Mbunge wa Mbarali (CCM) kwenda jela miezi 10 au kulipa faini

Status
Not open for further replies.
Hii ni janja ya CCM kuua ndege wawili kwa jiwe moja.
  1. Kama huyo mbunge alikuwa mpinga mafisadi basi atakuwa amekomolewa kwa sababu CCM inauhakika bora nchi iuzwe kuliko kulikosa hilo jimbo endapo mtoa habari yupo sahihi.
  2. Kuanza kuwafunga wabunge wa CDM kwani watakuwa wameonyesha mfano kwao, na bila ya shaka wataanza na G. Lema, wengine watafuata.
Ni hayo tu, hii habari si ya kuchekelea hata kidogo.

Mkuu unaona mbali sana, kweli yawezakuwa hv!
 
Kama ni kweli wamemfunga watakuwa wamemtoa kafara ili kutisha wabunge wa upinzani. Kigezo kitakuwa kama Tumemfunga mbunge wa CCM iweje wa CDM tumuogope. Kwa CCM hili linawezekana hasa kama mtu huyo haoneshi kuwaunga mkono katika harakati za kutetea uozo na ufisadi. Ila nawasihi wasijaribu kufanya hivyo kwa mbunge yeyote wa CDM kwenye Cangaroo court zinazoendelea sasa kwani ni dhahiri hizi ni kesi za kupika ili kuwaweka busy wapinzani. Strategy ya kurundikia wapizani kesi ilifanya kazi kwa Mrema, kwa sasa haitafanya kazi kwani badala ya kuwaweka busy, sasa itakuwa kila kesi inapotajwa linakuwa ni tukio la kisiasa kwa wafuasi kujazana mahakamani. Na hakuna sheria ya kuwazuia watu kusikiliza kesi, japo Zuberi alitaka kuweka predence hiyo last week akashindwa.
 
Acheni mbwembwe nyie mbona ameeleweka vizuri sana,CDM inalichukua hilo,maana CCm imefilisika watatoa wapi tena bil3 za uchaguzi
 
Miezi 10 tu! Hakuna haja ya kurudia uchaguzi, tusubiri akatumikie kifungo (ambacho kwa usiku na mchana ni miezi mitano), akitoka aendelee kuwakilisha wananci wake, tuokoe fedha za uchaguzi
 
Pole kwa Kilufi, CCM walimwandama muda mrefu, ndiyo maana chadema walipofanya mkutano wa hadhara Mkoani Mbeya walimwambia akahamie CHADEMA.
 
atakata rufaa na itakwenda muda mrefu,ccm hawawezi kukubali uchaguzi mwingine
 
akija aje kugombea jimbo hilo hilo kwa ticket ya chama kingine atashinda tu kama kasingiziwa kosa. Kama alikosa kweli alale mbele
Itawezekana tu endapo katiba mpya itabadilisha sheria inayosimamia sifa za mgombea uongozi kwa maana kwa sasa ukihukumiwa kifungo huna sifa za kugombea hata ukitoka labda kama ulikata rufaa na kushinda.
 
Miezi 10 tu! Hakuna haja ya kurudia uchaguzi, tusubiri akatumikie kifungo (ambacho kwa usiku na mchana ni miezi mitano), akitoka aendelee kuwakilisha wananci wake, tuokoe fedha za uchaguzi
Huijui sheria ya nchi wewe, ukifanya kosa la jinai na ukatiwa hatiani kwanza huruhusiwi kugombea nafasi yoyote ile serikalini kwa sababu ya kosa hilo la jinai. Kama una wadhifa wowote ukitiwa hatiani unakoma on the spot.
 
mi napenda tu kuona chaguzi ndogo sisi wauza pombe tunakesha tukiuza hadi asubuh, ngoja nikawahi frem mbarali
 
Huijui sheria ya nchi wewe, ukifanya kosa la jinai na ukatiwa hatiani kwanza huruhusiwi kugombea nafasi yoyote ile serikalini kwa sababu ya kosa hilo la jinai. Kama una wadhifa wowote ukitiwa hatiani unakoma on the spot.

sio kushitakiwa na kosa la jinai ila ukifungwa kama sikusei mwaka mmoja kwa kosa la jinai
 
wakuu tuwe makini hap na hawa 'wageni' kwani wengine hudhani kuweka habari za kusisimua na za uongo ndiyo ntoke vp nzuri kwao. Hebu tueleweshe vizuri vinginevyo nenda kakojoe kalale!
 
Wakuu hii habari hata mimi nimeipata kupitia kwa DMO wa Mbarali. Huyu mbunge alikuwa na kesi ya kutishia kuua kwa kutumia bastola. Ngoja niwaletee picha ya bastola yake ili muamini.
 
Huijui sheria ya nchi wewe, ukifanya kosa la jinai na ukatiwa hatiani kwanza huruhusiwi kugombea nafasi yoyote ile serikalini kwa sababu ya kosa hilo la jinai. Kama una wadhifa wowote ukitiwa hatiani unakoma on the spot.

mkuu wajanja wamebadili hiyo kitu, sasa hivi kwa mfano huyo mbungo atapoteza hiyo nafasi yake, lakini next time akitoka na ikapita miezi sita sheria inamruhusu kugombea tena na wamefanya hili ktk eneo la ubunge, magamba wehu kweli aiseee
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom