TANZIA Mbunge wa Chalinze (Said Bwanamdogo) afariki dunia

TANZIA Mbunge wa Chalinze (Said Bwanamdogo) afariki dunia

Inaaminika alikuwa akiumwa kansa ya koo. Kwa stage aliyofikia asingeweza kupona hata kama angerudi india sana sana angeongeza wiki chache au miezi kadhaa ya kuishi kwa mateso makali. Tatizo hili la kansa linakua kwa kasi ya ajabu. Sijui watafiti wa wizara ya afya wana majibu gani kuhusu tatizo hili. Kansa ishawamaliza ndugu zangu 4 na rafiki 3 kwa muda wa miaka takribani 5 hivi iliyopita.

Upimaji wa gonjwa hili haufanywi mapema kwa watu wengi. Kansa ikigundulika mapema sana kuna uwezekano 'mkubwa' wa kupona. Wagonjwa wengi hugundua ugonjwa wakiwa hoi na baada ya 'try and error treatment process' ya muda mrefu ya hospitali zetu za chini.

Mwisho iwapo utabahatika? kupewa rufaa toka muhimbili ya kwenda india hapo ndipo utawajua wizara ya afya kitengo cha wagonjwa waondao nje ya nchi. Rushwa, kujuana, na uzembe ni sehemu ya maisha yao. Pale unaweza kuambiwa kuwa zamu yako itakuwa miezi 7 ijayo. Kansa haitaki bureaucracy yenu ya kiswahili. Itaendelea kumtafuna mgonjwa. Anapofika india huwa too late.


Operations zao humpunguzia mgonjwa maumivu ya eneo ilipokuwa kansa. Baada muda atatakiwa arudi tena kwa matibabu ya sehemu nyingine.

Wakuu tupigane na tatizo hili. Ukimwi unaweza kuishi nao, sio kansa. Kwa kuanzia nenda kapime sasa. Kwa waliouguza nadhani wanafahamu hili, kwa kansa, unaweza kuomba hata kuanzishwe sheria ya 'mercy killing'.


Rip Bwanamdogo. Umetangulia.
koo, nakataa sikuwahi kusikia hilo...hasa kwa muheshimiwa!
anyway Mola amlaze mahala stahili mjomba wangu!
 
ccm wanatutia HASARA. WANAWEKA WAGOMBEA AMBAO NI WAGONJWA SO BAADA YA MUDA MFUPI WANATURUDISHA TENA KWENYE CHAGUZI NDOGO..!!! WENZAKE WANAFIA KUANZIA SOUTH AFRICA,USA N.K,YEYE MOI MUHIMBILI TENA ALIKOLAZWA MUDA MREFU??????????????????????????????????

Jamii forum hapaishiwi vituko.
 
View attachment 133696

Source: EA Radio

Mbunge wa Chalinze (CCM) Mh. Said Bwanamdogo amefariki Dunia leo asubuhi katika Taasisi ya Mifupa MOI, alikokuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu, Ofisi ya Bunge inaendelea na Taratibu za mazishi/maziko baada ya kuwasiliana na ndgu wa marehemu



NB: Tafadhali msiniulize ugonjwa maana haujasemwa
Kwanini ugonjwa haukusemwa? Hata hivyo tumejua, kama alikuwa Moi atakuwa alianguka na bodaboda
 
View attachment 133696

Source: EA Radio

Mbunge wa Chalinze (CCM) Mh. Said Bwanamdogo amefariki Dunia leo asubuhi katika Taasisi ya Mifupa MOI, alikokuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu, Ofisi ya Bunge inaendelea na Taratibu za mazishi/maziko baada ya kuwasiliana na ndgu wa marehemu



NB: Tafadhali msiniulize ugonjwa maana haujasemwa
Hiyo Tafadhari yako inatafakarisha sana
 
Baada ya hapo Imani Madega wa Yanga nae akachukua fomu ya ubunge jimbo hilo hilo akishindana na mbunge wa sasa. Nae alishatangulia mbele ya haki
Duh Imani Madega alikufa kwa ugonjwa ganI?
 
Back
Top Bottom