Mbunge wangu Mwigulu umeshindwa kabisa!

Mnambua

Member
Joined
Jan 6, 2020
Messages
92
Points
125

Mnambua

Member
Joined Jan 6, 2020
92 125
Wewe ni Mchumi na siku zote wachumi huelezea uhalisia wa mambo kwa namba. Wataalamu wanadai "namba haziongopi".

Mheshimiwa umekosa ujasiri wa kusema mambo ambayo umeifanyia Iramba kwa sababu hamna ulichofanya ambacho unaweza kujivunia.

Au unataka kuongelea kwa mfano shule yako ya Kata yaani Kyengege kutoka nafasi ya 15 kimkoa Mwaka juzi na kufikia nafasi ya 8 kwa Mwaka jana hayo ni mafanikio?

Viko wapi visima vya maji ulivyoahidi katika vijiji mbalimbali vya Iramba, umeshinikiza vipi Mradi wa umeme wa REA kukamilishwa pale ulipokomea?

Ukiacha Kituo cha Afya cha Kinampanda wapi kwingine unapojivunia uliacha?

Ukweli ulikazania siasa za Kitaifa za kutaka uwe Rais - wapi sasa maendeleo uyaonayo yameletwa na siasa zako za Kitaifa zaidi ya kuzidi kunyongonyezwa tu wewe na Nape na Januari?

Na inadaiwa umewekewa TISS wa kumwaga tu hadi chumbani kwako!

Kikubwa tumia akili achia ngazi mapema, tafuta kitu bora zaidi cha kufanya ili kuepukana na Rais Magufuli kwenye siasa kwa kuwa kwa vyovyote anavyokuchulia wewe ni threat kwake atahakikisha anakukata juu kwa juu na Ubunge hutopata!
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
33,366
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
33,366 2,000
Kama unataka kugombea Iramba, gombea tuu kwa kusema utafanya nini, hakuna jimbo lolote ni mali ya mtu, huna haja ya kutumia jina la Magufuli kumtishia Mwigulu, Mbunge aliyepo ni Mwigulu na ni Mbunge wa jimbo la Iramba na amechaguliwa na wana Iramba na sio Mbunge wa jimbo la Magufuli, hivyo hivyo vitisho vya kuwa Magufuli atamkata, usitishe watu, wanaochagua ni wana Iramba, wakijiona kama bado wanamuhitaji Mwigulu wao na Magufuli kweli akamkata, its up to Wanairamba kumkubali huyo atakayepitishwa au kumchukua Mwigulu wao na kumrudisha kupitia chama kingine, hivyo ndivyo wapinzani wengi waliingia bungeni toka Dr. Slaa hadi Mwambe.

P
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Messages
2,796
Points
2,000

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2018
2,796 2,000
Watu wanampigia kelele Zitto Kabwe haonekani jimboni kwake, wanawasahau wabunge wa CCM 90% wanajazana Dodoma na Dar es Salaam na kwenye majimbo yao hawaonekani kabisa kusaidia changamoto na kero za wananchi wao.

Hasa waliopata "VYEO" kwenye serikali hii. Ila muda ndio ushafika wa "MAPAMBANO".
 

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Messages
2,349
Points
2,000

chizcom

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2016
2,349 2,000
mimi mpaka leo sijaelewa kazi wala faida za wabunge na majimbo yao.

kwa maelezo fikirishi tu Majimbo yapo ndani ya wilaya na wilaya hipo ndani ya mkoa. Mkuu wa mkoa na wilaya miaka ya sasa ndio wamekuwa kama wanafanya kazi zisizo zao sijui mfano hapa Dar.

Hivi hizi Halmashauri kuna madiwani nazo hata kumpa nafasi mbunge hawe mwenye kupitia au kuongoza sioni.

labda wabunge wabaki bungeni tu kueleza

Sent from my iPhone using JamiiForums
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,539
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,539 2,000
Pascal Mayalla,

Paskali hapa ni kama unamchora tu Mwigulu. Ufahamu hata Mwigulu mwenyewe anajua hakuna uchaguzi bali rais ndio anaamua uwe mbunge, na iwapo Rais hataki uwe mbunge, hata uchaguliwe na wananchi wote hutatangazwa mshindi.

Uzuri hata Mwigulu anaujua ukweli huu kwani naye ameshiriki muda mrefu siasa chafu hapa nchini, hivyo kinachomkuta hivi sasa ni karma.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
33,814
Points
2,000

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
33,814 2,000
Pascal Mayalla, Tatizo Mwigulu akiwekewa mizengwe CCM anaweza kukimbilia wapi wakati hakuna ruhusa ya mgombea binafsi?

