Mbunge wa Mbarali (CCM) kwenda jela miezi 10 au kulipa faini

Status
Not open for further replies.
Wana JF mambo kama haya ni vizuri kuweka source hadharani.Mimi naona huu ni uvumi tu maana hiyo kesi itakuwa imeendeshwa kwa siku ngapi,maana hili jambo ni juzi tu na issue yenyewe ni kutishia kuua! Spidi hii ya mahakama imetoka wapi?
 
Mkuu unaona mbali sana, kweli yawezakuwa hv!

Mkuu hizi habari ni za kweli kabisa. Nimesikia muda huu kupitia redio one kuwa mbunge DICKSON KILUFI Amehukumiwa miaka kumi au alipe faini ya Tsh 500000/= na kua mbunge huyo amelipa cash laki tano na yupo huru.
 
.
Mbona rage alilioa faini ya bastola yake na kubaki na ubunge? Ama Tz sheria zina double standards.
.

Mkuu na huyu kilufi amelipia laki tano kwa kifungo cha miaka kumi na yupo huru. Kwa kweli hizi hukumu zina mambo kwelikweli.
 
Sources zangu toka Mbeya mjini zinasema alitakiwa aende jela miezi 10 au faini Sh 500,000. Yeye kalipa fani ya Sh 500,000 na kuwa huru.
Sheria inasemaje kuhusu hili?maana hapa keshapatikana na kosa la jinai jee bado anazo sifa za kuwa mbunge?
 
Huijui sheria ya nchi wewe, ukifanya kosa la jinai na ukatiwa hatiani kwanza huruhusiwi kugombea nafasi yoyote ile serikalini kwa sababu ya kosa hilo la jinai. Kama una wadhifa wowote ukitiwa hatiani unakoma on the spot.
December 14, 1999, Mtikila alifungwa mwaka mmoja jela kwa kukutwa na hatia ya uchochezi, lakini mwaka 2005 akagombea urais kwa tiketi ya DP. Au kosa lake sio la jinai?
 
Kesi iliyokuwa inamkabili Mbunge CCM Mbarali ambaye alikuwa katika kambi ya wapinga mafisadi alikuwa anakabiliwa na kesi ya kutishia kuua amefungwa miezi 10 na hivyo kuachia kiti kama sheria za uchaguzi zinavyosema.

Pole Nape, Sita, Mwakyambe na Mama kilago malecela shughuli inakuja kwenu mpiganaji wa tatu ametoweka tukianza na Seleli, Mpendazoe na sasa Kilufi wa Mbarali

Habari ..justifications pls

Wameanza kufangana kama .... Hivi!! Its a threat kwa uongozi wote wa Taifa hili! How can you say no when its the time for a Kiogozi namber 1 or 2 Or 3 of the country? ...just like that!!
 
Kesi iliyokuwa inamkabili Mbunge CCM Mbarali ambaye alikuwa katika kambi ya wapinga mafisadi alikuwa anakabiliwa na kesi ya kutishia kuua amefungwa miezi 10 na hivyo kuachia kiti kama sheria za uchaguzi zinavyosema.

Pole Nape, Sita, Mwakyambe na Mama kilago malecela shughuli inakuja kwenu mpiganaji wa tatu ametoweka tukianza na Seleli, Mpendazoe na sasa Kilufi wa Mbarali

Taarifa hii bado inahitaji kuthibitishwa kabla ya watu kufikia hitimisho.

Lakini niseme tu kwa ufupi kwamba, Mbunge wa mbarali Dickson Kilufi si maarufu kiasi hicho na hata kusema kwamba ni mmoja katika wale wa kundi la wapambanaji dhidi ya ufisadi, ingawa umaarufu si tiketi ya kuwa mpambanaji. Kumbukumbu yangu ni kwamba alikuwa ni diwani kabla ya kushinda ubunge 2010 na alielezwa tangu awali kuwa katika misuguano na uongozi wa ccm wilaya ya mbarali na uongozi huo wa ccm wilaya ya mbarali walishapendekeza afukuzwe uanachama lakini uongozi wa mkoa wa mbeya ukamnusuru. Bila shaka kinachoendelea kujiri huko mbarali ni muendelezo wa ugomvi uliopo baina yake na uongozi wa wilaya.

Sitegemei mbunge wa ccm kufungwa jela kirahisi kiasi hicho. Nachofikiria ni kwamba labda atakuwa amehukumiwa kifungo cha kwenda jela ama kulipa faini na bila shaka atakuwa amelipa faini na kurudi zake mbarali.
 
Radio One wametangaza amefungwa miezi kumi au alipe faini ya milioni 5. Amekubali kulipa faini.
 
nchi hii kweli inawenyewe!

I watched them on black and white electron tube TV

I now watch them on high resolution plasma tv

they are much older to be sure

more 'wizened' as they usher in their sons and daughters

to captain the ship in turbulent waters.
 
cha msingi alipe faini, awaachie ubunge wao - turudi kwenye kalinye kalinye na wanamagamba's kugawa mahindi ya misaada wakati wa kampeni na kununua vipande vya kupigia kura nyumba kwa nyumba. ila sina uhakika kama mbalali wana njaa, sasa sijui this time watapeleka msosi wa aina gani kule.
 
taarifa hii bado inahitaji kuthibitishwa kabla ya watu kufikia hitimisho.

Lakini niseme tu kwa ufupi kwamba, mbunge wa mbarali dickson kilufi si maarufu kiasi hicho na hata kusema kwamba ni mmoja katika wale wa kundi la wapambanaji dhidi ya ufisadi, ingawa umaarufu si tiketi ya kuwa mpambanaji. Kumbukumbu yangu ni kwamba alikuwa ni diwani kabla ya kushinda ubunge 2010 na alielezwa tangu awali kuwa katika misuguano na uongozi wa ccm wilaya ya mbarali na uongozi huo wa ccm wilaya ya mbarali walishapendekeza afukuzwe uanachama lakini uongozi wa mkoa wa mbeya ukamnusuru. Bila shaka kinachoendelea kujiri huko mbarali ni muendelezo wa ugomvi uliopo baina yake na uongozi wa wilaya.

Sitegemei mbunge wa ccm kufungwa jela kirahisi kiasi hicho. Nachofikiria ni kwamba labda atakuwa amehukumiwa kifungo cha kwenda jela ama kulipa faini na bila shaka atakuwa amelipa faini na kurudi zake mbarali.

habari ni kweli ila alitakiwa alipe faini TShs 500,000 au kifungo miezi kumi hivyo amelipa fedha na kuachiwa huru
 
Hizi sheria zetu hazieleweki, hata Steven Wassira Tyson alishawahi kupatikana na kosa mahakamani la kutoa
rushwa katika uchaguzi (Refer kesi ya Warioba V Wassira: Bunda constituent). Adhabu aliyopewa ni
kutogombea cheo chochote kwa uongozi kwa kipindi cha miaka 5, na baada ya hapo akawa huru na sasa
hivi ni Mbunge na Waziri.

Pamoja na madhaifu hayo ya sheria yetu, inakuwa je JK anateuwa a convicted corrupt guy kwenye cabinet
yake? Ni ujumbe gani anatuma kwa Watanzania? Kwamba birds of the same feather flocks together, TAFAKARI!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom