Mbunge wa Igunga, Dalaly Kafumu mikononi mwa TAKUKURU

Mpekuzi Tanzania

Senior Member
Mar 11, 2018
179
250
Mbunge wa Igunga Dalali Kafumu anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa tuhuma za kugawa milungula kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa JIMBO ili waweza kumpa kura kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea.

Heko kwenu takukuru lakini msiishie kuhoji tunataka kuona wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma, Sheria yenu ya 2007 inawapa Mamlaka.

Tunataka Taifa lenye mwelekeo wa maono ya Mkuu wa Nchi kuelekea uchumi wa kati

Dalaly-Kafumu.jpg

=====

UPDATES:
Dr Kafumu ambaye alikamatwa leo hii na baadaye kuachiliwa, amedai Vikao vyote anavyofanya amevitolea taarifa. Na anafuata muongo uliotolewa na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru ambaye aliwaaeleza Wabunge Wakamilishe ahadi zao.

Dr. Kafumu amedai yupo kwenye hii ziara kukamilisha ahadi alizotoa.

Hapa chini ni Barua aliyomuandika Katibu wa CCM (W), ya kutoa taarifa kuhusu Ziara za kutoa ahadi alizo ahidi.

====​

Katibu wa CCM (W)

Wilaya ya Igunga

IGUNGA

Ndugu,

Yah: KUKAMILISHA AHADI ZA MBUNGE JIMBO LA IGUNGA
Rejea somo hilo hapo juu.

Tarehe 14 Juni 2020 Wabunge wa CCM tulikutana na Katibu Mkuu wa CCM (Taifa) Mhe Bashiru Ally na akatuelekeza tukamilishe kazi za kutimiza ahadi zetu tulizoahidi kwenye Serikali, Jamii na Chama cha Mapinduzi kwa sababu tunaendelea kuwa Wabunge hadi pale Mhe Rais atakapovunja Bunge Kikatiba kwa Tangazo kwenye Gazeti la Serikali kwenye tarehe za mwezi Julai mwaka 2020. Alielekeza tuendelee na kazi zetu za kibunge hadi tarehe 13 Julai 2020, ambayo ni tarehe ya kuanza kuchukua fomu kwa ajili ya kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi.

Kwa maelekezo hayo nitakamilisha ahadi zangu kuanzia tarehe 23 Juni 2020 hadi tarehe 9 Julai 2020. Baadhi ya ahadi nilizoahidi wakati wa Ziara zangu za kikazi Jimboni Igunga mwezi Agosti mwaka 2018 na mwezi Septemba mwaka 2019 ambazo sijazikamilisha na natarajia kuzikamilisha ni kama ifuatavyo:-

[TD valign="top"]
Na
[/TD]
[TD valign="top"]
Kata
[/TD]
[TD valign="top"]
Kijiji
[/TD]
[TD valign="top"]
Ahadi
[/TD]
[TD valign="top"]
Gharama
(Shs)
[/TD]

[TD valign="top"]
1.​
[/TD]
[TD valign="top"]
Igunga​
[/TD]
[TD valign="top"]
Igunga Mjini​
[/TD]
[TD valign="top"]
Kuchangia ujenzi wa Ofisi ya CCM Tawi la Mashariki​
[/TD]
[TD valign="top"]
300,000​
[/TD]

[TD valign="top"]
Mgongolo​
[/TD]
[TD valign="top"]
Kuezeka Ofisi ya Tawi la CCM Mgongolo​
[/TD]
[TD valign="top"]
300,000​
[/TD]

[TD valign="top"]
Mwanzugi​
[/TD]
[TD valign="top"]Kuchangia ujenzi wa Mtaro wa umwagiliaji kilimo cha mpunga wa Kikundi cha Mabambasini Mwamapuli[/TD]
[TD valign="top"]
1,000,000​
[/TD]

[TD valign="top"]
2.​
[/TD]
[TD valign="top"]
Nanga​
[/TD]
[TD valign="top"]
Bulyang’ombe​
[/TD]
[TD valign="top"]Kuchangia nguvu za wananchi katika ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Bulyang’ombe[/TD]
[TD valign="top"]
1,000,000​
[/TD]

[TD valign="top"]
Nanga​
[/TD]
[TD valign="top"]Kununua masufuria kwa ajili ya kikundi cha akinamama wajasiliamali Nanga.[/TD]
[TD valign="top"]
200,000​
[/TD]

[TD valign="top"]
3.​
[/TD]
[TD valign="top"]
Bukoko​
[/TD]
[TD valign="top"]
Mangungu​
[/TD]
[TD valign="top"]Kuchangia nguvu za wananchi katika ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Mangungu[/TD]
[TD valign="top"]
1,000,000​
[/TD]

[TD valign="top"]
4.​
[/TD]
[TD valign="top"]
Kininginila​
[/TD]
[TD valign="top"]
Kininginila​
[/TD]
[TD valign="top"] Kuchangia sherehe ya wananchi kujipongeza kwa ajili ya ushidi wa CCM katika Uchaguzi wa Mkuu wa mwaka 2015. Ahadi hii niliitekeleza mwaka 2019 lakini Mwenyekiti wa CCM Kata ya kininginila hakuziwasilisha na akakimbia. (Nimelazimika kurudia kuzitoa ili kuweka uhusiano wa chama chetu CCM na wananchi sawa).[/TD]
[TD valign="top"]
600,000[/TD]

[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]

 Kukarabati pikipiki ya Ofisi ya CCM kata ya Kininginila​
[/TD]
[TD valign="top"]
200,000​
[/TD]

