Mbwana Samatta cheza mpira sasa

Wewe a
UZI wangu huu UNANIONYESHA vizuri sana watu ambao KICHWANI ZIPO na ambao HAMNAZO. Kwa mfano tu post yako imenionyesha kuwa dhahiri wewe ni Mr. HAMNAZO katika Bichwa lako. Kama ingekuwa ni hivyo basi hata hawa MARAIS wote duniani wasingekuwa na WASHAURI bali wangejifanyia tu wenyewe mambo yao! Hivi kule Vyuoni mlikuwa mnaenda kufanya nini kama hamjui hata kujenga HOJA yenye MASHIKO tena nyepesi tu kama hii?
Akipiga mapicha wewe unapungukiwa nini au ktk mafanikio take wewe ulichangia yeye kupata mafanikio
Mwache hiyo mtoto mtoto wa mbagala aishi atakavyo au ikiwa VP omba ajira ya wewe kuwa mshauri wake!
 
Mkuu kwa HIKI KITU CHA MAANA NA KIZURI ULICHOKIANDIKA AMBACHO KIMENIFANYA SASA NIAMINI KUWA KUMBE WENYE AKILI NA UWEZO WA KUCHAMBUA MAMBO NA KUJENGA HOJA TUMEBAKI WACHACHE SASA. Nimekukubali sana mkuu, asante na naomba niseme tu kwako SHIKAMOO.
Pamoja sana Mkuu.
 
Mkuu umeongea kitu cha maana sana! Natamani wote wale wanaopenda kuanzisha thread waisome comment yako.

Ndio mkuu kuna watu hawataki changamoto aisee wanataka kila mtu akubali hoja yake kitu ambacho hakitawezekana milele
 
Mkuu nakubaliana na wewe tena kwa 100% kuwa Waafrika wengi hasa WACHEZAJI mpira hupenda KUDANGANYA kuhusu UMRI wao ila kwa umri wa Mbwana Samatta HAJAONGOPA mkuu amini usiamini ila tatizo kubwa la sisi Waafrika na labda niseme kwetu hapa Tanzania huwa hatufanyi Scouting nzuri kwa Wachezaji wetu na kibaya zaidi hatuzingatii hata DOCUMENTATION. Kwa mfano nenda pale TFF sasa hivi uliza jambo tu la mwaka 1985 au 1990 ukilikuta ni MSALIA MTUME. Mbwana nisiwe mwongo bado ni mdogo na hata huo UMRI wake ni sahihi nenda kokote kaulize isipokuwa kuna Wachezaji leo naambiwa bado wadogo mfano Nahodha wa Mtibwa Shaaban Nditi nasikia hata katika Passport yake imeandikwa NJEMBA ndiyo kwanza Inagonga 26 sasa tizama NYAGO lake ongeza na UNYUMBULIFU wake uwanjani kisha JIONGEZE.
Mark my words, ana umri mkubwa zaidi ya huo anaotumia sasa !!
 
Kuna wabongo kama kawaida yao wamevamia facebook page ya Genk kuongea utumbo, kuna fala kasema Samata is better than Genk sasa sijui anamaana gani. Mwingine anadai hakuna striker bora pale Genk zaidi ya Samata, ali mradi waharibu hali ya hewa tu. Mpaka jamaa wanasema huyu Samata inaelekea ana fans wengi sana
 
acha wivu wa ajabu ajabu,hayo mambo unayoongea ni mambo ya zamani,watanzania wanataka kujua maendeleo ya kijana wetu,nenda instagram uone akina ronaldo wanapiga picha wamefunga mataulo,nyingine anaonyesha nyumba yake mpk chumba cha kulala,kijana ndio ananza kuyaona mafanikio kwanini asifurahie?kama ipo ipo tu wakowapi akina henry joseph,nizar khalfan,hatuna boban ambao tulikuwa hatujui hata wanapocheza leo hii tunao hapa hapa nyumbani.

Ningependa kuchukua FURSA hii murua kumshauri Mtanzania pekee aliyetutoa KIMASOMASO katika mchezo wa mpira wa miguu Mbwana Ally Samatta a.k.a POPA kuwa kwakuwa tayari tumeshajua kuwa yupo MAJUU na mambo yake ni safi kimtindo basi apunguze sasa kupiga piga MIPICHA na kuituma kwa Wana Blog na Washikaji zake kila mara huku zingine zikiwa hata hazina maana. Kwa mfano kuna moja amejipiga yupo juu GHOROFANI nadhani katika APARTMENT yake anapiga mswaki huku nyingine akiwa anavaa KANDAMBILI. Halafu kwa MSHANGAO mkubwa Miandishi yetu ya Habari za Kibongo na Bloggers nao wanatuwekea picha hizo hizo tuziangalie. Tunafaidika na nini sasa hapa?

Ningependa nichukue muda huu adhimu nimuonye Mbwana Ally Samatta kuwa hapo alipo asidhani ndiyo kamaliza tena kwa tunaojua soka la kulipwa hasa la ULAYA sasa Mbwana Samatta ndiyo anatakiwa akazane sana KIMAZOEZI huku akizingatia MAADILI yote muhimu ya Mchezaji wa Kulipwa ili aweze kuonekana zaidi na Klabu zingine Kubwa ILA akiwaendekeza Watanzania ambao wengi wao leo wanajifanya WANAMJUA namuhakikishia ATAPOROMOKA sasa hivi. Tulimuonya Mcheza Kikapu Mtanzania Hasheem Thabit hivi hivi kuwa awe makini na Kazi yake hakutusikia na matokeo yake VIDEMU DEMU vya kibongo bongo VIKAJIPENDEKEZA kwake na kumuharibu kabisa hadi akakosa nafasi na kupelekwa timu nyingine kwa MKOPO na sasa anahangaika kurudi katika KIWANGO lakini bado.

Mbwana Ally Samatta napenda nikutaarifu kuwa Watanzania SISI SISI ambao sasa tunajifanya tupo karibu nawe ndiyo SISI SISI ambao ukishindwa huko tutakuwa wa kwanza kukupiga MADONGO na KUKUZUSHIA mengine hadi ambayo HUKUYAFANYA. Sipendi nikufanye labda USIJICHANGANYE nao katika MITANDAO YA KIJAMII la hasha bali NAKUHUSIA tu kuwa acha KUTUMIA MUDA WAKO MWINGI MITANDAONI huku UKITURUSHIA au KUTUTUMIA PICHA zako bali poteza muda wako mwingi KUJIFUNZA SOKA LA KULIPWA LA ULAYA LIPOJE, CHANGAMOTO ZAKE ZIPOJE, PAMBANA na UWE NA MALENGO MAKUBWA zaidi.

Ushauri wangu una hiari ya KUUCHUKUA na KUUPIMA au KUUPUUZA ila kuna siku UTANIKUMBUKA na KUUKUMBUKA. Nakutakia maisha na mafanikio mema hapo Ubelgiji na FAHAMU kwamba Watanzania wote TUNAKUTEGEMEA Wewe uwe NURU ya kuwaangazia wenzako akina Mkude, Telela, Busungu na Ajib na WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO hebu muacheni basi Kijana ajipange kwanza na msaidieni KIUSHAURI.
 
Sidhani kama kunatatizo..
 

Attachments

  • 1455177086331.jpg
    1455177086331.jpg
    51.6 KB · Views: 49
Hii thread imenifanya nimkumbuke maywether...pesa anatafute yeye mipango ya matumizi wanapanga wengine....shwain africans
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom