Mbwa wamezua balaa!usiku wa manane mtaani kwetu

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,557
3,001
Heshima zenu wakuu!

Wanajamvi jana imetokea sokomoko mtaani mida ya saa 9:05 usiku kundi la mbwa linatembea huku wakibweka, wengine huenda waliachwa nyuma wakawa wanipita mmoja na wengine wawili nakumbuka kuna wengine walikuja dirishani kubweka dah!

Sijawah experience hili jambo, hivi wajuzi wa mambo inawezekana mbwa wakatembea kwa makundi na hata kufatana?
 
20230322_121857.jpg
 
Maandamano, kuna namna viongozi wao wanazingua, fuatilia mambo yao ya uchaguzi utajua sababu, poleni sana.
 
Kama umesoma biology basi utaelewa nini kilichoendelea hapo.
Yaani kuna jike lilimwaga uteute wa kuwavutia madume.
Sasa na menyewe kwa kunusa sio poa ndio maana yakajazana.
Ila wakianza kudinyana wakanasana hata kama uwapige mawe hawaachani wanakimbia hivyo hivyo huku wamenasana
 
Hao wapo kwenye msimu wa kupandana wanajikusanya wengii na wanakua na akili za ajabu sana. Sitasahau miaka ya nyuma kidogo nikiwa mkoani kwangu nilipokulia nilikua nafuga kondoo. Sasa bhana kwenye kuchunga nipo maeneo ya mashambani nikaona kundi la mbwa wakipandana na kukimbizana haikupita muda mbwa wale wakahamishia hisia zao kwenye kondoo wangu dah waliwakimbiza wakadaka kondoo wawili wakawang'ata miguu ya nyuma moja dume na mwingine jike alikua na mimba bahati nzuri kulikua na watu wakasaidia kupiga na kufukuza ila kondoo wangu walijiuguza kwa muda wa wiki mbili wakapona.

Kile kitu kiliniumiza roho sana nikaanza kuwasaka machimbo yao tulijikusanya wafugaji watatu mzee mmoja alikua na mshale mm panga na faza mmoja alikua na mkuki wale mbwa tuliwauwa kadhaa na yukapata msaada wa mamlaka ya mji mdogo wakapigwa risasi wakafa japo sio wote ila nilipunguza machungu....

Mbwa wakiwa msimu wa kupandana wanakua hawana akili kabisa sishangai hao waliokuja kubweka dirishani kiufupu wanamiyeyusho sana cha ajabu msimu ukiisha akili zao zinarudi timamu
 
Heshima zenu wakuu!

Wanajamvi jana imetokea sokomoko mtaani mida ya saa 9:05 usiku kundi la mbwa linatembea huku wakibweka, wengine huenda waliachwa nyuma wakawa wanipita mmoja na wengine wawili nakumbuka kuna wengine walikuja dirishani kubweka dah!

Sijawah experience hili jambo, hivi wajuzi wa mambo inawezekana mbwa wakatembea kwa makundi na hata kufatana?
Wakihisi mmebeba misosi ya harusini, hawawaachi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom