Polisi wavamia nyumbani kwa Mbunge wa Arusha G. Lema

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Polisi wamefika nyumbani kwa Mbunge wa Arusha mjini kwa ajili ya kufanya upekuzi! Itakumbukwa kuwa Tangu alipokamatwa Dodoma Jumatano jioni Mbunge huyo hajaruhusiwa kuonana na mtu yeyote,sio mke wake wala mwanasheria wake,

RPC amekuwa akijibu kuwa ni amri kutoka Ikulu kuwa asionane na mtu yeyote.Polisi kuzuia mbunge asionane na mtu ni ukikukwaji wa haki za msingi za binadamu na uvunjwaji wa katiba ya nchi.

Updates;

Polisi wamesachi nyumbani kwa mbunge wakiongozwa na OC CID na hawajakuta chochote. Ulikuwa msafara wa magari manne ya polisi walio na kila aina ya silaha
 
Msiwe na wasiwasi wana Arusha mkuu wa mkoa bwana Gambo na wengine zama zao nao zitapita tu Kama zilivyopita za Akina Magesa Mulongo aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha,awamu nao nae zama zake zitapita tu ni suala la muda tu kusubiri! Hivyo mpeni tu Lema moyo,mwambieni kuwa mtu mweusi na roho zao zinakuwa za kichawi msiogope
 
Polisi wamefika nyumbani kwa Mbunge wa Arusha mjini kwa ajili ya kufanya upekuzi!
Itakumbukwa kuwa Tangu alipokamatwa Dodoma Jumatano jioni Mbunge huyo hajaruhusiwa kuonana na mtu yeyote,sio mke wake wala mwanasheria wake,RPC amekuwa akijibu kuwa ni amri kutoka Ikulu kuwa asionane na mtu yeyote.Polisi kuzuia mbunge asionane na mtu ni ukikukwaji wa haki za msingi za binadamu na uvunjwaji wa katiba ya nchi

Kwahio angekuwa sio mbunge ingekuwa sawa?!!
 
Polisi wamefika nyumbani kwa Mbunge wa Arusha mjini kwa ajili ya kufanya upekuzi!
Itakumbukwa kuwa Tangu alipokamatwa Dodoma Jumatano jioni Mbunge huyo hajaruhusiwa kuonana na mtu yeyote,sio mke wake wala mwanasheria wake,RPC amekuwa akijibu kuwa ni amri kutoka Ikulu kuwa asionane na mtu yeyote.Polisi kuzuia mbunge asionane na mtu ni ukikukwaji wa haki za msingi za binadamu na uvunjwaji wa katiba ya nchi
Nendeni kwenye maono...Mjinga tu anafikiri anaweza ku mblackmail rais eti 'asipoacha kufanya anayofanya atakufa kabla ya 2020' Hiyo ndio nini kama sio kukosa akili. Watu wa usalama hawamwachii hadi aseme nani kampa maono. Msifikiri watu wenye akili zao wataamini huu upuuzi wa maono. Ngoja aisome namba vizuri.
 
mdomo ulikiponza kichwa...binafsi napenda sana harakati za kupinga maovu kwenye jamii lakini siungi mkono harakati za kufanya maovu na mambo ya wehu eti unapinga maovu. wapi wapinga maovu wengi tz nawaheshimu sanaaa MF. zitto na wengine wengi wanaotumia hoja za akili lakini sio lema. elimu...elimu....elimu.
 
Labda ni tishio kwa usalama wa Taifa, kwa hasira zake zile mmmh

Anaweza kufanya lolote hata na wale wanaopiga majanga ya dunia.
 
mdomo ulikiponza kichwa...binafsi napenda sana harakati za kupinga maovu kwenye jamii lakini siungi mkono harakati za kufanya maovu na mambo ya wehu eti unapinga maovu. wapi wapinga maovu wengi tz nawaheshimu sanaaa MF. zitto na wengine wengi wanaotumia hoja za akili lakini sio lema. elimu...elimu....elimu.
Lema huwa anachochea maovu?
 
Sijui lema anafanya vipi shughuli zake za kibunge maana kutwa kufanya mambo yasiyo na kichwa wala miguu! Kama sio mahakamani basi no polisi! Sidhani kama watu wa Arusha walimchagua ili awe anahudhuria kila Mara polisi na mahakamani? Halafu ikifika kipindi cha uchaguzi, atadai nadhani mliona namna nilivyokua nikinyanyasika na serikali, ndio maana sikuweza timiza ahadi zangu, hivyo nipeni muda tena ili niweze timiza ahadi zangu! Halafu anarudia Yale Yale! Janja yake ishafahamika! Arusha mkataeni huyu mtu hawafai kabisa!
 
Polisi wamefika nyumbani kwa Mbunge wa Arusha mjini kwa ajili ya kufanya upekuzi! Itakumbukwa kuwa Tangu alipokamatwa Dodoma Jumatano jioni Mbunge huyo hajaruhusiwa kuonana na mtu yeyote,sio mke wake wala mwanasheria wake,

RPC amekuwa akijibu kuwa ni amri kutoka Ikulu kuwa asionane na mtu yeyote.Polisi kuzuia mbunge asionane na mtu ni ukikukwaji wa haki za msingi za binadamu na uvunjwaji wa katiba ya nchi
Bavicha kwa uongo hamjambo teh teh yani mtu afanye uhalifu halafu msingizie ikulu
 
Polisi wamefika nyumbani kwa Mbunge wa Arusha mjini kwa ajili ya kufanya upekuzi! Itakumbukwa kuwa Tangu alipokamatwa Dodoma Jumatano jioni Mbunge huyo hajaruhusiwa kuonana na mtu yeyote,sio mke wake wala mwanasheria wake,

RPC amekuwa akijibu kuwa ni amri kutoka Ikulu kuwa asionane na mtu yeyote.Polisi kuzuia mbunge asionane na mtu ni ukikukwaji wa haki za msingi za binadamu na uvunjwaji wa katiba ya nchi
Polisi wanapowashughulikia wahalifu, wana utaratibu wa kutumia nguvu zao zote!
....hii si maskhara...!
...itafanyika, kisha vyovyote vile, itaendelea!
 
Aisee!
Niliona hapa jf maiti zilizotupwa Makuyuni na mwanafunzi wa Makumira kuawa, vipi wauaji wameshakamatwa!?
Hivi, ile habari ya aliyekutwa na bunduki 11 ilikuwa kweli? Amekamatwa!?
Hivi katika issues kama hizi, Spika wa Bunge hawezi kuingilia kati kuuliza kinachomkumba 'mwenzake'!?
 
Back
Top Bottom