Mbunge Latifa Juwakali: Rais Samia ni Mfano wa Kuigwa Amefanya Mkabwa Ndani ya Miaka Miwili.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MHE. LATIFA JUWAKALI ASEMA RAIS SAMIA NI MFANO WA KUIGWA, AMEFANYA MAKUBWA KWA MIAKA MIWILI MADARAKANI.

Mbunge wa Viti Maalum CCM Vijana Mkoa wa Unguja Mhe. Latifa Khamis Juwakali amesema kwa Miaka Miwili ya Madarakani Rais Mhe.. Samia Suluhu Hassan amekuwa mfano wa kuigwa maana amefanya makubwa kwa muda mchache.

Mhe. Latifa Juwakali amempongeza Rais Samia na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 Zanzibar kwa upande wa vijana ambapo yeye ni Mbunge wa Vijana kutoka Mkoa wa Kusini Unguja.

Mhe. Latifa Juwakali akiwa Paje tarehe 29 Disemba 2022 alichangia Shilingi Laki tano (500,000) kwa ajili ya matengenezo ya Ofisi ya UVCCM Jimbo la Paje ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025.

Mhe. Latifa Juwakali aliwachangia Shilingi Laki Tano (500,000) kikundi cha vijana wa CCM jimbo la.... kwa ajili ya kununua Vifaranga vya Kuku ili kuendeleza kuwapa nguvu vijana katika ufugaji.

Mhe. Latifa Juwakali katika kutoa ushirikiano Elimu aliweza kutembelea Shule ya Hasnuu Makame na kuchangia vifaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mashine ya Photocopy na kugawa taule za kike kwa wanafunzi wakike.

Mhe. Latifa Juwakali alipotembelea mradi wa Umoja wa Vijana CCM Kusini aliwakabidhi Mipira Miwili kwa ajili ya kusambazia Maji; Motor ya Maji; na Miche 2000 ya Mipensheni kwa ajili ya kuendeleza mradi wa kitalu jumba ambao wanaufanya kujiendeleza kiuchumi.

Pia, akiwa Wilaya ya Kusini aliwakabidhi Karatasi (Limu Paper tano UVCCM) na Karatasi (Limu Paper tano CCM Wilaya ya Kusini)

Mhe. Latifa Juwakali katika Jimbo la Paje aliwakabidhi kikundi cha vijana mashine ya kutolea maji katika mradi wao wa ufugaji Samaki wa Maji baridi.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-03-07 at 15.26.44.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-07 at 15.26.44.jpeg
    93.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-03-07 at 15.26.42.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-07 at 15.26.42.jpeg
    71.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-03-24 at 14.38.56.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-24 at 14.38.56.jpeg
    95.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-03-12 at 19.11.08.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-12 at 19.11.08.jpeg
    67.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-03-12 at 19.09.42.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-12 at 19.09.42.jpeg
    90.7 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-03-07 at 15.26.44(7).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-07 at 15.26.44(7).jpeg
    87.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom