Mbweni inapendelewa ujenzi wa barabara, Mbezi kwa miaka nenda rudi barabara hazijengwi

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,327
24,209
Majuzi nimepita Mbweni nikashangaa kabisa.

Barabara nyingi zilizokuwa hazipitiki sasa ni lami tupu.

Najua huu ni mkakati wa viongozi wengi kujipendelea maana wengi wamejenga huko.

Nimepata tetesi kuwa hata kwa Katibu Mkuu Kiongozi, watu wameamriwa barabara iendayo kwake iwekwe lami.

Tofauti na Mbweni, huku Mbezi Beach barabara za kwenda makazi ya watu hazijashughulikiwa kabisa.
Barabara za NSSF Flats
Barabara za Jogoo Cotex
Barabara za Mbezi Tangi Bovu
Barabara ya Mbezi 5 Star
Barabara ya Ndumbwi-Baraza la Mitihani
Barabara za chini Kwa Lukuvi

Ila barabara ya kwenda kwa Kikwete Kawe Beach ilijengwa chap chap!

Huu upundeleo dhahiri wa viongozi kujinufaisha Awamu hii!
 
Kaka nenda jimbo la ukonga ndio utaona maajabu ya dunia, wakati sehemu nyingine wanang'oa lami na kuweka nyingine, huko hata vifusi haviwekwi,kipindi cha mvua watu wanatamani kutorejea majumbani! hi keki ingegawanywa hata wapate "karobo" hao wakubwa wachukue robo tatu ila sio kulamba asali yote🙆‍♂
 
kaka nenda jimbo la ukonga ndio utaona maajabu ya dunia, wakati sehemu nyingine wanang'oa lami na kuweka nyingine, huko hata vifusi haviwekwi,kipindi cha mvua watu wanatamani kutorejea majumbani! hi keki ingegawanywa hata wapate "karobo" hao wakubwa wachukue robo tatu ila sio kulamba asali yote🙆‍♂
Sehem kubwa ya ukonga haijapimwa. Unataka serikali iingie gharama ya kuvunja nyumba za watu mje kulalamika hapa kuwa mnaonewa. Anzeni kuvunja nyumba zenu tengeni sehem ya barabara alafu iteni serikali muone kama hamtajengewa lami.
 
Inawezekana ndio wanatengeneza eneo la wazito kama ilivyo Oysterbay na Masaki, lazima ujenzi wake ufanyike kwa haraka ndio maana unashangaa.

Huko Mbezi kwenu unapotaka patengenezwe hakuna tofauti na maeneo mengine ambayo yamesahaulika nchi hii, au yanaendelezwa taratibu.
 
Nakumbuka miaka ya mwisho ya 90s na mwanzo wa 2000s kuna wakazi kadhaa wa maeneo ya Kimara nyumba zao zilipigwa X kupisha ujenzi wa barabara serikali ikawapimia viwanja Mbweni kama fidia.

Wakapaona maporini hawakwenda kuviendeleza na wengine wakavitelekeza. Wachache sana walienda kishingo upande. Hao wachache walichekwa saaana. Magu alivyoingia madarakani na kuwabomolea ili kutanua barabara wakaanza kumchukia. Sasa hivi Mbweni pamekua hot cake! Kupanga ni kuchagua.
 
Inawezekana ndio wanatengeneza eneo la wazito kama ilivyo Oysterbay na Masaki, lazima ujenzi wake ufanyike kwa haraka ndio maana unashangaa.

Huko Mbezi kwenu unapotaka patengenezwe hakuna tofauti na maeneo mengine ambayo yamesahaulika nchi hii, au yanaendelezwa taratibu.
Obay yenyewe bado kuna barabara ziko ovyo..mfano ile haile selasie Road nk

Ova
 
Sehem kubwa ya ukonga haijapimwa. Unataka serikali iingie gharama ya kuvunja nyumba za watu mje kulalamika hapa kuwa mnaonewa. Anzeni kuvunja nyumba zenu tengeni sehem ya barabara alafu iteni serikali muone kama hamtajengewa lami.
Jibu zuri umempa

Ova
 
Majuzi nimepita Mbweni nikashangaa kabisa.

Barabara nyingi zilizokuwa hazipitiki sasa ni lami tupu.

Najua huu ni mkakati wa viongozi wengi kujipendelea maana wengi wamejenga huko.

Nimepeta tetesi kuwa hata kwa Katinu mkuu Kiongozi, watu wameamriwa barabara iendayo kwake iwekwe lami.

Tofauti na Mbweni, huku Mbezi Beach barabara za kwenda makazi ya watu hazijashughulikiwa kabisa.
Barabara za NSSF Flats
Barabara za Jogoo Cotex
B arabara za Mbezi Tangi Bovu
Barabara ya Mbezi 5 Star
Barabara ya Ndumbwi-Baraza la Mitihani
Barabara za chini Kwa Lukuvi

Ila barabara ya kwenda kwa Kikwete Kawe Beach ilikengwa chap chap!

Huu upundeleo dhahiri wa viongozi kujinufaisha!
Ccm mtajuana wenyewe wapinzani wametucherewasha sannaaa ndugu zangu tuenderee kuchapa kazii....
 
Majuzi nimepita Mbweni nikashangaa kabisa.

Barabara nyingi zilizokuwa hazipitiki sasa ni lami tupu.

Najua huu ni mkakati wa viongozi wengi kujipendelea maana wengi wamejenga huko.

Nimepeta tetesi kuwa hata kwa Katinu mkuu Kiongozi, watu wameamriwa barabara iendayo kwake iwekwe lami.

Tofauti na Mbweni, huku Mbezi Beach barabara za kwenda makazi ya watu hazijashughulikiwa kabisa.
Barabara za NSSF Flats
Barabara za Jogoo Cotex
B arabara za Mbezi Tangi Bovu
Barabara ya Mbezi 5 Star
Barabara ya Ndumbwi-Baraza la Mitihani
Barabara za chini Kwa Lukuvi

Ila barabara ya kwenda kwa Kikwete Kawe Beach ilikengwa chap chap!

Huu upundeleo dhahiri wa viongozi kujinufaisha!
Kwani hujui nani ana makazi yake Mbweni? Kujipendekeza hakuishi Tz hii,mwenyewe hata habari hana watu wanahangaika!
 
Kaka nenda jimbo la ukonga ndio utaona maajabu ya dunia, wakati sehemu nyingine wanang'oa lami na kuweka nyingine, huko hata vifusi haviwekwi,kipindi cha mvua watu wanatamani kutorejea majumbani! hi keki ingegawanywa hata wapate "karobo" hao wakubwa wachukue robo tatu ila sio kulamba asali yote🙆‍♂
Ukonga kule nadhani tumelaaniwa maana hatukumbukwi kabisa. Zile siyo barabara kabisa. Nashangaa Segerea kila siku watu wanang'oa lami na kubandika nyingine.
 
Sehem kubwa ya ukonga haijapimwa. Unataka serikali iingie gharama ya kuvunja nyumba za watu mje kulalamika hapa kuwa mnaonewa. Anzeni kuvunja nyumba zenu tengeni sehem ya barabara alafu iteni serikali muone kama hamtajengewa lami.
Kisingizio Cha kijinga. Mwisho utakuja dai "chato ilikuwa inajengwa kwa nguvu zote kwa kuwa mikoa mingine haijapimwa".
 
Back
Top Bottom