[TD valign="top"]
5.​
[/TD]
[TD valign="top"]
Itunduru​
[/TD]
[TD valign="top"]
Kagongwa​
[/TD]
[TD valign="top"]Kuchangia nguvu za wananchi katika ujenzi wa Bwawa la Kijiji cha Kagongwa.[/TD]
[TD valign="top"]
500,000​
[/TD]

[TD valign="top"]
6.​
[/TD]
[TD valign="top"]
Lugubu​
[/TD]
[TD valign="top"]
Lugubu​
[/TD]
[TD valign="top"]Kuchangia nguvu za wananchi katika ukarabati wa bwawa la kijiji cha Lugubu linalotmiaka na wananchi wa vijiji vya Itumba na Lugubu[/TD]
[TD valign="top"]
1,000,000​
[/TD]

[TD valign="top"]
7.​
[/TD]
[TD valign="top"]
Isakamaliwa​
[/TD]
[TD valign="top"]
Isakamaliwa​
[/TD]
[TD valign="top"]Kununua pikipiki ya Ofisi ya CCM kata ya Isakamaliwa ambapo niliyonunua mwaka 2014 aliondoka nayo isivyo kihalali Katibu aliyemaliza muda wake.[/TD]
[TD valign="top"]
2,200,000​
[/TD]

[TD valign="top"]
8.​
[/TD]
[TD valign="top"]
Mtungulu​
[/TD]
[TD valign="top"]
Mtungulu​
[/TD]
[TD valign="top"]Kununua sare za vikundi vya ngoma za akinamama Mtungulu, Mwajinjama na Maguguni[/TD]
[TD valign="top"]
600,000​
[/TD]

[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
[/TD]
[TD valign="top"]
Jumla
[/TD]
[TD valign="top"]
8,900,000
[/TD]

Naomba kuwasilisha.

Asante sana.

Dkt. Dalaly Peter Kafumu
MBUNGE WA IGUNGA

Nakala:

 Katibu wa CCM

Mkoa wa Tabora

TABORA

 Mkuu wa Wilaya

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama

Wilaya ya Igunga

IGUNGA
 
900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
3,055
2,000
Mbunge wa Igunga Dalali Kafumu anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa tuhuma za kugawa milungula kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa JIMBO ili waweza kumpa kura kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea.

Heko kwenu takukuru lakini msiishie kuhoji tunataka kuona wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma, Sheria yenu ya 2007 inawapa Mamlaka.

Tunataka Taifa lenye mwelekeo wa maono ya Mkuu wa Nchi kuelekea uchumi wa kati

jamaa kafanya udalali
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
12,385
2,000
Mbunge wa Igunga Dalali Kafumu anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa tuhuma za kugawa milungula kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa JIMBO ili waweza kumpa kura kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea.

Heko kwenu takukuru lakini msiishie kuhoji tunataka kuona wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma, Sheria yenu ya 2007 inawapa Mamlaka.

Tunataka Taifa lenye mwelekeo wa maono ya Mkuu wa Nchi kuelekea uchumi wa kati

Huyu siyo mbunge bali alikuwa mbunge. Ungeandika aliyekuwa mbunge..
 
mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,365
2,000
Mbunge wa Igunga Dalali Kafumu anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa tuhuma za kugawa milungula kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa JIMBO ili waweza kumpa kura kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea.

Heko kwenu takukuru lakini msiishie kuhoji tunataka kuona wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma, Sheria yenu ya 2007 inawapa Mamlaka.

Tunataka Taifa lenye mwelekeo wa maono ya Mkuu wa Nchi kuelekea uchumi wa kati

Wanamuonea mzee wa watu wangapi wanatoa rushwa hawakamatwi,Tulia ametoa ngapi mbeya,kigwangala mbona hatusikii kukamatwa
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,100
2,000
Mbunge wa Igunga Dalali Kafumu anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa tuhuma za kugawa milungula kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa JIMBO ili waweza kumpa kura kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea.

Heko kwenu takukuru lakini msiishie kuhoji tunataka kuona wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma, Sheria yenu ya 2007 inawapa Mamlaka.

Tunataka Taifa lenye mwelekeo wa maono ya Mkuu wa Nchi kuelekea uchumi wa kati

Ni yule wa kutoa siri za makinikia?
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
35,896
2,000
Takukuru chini ya Brigedia John Mbungo naona wamepata meno zaidi. Kumbe hakuna kinachoshindikana

Hao takukuru wanacheza siasa nyepesi. Ukiona mtu wa ccm anasumbuliwa na takukuru, ujue sio kwa sababu ya kutoa rushwa kwani wanaccm wote wanatoa rushwa, ila ujue huyo haaminiki kuwa atakubali hoja ya kumuongezea muda Magufuli ya kukaa madarakani zaidi ya miaka 10.
 
dolevaby

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
11,328
2,000
Mbunge wa Igunga Dalali Kafumu anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa tuhuma za kugawa milungula kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa JIMBO ili waweza kumpa kura kwenye mchakato wa uteuzi wa wagombea.

Heko kwenu takukuru lakini msiishie kuhoji tunataka kuona wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma, Sheria yenu ya 2007 inawapa Mamlaka.

Tunataka Taifa lenye mwelekeo wa maono ya Mkuu wa Nchi kuelekea uchumi wa kati

Hivi hawa watu wanaopenda kujiita wasomi mbona wanaakili za mbuzi? kwanini hawawezi kuendesha maisha bila vyeo? kwanini wanakuwa waoga wa maisha ya mtaani mtu kama kafumu ameshika nyadhifa nyingi lkn bado anahonga ili achaguliwe daah itabidi Shule na vyuo tufugie Mbuzi hakuna msaada shuleni
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom