Uchaguzi ujao CCM Karagwe waweweseka na kivuli cha UKAWA

kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,025
494
Habari nilizorushiwa na mtu wangu wa karibu ni kuwa CCM Karagwe imezidi kuweweseka baada ya wananchi jana kuandamana kupinga hotuba ya mbunge wao ndg Blandes aliyoitoa tarehe 15/05/2015 akimshambulia DC wa Wilaya hiyo kwamba ni mzigo na ana uswahiba na wananchi wa RWANDA ambao wengi ni wahamaji haramu.

WanaCCM wenye nia ya kugombea ubunge jana wakachukua nafsi hiyo kuandaa wananchi wengi kufanya maandamano hayo toka mji wa kibiashara Omurushaka hadi mji wa kiutawala Kayanga mwendo wa kilomita 10.

Nyepesi nyingine ni kuwa CCM ilihaha kuokoa aibu ya kupigwa chini mahakamani kupinga ushindi wao wa vijiji 36 katika kata ya Kiruruma ambapo huko ndiko anatokea mwenyekiti wa CCM Wilaya ndg Mutafungwa.

Habari mitaani zinasemekana CCM wilaya walikuwa wanachangishana fedha ambazo malengo yake hayakujulikna wazi kuwa ni ya nini kwenda kuokoa ushindi wao dhidi ya hukumu ambayo wengi walitarajia kuwa ushindi huo ungepigwa chini na mahakama baada ya kuona utetezi na mashahidi wa CCM kuwa weupe kulingana na kanuni za uchaguzi.

Taarifa zilizo wazi ni kwamba mbunge wa sasa ndg Blandesi chama kimemchoka na alifanya makusudi bungenzi kumwaga mboga za DC kwa PM , Nyepesi zilizo wazi ni kuwa KARAGWE wanataka mabadiliko kupitia CHADEMA na mbunge mtarajiwa ni ni yule aliye na makao ya kudumu na inasemekana Mwl Prince Rwazo vijana wanamtegemea sana na wana ishi naye huko japo Blandes alimfanyia rafu kwa RAS akahamishiwa Biharamulo.
 
Back
Top Bottom