Mbunge wa Tabora Mjini Aden Rage apata ajali Dodoma

Mbunge wa Tabora Mjini Aden Rage apata ajali Dodoma

Dotto Mnzava

R I P
Joined
Mar 6, 2014
Posts
864
Reaction score
427
Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM), ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, amenusurika kifo na kuumia bega la Kushoto akiwa na watu wengine watatu baada ya gari alilokuwa akitumia kusafiria aina ya Toyota Lund Cruser T 845 DQS (gari binafsi) kuacha njia na kuanguka katika eneo la Chigongwe wakati akiwa njiani kuelekea mjini Dodoma kuanza vikao vya Bunge la Katiba hapo kesho.

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, David Misime, amesema ajali hiyo imetokea leo Agost 4, 2014 na kuwa imetokea katika eneo la Njia panda ya Kigwe katika barabara ya Singida Dodoma, wakati mbunge huyo akielekea mkoani Dodoma kwa ajili ya kuanza vikao vya Bunge Maalum la katiba.

Amesema Rage, ameumia katika bega la kushoto na mgongoni huku Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Tabora, Munde Abdalla Tambwe, akiumia sehemu za kichwani na kuwa majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Amesema watu wengine waliokuwepo katika gari hilo ni pamoja na Mwanahamis Athumani, John Hoya ambao wote kwa pamoja wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo.

Hata hivyo amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika, na kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha ajali hiyo.
 
Pole sana Rage. Swali kwa mleta mada. hizi number za gari ni za gari la wapi? DQS??
 
Mh Aden Rage amepata ajali ya gari eneo la Chigongwe nje kidogo ya mji wa Dodoma. Amepata ajali akitokea jimboni kwake Tabora mjini kuelekea Dodoma kuhudhuria "BONGE MAALUM LA KATIBA". Abiria wote watano wanusurika kifo. Ajali hiyo imetokea wakati dereva wake akijaribu kulipita Lori na baadaye kuona gari ikitokea kwa mbele na kumpa mtihani wa kugonga Lori kwa nyuma, kugongana na gari la mbele - anako-overtake au kuingia mtaroni. Dereva kaliingiza gari mtaroni, ambapo wamepata majeraha madogo.

Source: ITV - Breaking news.
 
Gundu na laana ya upumb.avu wa kuchakachua rasimu yKa wananchi ilishaanza kuwashughulikia.
Bila UKAWA hakuna bunge la katiba ila kuna BUNGE LA POSHO. Wanachoenda kujadili na kupitisha ni serikali 2 ambazo hazipo kwenye rasimu.
 
Daah! Israel alikuwa mitaa gani mtu wangu! maana angemtwaa tu! hizo laki tatu tatu anazofuata zingeokoa wa mama wajawazito kibao na watoto wao! kuliko hicho anachokifuata ambacho hakitakamilika ! rest in Hell Rage wa CCM

Raana za watanganyika wapenda nchi yao zinaanza kuwafikia mmoja baada ya mwingine mpaka wairudishe bungeni rasimu ya wananchi kabla ya ccm wote kuipata raana hiyo.
 
mbunge wa jimbo la tabora mjini, ismail aden rage (ccm), ambaye pia ni mjumbe wa bunge maalum la katiba, amenusurika kifo na kuumia bega la kushoto akiwa na watu wengine watatu baada ya gari alilokuwa akitumia kusafiria aina ya toyota lund cruser t 845 dqs (gari binafsi) kuacha njia na kuanguka katika eneo la chigongwe wakati akiwa njiani kuelekea mjini dodoma kuanza vikao vya bunge la katiba hapo kesho.

Kamanda wa polisi mkoa wa dodoma, david misime, amesema ajali hiyo imetokea leo agost 4, 2014 na kuwa imetokea katika eneo la njia panda ya kigwe katika barabara ya singida dodoma, wakati mbunge huyo akielekea mkoani dodoma kwa ajili ya kuanza vikao vya bunge maalum la katiba.

Amesema rage, ameumia katika bega la kushoto na mgongoni huku mbunge wa viti maalumu mkoa wa tabora, munde abdalla tambwe, akiumia sehemu za kichwani na kuwa majeruhi hao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa dodoma.

Amesema watu wengine waliokuwepo katika gari hilo ni pamoja na mwanahamis athumani, john hoya ambao wote kwa pamoja wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo.

Hata hivyo amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika, na kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha ajali hiyo.

ni .cqs au dqs?
 
Huu ni wakati mzuri wa wote kumpokea Yesu kuwa BWANA NA MWOKOZI WETU. Ili kupata uzima wa milele. Uzima wa mwili tunaoumiliki ni wa muda mfupi, bali wa YESU NI WA MILELE.
 
Mungu hana makosa ila kwa kumbakisha huyu gamba ni kosa atakuwa iziraeli kachemka kidogo he should go to hell kabisaaaaa good for nothing mp
 
Back
Top Bottom