Kitilya na wenzake wakiri makosa, wahukumiwa kulipa faini TZS Bilioni 1.5 au kwenda jela miezi 6

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitillya, Shose Sinare, Sioi Solomon, Bedason Shallanda na Alfred Misana wamekiri makosa na wametakiwa kulipa TZS 1.5 bilioni kama fidia kwa kuisababishia hasara Serikali na kila mmoja kulipa faini shilingi milioni 1 ya mahakama au kwenda jela miezi 6, kutoka na kesi ya Uhujumu Uchumi iliyokuwa inawakabiri

Mashtaka yote 58 yalifutwa kwao na kubakiza shtaka moja la kuisababishia hasara Serikali

Kesi hii ilianza jana saa 11 na kuisha saa 2 usiku katika Mahakama ya Mafisadi.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani milioni 550 kwa Serikali ya Tanzania kutoka benki ya Standard ya Uingereza.

Aidha, wanadaiwa kula njama za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ili waweze kujinufaisha wenyewe na washirika wao.

Mawakili wa washtakiwa walikuwa ndg. Alex Mgongolwa na Jeremiah Mtobesya.

Soma pia > Kisutu: Mahakama yawafutia Mashtaka Harry Kitilya na wenzake, Polisi yawakamata tena
 
Kuliko kulipa hiyo Bilioni 1.5 ni bora kukubali kukaa jela miezi sita (ambayo kiuhalisia ni miezi isiyozidi minne) na hapo hapo kuvuta muda kwa kukata rufaa.

Wakilipa pesa, basi watakuwa wanayo pesa mingi ya kuchezea, na wakitoka bado watafuatwa fuatwa sana.

Hizi hukumu ni maalum kwa matajiri tu, maskini mwenye kushtakiwa kwa kuiba mbuzi mmoja, atahukumiwa kukaa jela miaka miwili.
 
Sasa hapo ndo Sheria huwa siielewi, Hawa jamaa walipiga billion 6, wamekaa mahabusu muda mrefu Sana halafu hukumu walipe 1.5 billion au jela miezi 6!

Naona wamalizie tuu hiyo Miezi 6 ambayo watatumikia 4, na wakitoa muda waliokaa gerezani naona wataachiwa tuu wakikubali kifungo.
 
Sasa kosa la kuisababishia hasara serikali nalo halina dhamana? au ndio uhujumu uchumi kwa lugha nyingine? kama halina iweje wao wakae jela zaidi ya miaka mitatu kwa kosa lenye dhamana? wakikata rufaa wanashinda, na serikali ndio itatakiwa kuwalipa wao fidia, wameonewa kwa makosa yaliyokuwa hayana dhamana halafu leo wanayafuta kirahisi tu.

Na hiyo milioni moja ya mahakama ndio adhabu mpya au maana sijawahi kuisikia kabla, kumbe siku hizi mahakama inalipwa kwa kutekeleza wajibu wake.
 
Mbona faini na kifungo haviendani? Kulipa faini Bilioni 1.5 au kwenda jela miezi 6. Si bora niende tu jela hiyo miezi 6 ambayo ni kama miezi mi 3, kisha nitoke nije nitumie kwa uhuru hizo Bill 1.5. Tena hao jamaa wameshasota sana ndani.
 
Kuliko kulipa hiyo Bilioni 1.5 ni bora kukubali kukaa jela miezi sita (ambayo kiuhalisia ni miezi isiyozidi minne) na hapo hapo kuvuta muda kwa kukata rufaa.

Wakilipa pesa, basi watakuwa wanayo pesa mingi ya kuchezea, na wakitoka bado watafuatwa fuatwa sana.

Hizi hukumu ni maalum kwa matajiri tu, maskini mwenye kushtakiwa kwa kuiba mbuzi mmoja, atahukumiwa kukaa jela miaka miwili.
Hujaelewa hukumu mkuu. Wanatakiwa kulipa fidia ya 1.5B. Hii wameshakubalia kuwa watalipa. On top of that wamepigwa fine ya 1M au kifungo cha miezi 6. Tofautisha hivyo vitu. Mimi ndio nimeelewa hivyo. Yaani alipe 1M au afungwe miezi 6. Ila 1.5B iko pale pale
 
Ila Magufuli bhana eti anapambana na ufisadi upuuzi mtupu.
Hawa mimi nawashauri wakakae nyuma ya nondo kwa hiyo miezi sita yaishe maana hata wakiwahi kutoka hakuna faida hata kuwania ubunge tena. Wangehukumiwa mapema kama Mwanyika basi wangeweza kutoa hako ka bilioni maana wangekuwa wamechukua fomu za ubunge na CCM ya Magufuli ingewapitisha chap. Kwa sasa huku kitaa waambieni dili zote zimeshaisha hadi 2025.
 
Kuliko kulipa hiyo Bilioni 1.5 ni bora kukubali kukaa jela miezi sita (ambayo kiuhalisia ni miezi isiyozidi minne) na hapo hapo kuvuta muda kwa kukata rufaa.

Wakilipa pesa, basi watakuwa wanayo pesa mingi ya kuchezea, na wakitoka bado watafuatwa fuatwa sana.

Hizi hukumu ni maalum kwa matajiri tu, maskini mwenye kushtakiwa kwa kuiba mbuzi mmoja, atahukumiwa kukaa jela miaka miwili.
Mkuu umesoma vizuri kweli hayo maelezo kunafidia ya 1.5b halafu kuna faini ya 1m
 
Back
Top Bottom