GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,044
- 119,624
Ningependa kuchukua FURSA hii murua kumshauri Mtanzania pekee aliyetutoa KIMASOMASO katika mchezo wa mpira wa miguu Mbwana Ally Samatta a.k.a POPA kuwa kwakuwa tayari tumeshajua kuwa yupo MAJUU na mambo yake ni safi kimtindo basi apunguze sasa kupiga piga MIPICHA na kuituma kwa Wana Blog na Washikaji zake kila mara huku zingine zikiwa hata hazina maana. Kwa mfano kuna moja amejipiga yupo juu GHOROFANI nadhani katika APARTMENT yake anapiga mswaki huku nyingine akiwa anavaa KANDAMBILI. Halafu kwa MSHANGAO mkubwa Miandishi yetu ya Habari za Kibongo na Bloggers nao wanatuwekea picha hizo hizo tuziangalie. Tunafaidika na nini sasa hapa?
Ningependa nichukue muda huu adhimu nimuonye Mbwana Ally Samatta kuwa hapo alipo asidhani ndiyo kamaliza tena kwa tunaojua soka la kulipwa hasa la ULAYA sasa Mbwana Samatta ndiyo anatakiwa akazane sana KIMAZOEZI huku akizingatia MAADILI yote muhimu ya Mchezaji wa Kulipwa ili aweze kuonekana zaidi na Klabu zingine Kubwa ILA akiwaendekeza Watanzania ambao wengi wao leo wanajifanya WANAMJUA namuhakikishia ATAPOROMOKA sasa hivi. Tulimuonya Mcheza Kikapu Mtanzania Hasheem Thabit hivi hivi kuwa awe makini na Kazi yake hakutusikia na matokeo yake VIDEMU DEMU vya kibongo bongo VIKAJIPENDEKEZA kwake na kumuharibu kabisa hadi akakosa nafasi na kupelekwa timu nyingine kwa MKOPO na sasa anahangaika kurudi katika KIWANGO lakini bado.
Mbwana Ally Samatta napenda nikutaarifu kuwa Watanzania SISI SISI ambao sasa tunajifanya tupo karibu nawe ndiyo SISI SISI ambao ukishindwa huko tutakuwa wa kwanza kukupiga MADONGO na KUKUZUSHIA mengine hadi ambayo HUKUYAFANYA. Sipendi nikufanye labda USIJICHANGANYE nao katika MITANDAO YA KIJAMII la hasha bali NAKUHUSIA tu kuwa acha KUTUMIA MUDA WAKO MWINGI MITANDAONI huku UKITURUSHIA au KUTUTUMIA PICHA zako bali poteza muda wako mwingi KUJIFUNZA SOKA LA KULIPWA LA ULAYA LIPOJE, CHANGAMOTO ZAKE ZIPOJE, PAMBANA na UWE NA MALENGO MAKUBWA zaidi.
Ushauri wangu una hiari ya KUUCHUKUA na KUUPIMA au KUUPUUZA ila kuna siku UTANIKUMBUKA na KUUKUMBUKA. Nakutakia maisha na mafanikio mema hapo Ubelgiji na FAHAMU kwamba Watanzania wote TUNAKUTEGEMEA Wewe uwe NURU ya kuwaangazia wenzako akina Mkude, Telela, Busungu na Ajib na WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO hebu muacheni basi Kijana ajipange kwanza na msaidieni KIUSHAURI.