Mch. Gwajima amgomea Makonda

Mch. Gwajima amgomea Makonda

Inafuatana na nafasi yake katika jamii! Hata anaemhoji ni mtu mwenye cheo! Na katika hili ni zaidi ya yale aliyoyatamka kuna lingine nyuma yake!
 
Hakuitwa na Kova bali aliitwa na jeshi la polisi kupitia kamanda Kova kwa mujibu wa sheria...

Mbona kamanfda Kova hana muumini wala mfuasi wake hata mmoja mbona alipomwambia Gwajima aende kuripoti kwake mbona Gwajima alienda mbio tena kwa miguu baada ya kuona foleni ya magari inamchelewesha?
Kwenye mambo ya NGO mkuu wa wilaya ana nguvu kuliko Kamanda KOVA.

Gwajima anachezea moto.Hamjui mikuu wa wilaya ni nani anadhani naye ni mmoja wa hao misukule wake.Shauri yake wale mnaomuunga mkono asiende msije kuja kupiga yowe hapa tena kulalamika
 
Makonda alimwita Gwajima maksudi akijua kuwa Lazima Gwajima atakaidi Amri ili yeye apate Sababu ya kumtoa nduki kule kawe, Gwajima uwe makini na hilo.

Adhabu ya kutokufika (kuitikia wito) kwenye kikao siyo kufukuzwa wala kufutiwa usajili wa NGO. Ni makosa makubwa kumuogopa kwa njia ya kumuabudu binadamu, inakuwa mbaya zaidi mtu mwenyewe anapokuwa Makonda.
 
Gwajima kachemka.Mkuu wa wilaya aweza futa au omba NGO fulani ifutwe au isifanye kazi wilayani kwake.hajui role ya mkuu wa wilaya kwenye NGO? ASUBIRI MUZIKI WAKE

hivi gwajima ana miliki NGO au jumba la ibada..hakuna sehemu mkuu wa wilaya anaweza kufuta kanisa LA bwana,coz yeye hatowi usajikibwa makanisa.
Kanisa sio NGO ndugu
 
Jamaa jeuri ila muache aendeleze jeuri atapata anacho kitafuta
 
Binafsi sidhani kama Mch. Gwajima amekurupuka katika kauli yake. Nadhani kuna jambo na ndo maana amegoma kwenda kwa Kamati inayoongozwa na Makonda. Ikumbukwe kuwa Makonda Mwenyewe hana nidhamu kwani kipindi fulani aliwahi kuporomosha mvua ya matusi kwa viongozi wetu lakin hakuna Jeshi la Police wala Kamati ya ulinzi na usalama iliyomwita kumuhoji.
Sheria za nchii zina macho kama ya Kova.

Ahsante sana kwa kauli hii [maandishi mekundu]...umeniguza saana na hadi sasa hacheka kwa jinsi ulivyoutoboa ukweli huu!...'...a.k.a...'squinted laws'
 
Kuna masharti na mambo ambayo NGO ikiwemo hiyo ya Gwajima inabidi iyafanye au izingatie katika utendaji wake ikikiuka yaweza futiwa usajili mkuu wa wilaya akiita sio wito mdogo.Kuhojiwa na polisi hakuondoi yeye kwenda kwa mkuu wa wilaya.Mkuu wa wilaya ana kazi zake kuhusiana na NGO na polisi wana kazi zao kuhusiana na mambo ya kazi zao.
Ndio maana nimekuuliza alifute kanisa kwa kosa lipi, unajua madhara ya kufuta kanisa au migogoro ya dini unaisikia redioni tu?

Kanisa la Gwajima lina mizizi yake na lipo pale kwa muda mrefu nafikiri inaweza kuwa hata kabla Makonda hajaanza shule ya msingi, jiulize ni ma dc wangapi wamelikuta na kuliacha kwani Makonda anawazidi nini.

Uongozi sio power pekee ni pamoja na busara akijifanya 'much know' atakosana na wengi sana.
 
Kova sawa! Lile ni jeshi la polisi ambalo linafanya kazi chini ya sheria inayoliongoza! Huyu D.C. ana mamlaka gani ya kufanya hivyo? Huo ni ulevi wa madaraka na kutokutumia akili!

Mkuu wa wilaya yuko kisheria na polisi unajua huwa wanampiga salute.
Mkuu wa wilaya ndiye raisi wa wilaya.Gwajima yuko chini ya raisi wa wilaya Makonda.
 
