Jimbo la Igunga kunufaika na minara ya mawasiliano ya simu kwenye Kata 11

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945
Igunga kunufaika na minara ya mawasiliano ya simu kwenye kata kumi na moja.

Tarehe 13 Mei, 2023 serikali imesaini mikataba na makampuni kwa ajili ya ujenzi wa minara ya mawasiliano ya simu. Halfa ya utiaji saini ilishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Jimbo la Igunga tumepatiwa minara ya mawasiliano ya simu itakayojengwa kwenye vijiji kwa mchanganuo ufuatao:

1. Kata ya Igurubi (Kalangale)
2. Kata ya Isakamaliwa (katikati ya Hindishi na Isakamaliwa)
3. Kata ya Itumba (Itumba)
4. Kata ya Itunduru (Itunduru)
5. Kata ya Bukoba (Mangungu)
6. Kata ya Kining'inila (katikati ya Iyogelo na Mwanyagula)
7. Kata ya Kinungu (Katikati Mwamagobo, Mwandinhimiji na Kinungu)
8. Kata ya Mbutu (katikati ya Mbutu na Mwabakima)
9. Kata ya Mwamashimba (katikati ya Mwamashimba, Ijogoyha na Mwanyalali)
10. Kata ya Nguvumoja (katikati ya Nguvumoja na Mwanshoma)
11. Kata ya Mtungulu (Mtungulu)

Tunaishukuru serikali kwa kuendelea kutoa kipaumbele kwa wananchi wa Jimbo la Igunga kwenye kuboresha miundombinu ya kiuchumi na huduma za kijamii. Kazi iendelee.

Nicholaus George Ngassa
Mbunge wa Jimbo la Igunga
17 Mei, 2023

WhatsApp Image 2023-05-17 at 10.00.57.jpeg

#KAZINAMAENDELEO
 
Back
Top Bottom