Mbunge wa Tabora Mjini Aden Rage apata ajali Dodoma

Mbunge wa Tabora Mjini Aden Rage apata ajali Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM), ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, amenusurika kifo na kuumia bega la Kushoto akiwa na watu wengine watatu baada ya gari alilokuwa akitumia kusafiria aina ya Toyota Lund Cruser T 845 DQS (gari binafsi) kuacha njia na kuanguka katika eneo la Chigongwe wakati akiwa njiani kuelekea mjini Dodoma kuanza vikao vya Bunge la Katiba hapo kesho.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, David Misime, amesema ajali hiyo imetokea leo Agost 4, 2014 na kuwa imetokea katika eneo la Njia panda ya Kigwe katika barabara ya Singida Dodoma, wakati mbunge huyo akielekea mkoani Dodoma kwa ajili ya kuanza vikao vya Bunge Maalum la katiba.

Amesema Rage, ameumia katika bega la kushoto na mgongoni huku Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Tabora, Munde Abdalla Tambwe, akiumia sehemu za kichwani na kuwa majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Amesema watu wengine waliokuwepo katika gari hilo ni pamoja na Mwanahamis Athumani, John Hoya ambao wote kwa pamoja wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo.

Hata hivyo amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika, na kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha ajali hiyo.
Nilishafurahi uchaguzi mdogo tena tabora jimbo lipokonywe magamba
 
Juhudi za ukawa kukwamisha katiba zinaendelea
 
nampa pole sana , lakini wakati huohuo namkumbusha kwamba dunia ni mapito , na kwamba huenda MKOSI HUU umempata baada ya yeye mwenyewe kwa kushirikiana na mary chatanda kuongoza MAPAMBANO OVU YA KUDHAMIRIA KUMUUA KAMANDA SWAI KWA MAWE NA MAGONGO tena hapohapo dodoma , DUNIA NI MAPITO TUJIFUNZE KUVUMILIANA , HAYA KIKO WAPI SASA ?
 
Mh Aden Rage amepata ajali ya gari eneo la Chigongwe nje kidogo ya mji wa Dodoma. Amepata ajali akitokea jimboni kwake Tabora mjini kuelekea Dodoma kuhudhuria "BONGE MAALUM LA KATIBA". Abiria wote watano wanusurika kifo. Ajali hiyo imetokea wakati dereva wake akijaribu kulipita Lori na baadaye kuona gari ikitokea kwa mbele na kumpa mtihani wa kugonga Lori kwa nyuma, kugongana na gari la mbele - anako-overtake au kuingia mtaroni. Dereva kaliingiza gari mtaroni, ambapo wamepata majeraha madogo.

Source: ITV - Breaking news.

Hahahaha! eti BONGE MAALUM LA KATIBA hapo umeua mkuu
 
Daah! Israel alikuwa mitaa gani mtu wangu! maana angemtwaa tu! hizo laki tatu tatu anazofuata zingeokoa wa mama wajawazito kibao na watoto wao! kuliko hicho anachokifuata ambacho hakitakamilika ! rest in Hell Rage wa CCM

Hii laana ikurudie wewe, ukipata hata ka-ajali cha kuteleza na toyo kasikuache mzima.
 
Naona mnawaombea watu Vigo, ongera yenu kwa kupewa na mungu amri ya kuukumu,
 
Wallah kwa alichofanya kwa kamanda Swai ningekuwa karibu ningemmalizia mbali...Ana bahati sana huyu Rage!!!
 
Haya mmeyarithi kutoka kwa viongozi wenu wakuu wa CHADEMA, kuna kipindi waliliegeza NATI kwenye gari la ZITTO ili apate ajali!
Mkuu MSALANI umenena ni wazi Walilegeza nati za gari la Zitto na walilipua mkutano wao Soweto!
 
Last edited by a moderator:
Astakafirllah ... sisi sote Waja wa Mwenyezi Mungu Sheikh wangu.... Kusameheana ni jambo zuri sana kwetu sisi Wanaadamu... Pamoja na Mabaya yake yote na ukatili ule wa kutaka kumtwanga mawe kada wa CDM ... Bado yafaa kumsamehe ili ajifunze kuwa na huruma kwa viumbe wenzie ...
Daah! Israel alikuwa mitaa gani mtu wangu! maana angemtwaa tu! hizo laki tatu tatu anazofuata zingeokoa wa mama wajawazito kibao na watoto wao! kuliko hicho anachokifuata ambacho hakitakamilika ! rest in Hell Rage wa CCM
 
Taarifa hizi nimezipata kutoka BAHI kwamba Mbunge Ismail Aden Rage pamoja na mbunge wa viti maalum Munde Tambwe wamepata ajali ya gari maeneo ya Bahi, Dodoma. sijapata hali ya majeruhi wala sababu za ajali. mwenye taarifa zaidi atupie hapa!
 
nampa pole sana , lakini wakati huohuo namkumbusha kwamba dunia ni mapito , na kwamba huenda MKOSI HUU umempata baada ya yeye mwenyewe kwa kushirikiana na mary chatanda kuongoza MAPAMBANO OVU YA KUDHAMIRIA KUMUUA KAMANDA SWAI KWA MAWE NA MAGONGO tena hapohapo dodoma , DUNIA NI MAPITO TUJIFUNZE KUVUMILIANA , HAYA KIKO WAPI SASA ?

Dah...Mkuu unekumbuka mbali sana kamanda wangu duh......Hivi Kamanda Swai yupo?? maana nasikia maintarehamwe yalimtupa lupango, Vipi alitoka?

Wakuu yeyote mwenye ile picha ya huyo Rage akimshambuli Kamanda Swai pamoja na maintarehamwe wenzie Aiweke hapa tujikumbushe simanzi jinsi haya madubwana yanvyojifanya kuwa juu ya Sheria

BACK TANGANYIKA
 
TUMUOMBE mag 3 ATUWEKEE HIYO PICHA .
 
Poleni majeruhi, Mungu awatie nguvu mpone haraka.

R.I.P. CCM
 
Mkuu kuna wakati nilihuzunika sana kutokana na kuona kijana mpambanaji akikubali kutumiwa kama mamluki! Siku muelewa Zitto kabisa, nae bila ajizi alikuja hapa jukwaani kuomba msamaha kwa mabaya aliyowafanyia wapenda mabadiliko Tanzania, well alisamehewa lakini baadae ikaja kubainika kuwa saratani ya usaliti ilishamtafuna ubongo na hakuna uwezekano tena wa kumpata Zitto kijana alielelewa na Mbowe toka akiwa O level pale Kibohehe... kama kawa time heeling! ... Sasa tunafarijika kuwa Zitto si lolote si Chochote mbele ya mamia kwa maelfu ya Watanzani tena wenye weledi wajuzi waliobobea kama akina Lisu, Butiku, Warioba, Mbowe, Slaa, Lipumba, Palamagamba Kabudi et al... Bado CHADEMA na Tanzania ina hazina kubwa sana ya Wazalendo wa Kweli wasiokuwa na Price Tag Mgongoni ...
Mkuu MSALANI umenena ni wazi Walilegeza nati za gari la Zitto na walilipua mkutano wao Soweto!
 
Back
Top Bottom