Mbunge Latifa Juwakali ashiriki hafla ya ugawaji wa sare za skuli ya Uzini kusini Unguja

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,890
939
Mbunge wa Viti Maalum Vijana Kusini Unguja Latifa Juwakali alishiriki halfla ya Uzinduzi wa ugawaji wa sare za Skuli kwa watoto wenye mahitaji Maalum katika Skuli ya Uzini, Wilaya ya Kati, Kusini Unguja tarehe 06 Machi, 2023.

Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Khamis Hamza Chilo, Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira hafla iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali inayoitwa HANII Foundation

Katika hafla hiyo Juwakali amewasisitiza wanafunzi wa Skuli ya Uzini kusoma kwa bidii na kutumia vyema fursa za Misaada inayotolewa kutoka kwa wahisani mbalimbali wanaoonyesha nia ya kuwajali.

Aidha, Latifa Juwakali amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Latifa Juwakali amempongeza Rais Samia kwa kuongeza pesa ya wanafunzi Chuo Kikuu kutoka Shilingi 7,000 mpaka Shilingi 10,000 kwa siku. Na kuahidi kuwafikiria wanafunzi wa Elimu ya Kati (Cheti na Diploma) na Elimu bure kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi mpaka Kidato cha Sita.

Latifa Juwakali amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuchukua hatua mbalimbali ambazo zimesaidia kukamilika kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM Zanzibar.

Latifa Juwakali amewaomba vijana kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi ili kuzidi kuongeza kasi ya maendeleo Tanzania Bara na Zanzibar.

#KaziIendelee

WhatsApp Image 2023-03-07 at 12.48.40.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-07 at 12.48.44.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-07 at 12.48.49.jpeg
 
Back
Top Bottom