"Mbunge" wa Karagwe asindikizwa na Polisi kwenda nyumbani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Mbunge" wa Karagwe asindikizwa na Polisi kwenda nyumbani

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Baija Bolobi, Nov 4, 2010.

 1. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Wana Jamvi

  "Mbunge" wa Karagwe kwa njia ya Kuchakachua, Gosbert Blandes (CCM), leo amesindikizwa na kikosi kizima cha Polisi ili kwenda nyumbani kwao kijijini kufanya sherehe ya kujipongeza. Msafara wake ulihudhuriwa na watu waliokuwa wanaficha nyuso zao kwa aibu ili wasifahamike ni kina nani.

  Huku mitutu ya bunduki ikielekezwa kila upande wa barabara, watu waliokutana na msafara huo walikuwa wakitoa kilio kuashiria msiba mkubwa uliogubika hapa Karagwe.

  Wakati hayo yakifanyika "Mbunge" kipenzi wa wana Karagwe, Deusdedit Jovin Kahangwa, leo amehutubia wana Karagwe kupitia Fadeco Radio, akiwashukuru kwa kumpigia kura nyingi na mshikamano waliouonyesha wakati wote. Katika hotuba hiyo iliyochukua takribani nusu saa, shughuli za biashara katika mji wa Karagwe zilisimama kwa muda huku kila mtu akisikiliza kwa makini hotuba hiyo. Baadaye alibaki studio akijibu maswali mbalimbali ya wasikilizaji kwa muda wa saa moja.
   
 2. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Radio Fadeco please tuwekeeni clip ya mahojiano mlofanya na huyo mbunge mdhurumiwa
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Inasikitisha sana...
  Hao maaskari waendelee kumlinda 24/7, vinginevyo naye atachakachuliwa...haki ya wengi si ya ku'fondle nayo ati!
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Sasa haya ni maisha gani? Atalindwa siku zote?
   
 5. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mimi nilikuwa omurushaka, nilishangaa sana maana hata msafara wa rais haulindwi hivyo, Bunduki zilikuwa njenje kana kwamba adui yuko karibu. Polisi walikuwa tayari kufyatua risasi.
  Kwa masikitiko waliyoonyesha watu wa omurushaka, ni kweli ni kama wamefiwa. Polisi kumlimda hivyo mbunge ni dalili ya wazi kuwa ni mbunge wa kuchakachua, na wananchi ndio adui zake waliolengwa mitutu na polisi. Mama mmoja amesikika akisema, "miaka mingine mitano ya kuumia"
   
 6. Profesy

  Profesy Verified User

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  This if unfair and this is complete oppression. Hivi kitu kama hii tunashughulikia vipi?
   
 7. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Itabidi iwe hivyo mkuu. Labda akaishi exile.
   
 8. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Sasa huyo mbunge wa kuchakachua atawakilisha nani kama watu wake hawamtaki kiasi hicho? Haya maajabu jamani!
   
 9. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Haitawezekana kulindwa mda wote siku yake itafika tu,sasa jeshi limekuwa la kulinda wezi jamani na sio kupambana na wezi.
   
 10. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Blandes my Friend, najua wewe umebebeshwa mzigo ulioukataa kiungwana. Maisha yanaweza kuendelea tena kwa usalama na tena bila hofu nje ya ubunge. Fanya maamuzi sahihi kwa thamani ya maisha yako, familia YETU na wategemezi Wako.
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kuna jambo naamini, Bila kuchakachuana wenyewe kwa wenyewe hatuwezi kuheshimiana.
   
 12. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  you can't fool people all the time!
   
 13. W

  We can JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Heri uwe maskini wa mali ukawa huru na amani kuliko kulalia mapesa huku ukilamba miguu ya mafisadi na kuwapa laana wanao, wazazi wako na wajuu pia. Laana hii ni ya kujitafutia. Utaishije kwa namna hii mbunge. Mbunge ameajiriwa na wananchi wake. Kabla ya kuingia bungeni, lazima akae nao, ajui shida zao, mawazo na mapendekezo yao, na akitoka bungeni lazima afanye mkutano nao kuwapa yaliyojiri. Mwajiri ni bosi. Sasa kama mwajiriwa anapewa ulinzi huku waajiri hawana, maana yake yeye ni bosi. Na si hivyo tu, yeye ni mungu mtu. Tokea lini mungu akawatumikia aliowaumba? Bila shaka maana ya neno MTUMISHI limepotea. Kulirudisha ITAGHARIMU siyo pesa, bali AMANI ya nchi yetu.
   
 14. Ngigana

  Ngigana JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Mheshimiwa you have made my day!" Bila kuchakachuana wenyewe kwa wenyewe hatuwezi kuheshimiana"! Loo hii ni kali!:hippie:
   
 15. U

  Uswe JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  unaogopa nini kama umachaguliwa na watu?
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ipo siku walinzi wataanza apo ndo atatia akili,piga moto then kushney
   
 17. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  https://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania-2010/84991-msimamizi-wa-chadema-north-mara-kijijini-nyamongo-anechinjwa-jioni-ya-leo.html
   
 18. kuberwa

  kuberwa JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 568
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mwisho wake umefika huyo! May b ameahidiwa uwaziri ndo maana anafanya hivyo kwa uroho wake wa madaraka! Poleni ndugu zangu wa karagwe Mungu atamshushia galika afie mbali!
   
 19. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hizo ndiyo tabia ya Mtawala kwamba lazima awe na ulinzi. Lakini kama angekuwa amechaguliwa kama kiongozi wa watu angekuwa anabebwa na kushangiliwa badala ya kuzomewa.
   
 20. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #20
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 513
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Poleni wana Karagwe na Wanyambo wote kwa kuchaguliwa mbuge asiyekuwa chaguo lenu. Poleni kwasababu hayo ndo madhara ya uchakachuzi. Kukimbia au kuwekewa ulinzi sio muafaka wa tatizo. Blandes dhuruma ni dhuruma tu. Historia itakuhukumu na sidhani kama wananchi wa Karagwe na hasa kule kijijini kwenu Ihembe II watafurahi na kukupa ushirikiano, na hata wakifanya hivyo itakuwa haitoki moyoni. Pengine utakuwa mmoja wa wabunge wengi ambao wakisha chaguliwa uhamia Dar es salaam. Je uko Dar es salaam si kuna wananchi wa jimbo hilo ulilolazimisha kuongoza. Unadhani watakupa ushirikiano. Haiwezekani kwani dhuruma ni dhuruma na haina mipaka. Utakuwa rafiki wa nani wewe. Kwanini uwe mpweke katika jamii yako, acha watu waamue ni nani wanamtaka awaongoze. Inshort for the last 5 years you have done nothing tangible to your people.
   
Loading...