Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,726
Wana Jamvi
"Mbunge" wa Karagwe kwa njia ya Kuchakachua, Gosbert Blandes (CCM), leo amesindikizwa na kikosi kizima cha Polisi ili kwenda nyumbani kwao kijijini kufanya sherehe ya kujipongeza. Msafara wake ulihudhuriwa na watu waliokuwa wanaficha nyuso zao kwa aibu ili wasifahamike ni kina nani.
Huku mitutu ya bunduki ikielekezwa kila upande wa barabara, watu waliokutana na msafara huo walikuwa wakitoa kilio kuashiria msiba mkubwa uliogubika hapa Karagwe.
Wakati hayo yakifanyika "Mbunge" kipenzi wa wana Karagwe, Deusdedit Jovin Kahangwa, leo amehutubia wana Karagwe kupitia Fadeco Radio, akiwashukuru kwa kumpigia kura nyingi na mshikamano waliouonyesha wakati wote. Katika hotuba hiyo iliyochukua takribani nusu saa, shughuli za biashara katika mji wa Karagwe zilisimama kwa muda huku kila mtu akisikiliza kwa makini hotuba hiyo. Baadaye alibaki studio akijibu maswali mbalimbali ya wasikilizaji kwa muda wa saa moja.