Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM) mbaroni kwa kukutwa na Silaha 16 na risasi 536

Mimi nilidhani Wabunge wanaoonekana hawafai ni wa Upinzani pekee na CCM wote ni Malaika kumbe hata Kwao kuna Vitimbi?

Huyo mbunge alikuwa kasahau kuwa kipindi hiki cha awamu ya tano siyo sawa na vipindi vya awamu ya tatu na nne! Ni sawa na ile awamu ya kwanza, chini ya jemedari Dr Magufuli!!!
 
Asilimia kubwa ya Waarabu na Wahindi wanaoishi Bara wameshiriki sana kufanya uharamia huu ! Then mtu baadaye anakuja kutajirika anatudaganaya eti anafanya kazi kwa bidii ,masa mengi,......Ndio maana amekuwa Bilionea akiwa kijana mdogo ...tunaojua aasili ya utajiri wao tunachekaaaaaa ,...hlafu hapo kwenye hiyo orodha ya maeneo ya uharamia umeisahau Singida!
Majangili mengi yamejificha kwenye chama cha CCM
 
Mtazame na msikilize RPC wa Mkoa wa Shinyanga akifafanua ujangili wa mbunge huyu wa CCM wazee wa sifa na mapimbio kwa jiwe kumbe wana mambo yao.....
 
Huwa tunawaambia mazwazwa ya ccm yakiongozwa na kibogoyo wao kuwa ni wahuni na wezi pia majangili lakin wachache huwa hawaelewi now wataelewa hasa lile genge la wahuni linaloongozwa na yule mpuuz wa uvccm supported by jujumani bashite.
 
Kumbe Sasa nyie nanihii eeh Nani nyie uvccm huyu nchambi atakuwa ametumwa na mabeber amchafue nchambi kwa kumwekea siraha na na nyama poli ili kumchonganisha na serkali ya malaika mtukufu jiwe chuma kwelikweli, hao hawakitakii mema chama chetu wanataka bavicha tuwape mwanya wa kutusema.
 

Polisi mkoani Shinyanga wanamshikilia Mbunge wa Kishapu (CCM) Suleiman Nchambi kwa tuhuma za kukutwa na silaha 16, risasi 536 pamoja na nyara za Serikali
==

Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Suleiman Masoud Suleiman maarufu Suleiman Nchambi (CCM) kwa tuhuma za kupatikana na silaha 10, risasi 536 na nyama zinazodhaniwa kuwa ni za wanyawapori kinyume cha sheria.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano Mei 6,2020, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Mei 3,2020 majira ya saa sita kasoro usiku katika mtaa wa Lubaga kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

“Mei 3,2020 majira ya sita kasoro usiku Kikosi kazi cha askari wa upelelezi kikiongozwa na Kaimu Mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi kwa kushirikiana na Afisa wa Wanyamapori mkoa wa Shinyanga Perfect Mbwambo walifanya upekuzi kwenye makazi ya Mbunge wa Jimbo la Kishapu baada ya kupata taarifa za kiintelejensia kuwa Mheshimiwa huyo alikuwa akifanya uwindaji haramu kwenye eneo la Negezi wilayani Kishapu akiwa na gari yenye namba za ujasili T760 DSD Nissan Hard Body”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

“Katika upekuzi huo walifanikiwa kukamata nyama iliyodhaniwa kuwa ni wanyamapori yenye uzito wa kilogramu 35 zikiwa zimehifadhiwa kwenye jokofu lililokuwa jikoni,jingine sehemu ya mazoezi na nyama nyingine ilikutwa kwenye gari hilo likiwa limeegeshwa nyumbani kwake ndani ya uzio wa nyumba hiyo”,amesema Kamanda Magiligimba.

“Katika gari hilo kulikutwa silaha moja aina ya shortgunWakati askari hao wakiendelea na upekuzi ndani ya chumba chake cha kulala zilipatikana silaha zingine za aina mbalimbali na kufanya jumla ya silaha zilizokamatwa kuwa 16 ambazo ni Airgun 3, Shortgun 3,Rifle 8, Pistol 1 na Mark IV 1 pamoja na risasi 536 zikiwa kwenye kabati la nguo",anaeleza Kamanda.

“Baada ya uchunguzi wa awali iligundulika kuwa silaha 10 ambazo ni Airgun 2, Rifle 5, Shortgun 2 na Mark IV 1 kati ya 16 anazimiliki isivyo halali”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

Kamanda Magiligimba amesema nyama hizo zimepelekwa maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi na gari husika limekamatwa.

“Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. Natoa onyo kali kwa yeyote atakayejihusisha na vitendo vya kumiliki silaha isivyo kihalali hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake”,amesema Kamanda Magiligimba.
Good intelligence n good work of the spy defective.... Hii kazi ni ya muda mrefu na uweledi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom