Chimunguru
JF-Expert Member
- May 3, 2009
- 10,678
- 4,377
Mh jamani hapa kuna usanii unatembea, mie nilikuwa simwamini huyu DR. na Mbunge wetu, wife wangu alikuwa anapenda kwenda kwa maombezi huko mikocheni, alipenda kwenda kuombewa kwenye hilo kanisa, mie sijawahi kwenda hapo na sikuwa na mpango wa kwenda kabsaa. Mwaka jana mwezi kama wa saba hivi wife alimpeleka mtoto wetu akaombewe maana alikuwa anatatizo sana la kukataa kula. mara nyingi nilikuwa namwambia wife kwamba pale ni imani yako ndo inakuponya, lkn si uwezo wa yule mama, wife alikwenda pale alikutana na mmoja kati ya wale wachungaji wawili wa kiume ambao mara nyingi hounekana na yule mama MBUNGE, kilichotokea yule mchungaji akaanza KUMTONGOZA wife, kwa kweli wife alishtuka sana akauliza hii ndo huduma ya mungu mnayosema mnatoa hapa? yule mchungaji akatetemeka akaomba msamaha, wife akageuza hapo akanipigia simu nikamwambia, I TOLD YOU HOME GIRL! kweli pale ni pure bizness, wengi wetu tunaenda sali kwenye haya makanisa tukiwa na SHIDA, pale mchungaji atakujaza woga na ile shida yako basi utaamini kila kitu. Nilienda kwenye kanisa Moja mbezi, mchungaji alisisitiza sana fungu la kumi, tena sana hata sisi wakatoliki huwa hatukamuani namna ile DAH!