Mbunge wa Makambako (Jah People) atangaza kuwachangia Fedha Vijana watakaotaka Kuoa au Kuolewa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Mbunge wa Jimbo la Makambako Mkoani Njombe Deo Sanga (Jah People) amesema Kijana yeyote ambaye atahitaji kuoa au kuolewa ofisi yake itamchangia fedha ili kumuunga mkono katika kufanikisha ndoa yake lengo ikiwa ni kuhamasisha utaratibu mzuri wa kuoana pamoja na kuongeza idadi ya Watu Mkoani humo.

Amesema hayo wakati akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Mawande kilichopo Kata ya Utengule ambapo amesema ili kupata fedha kila Kijana mwenye dhamira hiyo anapaswa kutoa taarifa rasmi kwa Viongozi wa Serikali za Vijiji vyao na kwenda katika ofisi yake kupata fedha hiyo.

"Kwa kila Kijana anayetaka kuoa ama kuolewa katika Jimbo langu nitamchangia kiasi cha Tsh. Laki moja na anayetaka kutoa mahari nitamchangia Tsh. Elfu 50 kupitia kampuni yangu ya Jah People, pelekeni kadi au uthibitisho wa matukio hayo kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa au Kijiji kwenye kituo changu cha mafuta mtakutana na Mtu anaitwa Neto atatoa mchango wangu"

Ikumbukwe kuwa Mbunge huyo hajaanza sasa kutoa fedha hizo kwa Vijana wanaohitaji kufunga ndoa ambapo amesema jambo kubwa linalofanyika ni uboreshaji kwenye namna ya utoaji wa fedha kutokana na shughuli nyingi alizonazo.
 
Anawapa na kazi ama shughuli za kufanya kulea wake watakaoooa?

Maana wengine hawaoi sababu wanahofia kutunza familia kutokana na kukosa vipato vya kujitosheleza.

Sasa elfu 50 sawa nimepewa kisha tunaishije kwa wale wasio na shughuli?na hali ngumu hii labda uelewa wangu mdogo
 
Puuzi sana huu badala ya kuangalia huduma mbovu za kijamii na jinsi ya kutatua!

Hawa viongozi wetu ni mapoyoyo!

Kwa hiyo ukishamwolea Hana kazi Hana nyumba na hajui atakula nini !!
 
UKITAKA KUOA, KUOLEWA AU KUTOA MAHARI UTACHANGIWA PESA NA MBUNGE

"Kwa kila kijana anayetaka kuoa ama kuolewa katika jimbo langu nitamchangia kiasi cha shilingi laki moja na anayetaka kutoa mahari nitamchangia elfu hamsini kupitia kampuni yangu ya Jahpeople "-

"Pelekeni kadi au uthibitisho wa matukio hayo kutoka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa au kijiji kwenye kituo changu cha mafuta mtakutana na mtu anaitwa Neto atatoa mchango wangu" - Mbunge jimbo la Makambako Deo Sanga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mawande kilichopo kata ya Utengule.

Chanzo: Ice Fm
FB_IMG_1692117950689.jpg
 
Back
Top Bottom