Shida ya Mwigulu wakati akiwa madaraka vyama vingine alivifanya adui na kuviona takataka, nani anaweza kumpa nafasi hata kama anao wapiga kura wa kutosha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,539
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,539 2,000
chizcom,

Mkuu tunashukuru kwa mchango wako, nakushauri achana na michango ya siasa rudi shule kwanza ukijifunze kuandika kwa usahihi, kama kuweka koma, nukta na matumizi ya herufi kubwa na ndogo. Pia una tatizo la matumizi ya herufi H kwenye uandishi wako. Usidhalilishe shule za kata tafadhali.
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,539
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,539 2,000
Chakaza,


Mkuu wala usiseme hivyo, kama cdm walimpokea Lowassa usishangae Mwigulu akiwa mgombea wa cdm. Hivyi vyama vyetu vya upinzani navyo havina msimamo ambao unaweza kuwaamini. Lakini piga ua, Mwigulu yuko radhi adhalilike akiwa ccm, maana anajua fika hana uwezo wa siasa za ushindani nje ya mbeleko ya vyombo vya dola. Na yeye ndio amekuwa akishiriki na kupanga chaguzi za dhuluma, hivyo anajua fika akitoka ccm dhuluma alizokuwa anashiriki zitamfika hata yeye. Atakachofanya ni kuweka sura ya huruma ili apewe hata ukuu wa mkoa. Mwigulu ni baadhi ya viongozi wa ccm walioendesha siasa za chafu sana ndani ya nchi hii.
 

Mnambua

Member
Joined
Jan 6, 2020
Messages
92
Points
125

Mnambua

Member
Joined Jan 6, 2020
92 125
Pascal Mayalla,
Nilichogundua tangu zamani wkt nikiperuzi JF nikiwa sina akaunti Paskali wewe ni "mtabiria kila mtu". Paskali wkt wa Uchaguzi ukifika kila aliyekuwa akionesha anaonesha nia ulikuwa ukimtabiria tu vile au vile ilimradi tu ikitokea kashinda au kakwama basi moja kwa moja inaonekana utabiri wako ulikuwa wa kweli. Hamna uliyekuwa ukiacha kumwongelea ndiyo maana na hapo umeleta thread uliyowahi kuandika ukimtabiria Mwigulu.
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,539
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,539 2,000
Swadakta, Kila kitu hatari na kibaya MAGUFULI mnyonge mnyongeni haki zake mpeni. Magufuli hayupo kwenye mchakato wowote Iramba,singida nk na sauti ya mwisho ni yawairamba
Wanairamba au wapiga kura wowote ndani ya nchi hii hawana sauti zaidi ya rais kwenye uchaguzi. Hilo unataka hutaki ukweli ndio huo.
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,539
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,539 2,000
Mnambua,

Ahaaa ahaaaa ni sawa na mtu anazifuata timu zote kwenye ligi kila moja kwa wakati wake na kuiambia utashinda ligi, kisha mwisho wa ligi ile iliyoshinda anasema si mnaona nilitabiri!
 

Mnambua

Member
Joined
Jan 6, 2020
Messages
92
Points
125

Mnambua

Member
Joined Jan 6, 2020
92 125
Wanairamba au wapiga kura wowote ndani ya nchi hii hawana sauti zaidi ya rais kwenye uchaguzi. Hilo unataka hutaki ukweli ndio huo.
Ndiyo maana Mwigulu anatakiwa kujitengenezea mazingira ya ama kuachana na siasa kwa wakati huu au kufikiria kuwapigia magoti wapinzani ili JPM akimkata awe na tawi la mti mwingine alishike. Harakati hizo azionesha sasa naawe Mwanaume wa shoka asiwe mnyonge kwa JPM.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
33,366
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
33,366 2,000
Paskali hapa ni kama unamchora tu Mwigulu. Uzuri hata Mwigulu anaujua ukweli huu kwani naye ameshiriki muda mrefu siasa chafu hapa nchini, hivyo kinachomkuta hivi sasa ni karma.
Kwenye hili la karma, naomba kumtetea Mwigulu.

Kuna viongozi wengi wametumbuliwa katika hao wanaotumbuliwa kuna baadhi kweli ni majipu na sababu za kutumbuliwa huwa zinawekwa. Lakini wengine wanatumbuliwa tuu kwa sababu nyingine na sio majipu, hawa wanaotumbuliwa ambao sio majipu, sababu za kutumbuliwa kwao huwa hazitolewi, Mwingulu Mchemba ni mmoja wa watu hawa, sasa kwa mujibu wa taarifa za koridoni zilizopelekea Mwigulu kutumbuliwa, naomba uniamini mimi, karma haitamhusu!.

Ukipitia bandiko hili, kuna kitu nilikisema kumhusu Mwigulu kabla hajatumbuliwa kilichopelekea akatumbuliwa ila huyu sio jipu!.

P
 

Forum statistics

Threads 1,392,003
Members 528,520
Posts 34,095,296
Top