Ndio maana nimekuuliza alifute kanisa kwa kosa lipi, unajua madhara ya kufuta kanisa au migogoro ya dini unaisikia redioni tu?

Kanisa la Gwajima lina mizizi yake na lipo pale kwa muda mrefu hata Makonda hajaanza shule ya msingi, jiulize ni ma dc wangapi wamelikuta na kuliacha kwani Makonda anawazidi nini.
Kama linatakiwa kufutwa au la lina makosa au halina aende kwa mkuu wa wilaya anayemwita atayajua huko.
Ndio maana anatakiwa kwenda kusikiliza anachoitiwa.Jeuri ya kukataa ina madhara yake tena makubwa mno.Kufuta Kanisa hata kama lina mizizi hadi wapi sio issue.Sawa limekuweko miaka yote lakini halikuwa na matatizo hiyo miaka mingine.Kanisa kama binadamu laweza badilika laweza kuwa malaika lakini baadaye likageuka ibilisi
 
Duuh hajui huyo ni milinzi wa amani aka mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, ila nchi hii kuna baadhi ya watu wana raha wakitoa maneno yanayodhaniwa yamemkashifu mtu mwingine wanachoambiwa waende kituo cha polisi wakaripoti wenyewe lakini wengine utatafutwa kwa marungu au hapo hapo unapotoa hayo maneno unazuiwa na kufunguliwa mashitaka.

Mkuu unachosema ni kweli, hii nchi ina "waheshimiwa" na wasio "waheshimiwa" haya matabaka nyerere aliyapinga sana na kulikuwa na neno "ndugu". ambalo lilionyesha wote tupo sawa. Tafsiri ya kuwa na mheshimiwa maana yake kuna mtu ambaye hastahili heshima ie yule ni mheshimiwa ila wewe/mimi siyo mheshimiwa.
 
Mkuu wa wilaya yuko kisheria na polisi unajua huwa wanampiga salute.
Mkuu wa wilaya ndiye raisi wa wilaya.Gwajima yuko chini ya raisi wa wilaya Makonda.
Kuwa mkuu wa wilaya sio warranti ya kutenda mambo kilevi yasiyofuata sheria hata yeye yuko chini ya sheria lazima afuate utawala wa sheria rule of law.
 
hivi gwajima ana miliki NGO au jumba la ibada.
Kanisa sio NGO ndugu

Serikali haina dini haisajili makanisa wala misikiti huwa inasajili NGO.Hicho mnachoita kanisa la Ufufuo na Uzima Serikalini imesajiliwa kama NGO tu wala si kanisa.Huyo anayeendesha ndio anajua ni kanisa serikali inajua ni NGO yaani kiswahili shirika lisilo la kiserikali lililoko viwanja vya kawe linalolikana jina kama kanisa la ufufuo na uzima.Linawajibika kwa mkuu wa wilaya kama NGO.
 
Kuwa mkuu wa wilaya sio warranti ya kutenda mambo kilevi yasiyofuata sheria hata yeye yuko chini ya sheria lazima afuate utawala wa sheria rule of law.

Gwajima kaitwa kisheria jopo la kamati ya ulinzi na usalama la wilaya lenye wajumbe kama 20 linamsubiri hajaitwa na makonda kama makonda
 
Gwajima kachemka.Mkuu wa wilaya aweza futa au omba NGO fulani ifutwe au isifanye kazi wilayani kwake.hajui role ya mkuu wa wilaya kwenye NGO? ASUBIRI MUZIKI WAKE

Lakini hawezi kuifuta ndani ya mioyo. Muziki huu Makonda hauwezi! Ni mkurupukaji tu siku zote.
 
Makonda anataka kumpiga Gwajima ili azawadiwe ukuu wa mkoa. Alimpiga Warioba akapewa u-DC
 
Gwajima kachemka.Mkuu wa wilaya aweza futa au omba NGO fulani ifutwe au isifanye kazi wilayani kwake.hajui role ya mkuu wa wilaya kwenye NGO? ASUBIRI MUZIKI WAKE
mwambie basi alifute kanisa la Gwajima kama yeye ni kidume!!
 
Unamaanisha kanisa la Gwajima ni NGO!!!! You must be kidding!
Gwajima kachemka.Mkuu wa wilaya aweza futa au omba NGO fulani ifutwe au isifanye kazi wilayani kwake.hajui role ya mkuu wa wilaya kwenye NGO? ASUBIRI MUZIKI WAKE
 
Back
Top Bottom