja sio miguvu
 
Rais wetu anazo akili kubwa kuliko unavyomdhania.Huo Ushauri wako kwa Rais wetu,Kama marehemu Mzee Mkapa angekuwa yupo hai,angekushushua kwa kukuambia kwamba,hUO Ushauri wako Ni umbea wa kikee.

Kakojoe ulale. Mbona Magufuli Kila J2 Alipokuwepo Dodoma au Chato au St Peters DSM,Alikuwa anapanda kwenye Mimbari na kuhutubia Siasa naWewe ikawa husemi au ku-Comment chochote.Acha kukereka mkuu.
 
Muda ni Mwl mzuri. Huyu gaidi lazima afungwe tu.
Muda (wote) hauwezi kuwa wa upande mmoja hata siku moja. 'Muda' huo huo unaoutegemea wewe unaikeketa CCM, bado hili hulijui?

Najuwa nimepoteza muda wangu kukujibu wewe, lakini potelea mbali, si neno.
 
Tumeshafika sehemu ya kuwapangia watu wavae vipi kwenye makanisa yao na imani zao! Kila mtu ana uhuru wake na kanisa lina sheria zake. Rais Samia naye atafanya kwa imani yake.
 
Haya ni mawazo yaliyojaa hila na tamaa za kuendeleza udikteta wa CCM wa chama kimoja. Mungu hakupendezwa na hila zenu, kiongozi wenu Magufuli akafariki lakini bado mna hangover.

Tunataka katiba mpya
 
Back
Top Bottom