Mbunge wa CHADEMA (Msigwa) atalipoteza jimbo kwa mwendo huu

CCM will make both Sugu and Msigwa to be one-term assemblymen. Their victories were something of serependity and entirely fortuitious since none of them drudged for them. For instance, internal disputes within CCM and subsequent party leaders split over Mwakalebela's case are major culprits behind the party's defeat in Iringa. But as CCM attempts to consolidate coherence within itself and among its proponents, I don't see any chances of such fluke victories for Magwanda in 2015 general elections. Next time you will real have to moil and toil to grab each single vote you're looking for.
 
Hizi dhana mbili kwa ukweli siziamini sana kwani zinawafanya wengine waonekane bora kwa wengine. Kusema kwamba kwa "beef" za CCM ndiyo maana Msigwa akashinda siyo kweli na ni kutaka kuwafanya wana Iringa Mjini hawajui ni nini maana ya mabadiliko. Bifu zao ni kichocheo kilicho wafanya wana Iringa waone kwa urahisi kwamba CCM hawako kwa maslahi yao na hivyo kuigeukia CHADEMA na Msigwa.

Duniani kote wananchi hubadilisha uongozi kutokana na makosa ya uongozi wenyewe. kama siyo sera za CCM kutofautiana na zile za CHADEMA unafikiri wana Iringa wangeichagua CHADEMA? Kulikuwa na mgombea mwingine wa nafasi hiyo hiyo ya Ubunge kutoka NCCR-Mageuzi, Mariam Mwakingwe. Mbona yeye hilo Bifu la wana CCM halikumsaidia kushinda? Ili uweze kumshinda mpinzani wako kisiasa ni lazima uka-pitalize kwenye makosa yake na ndivyo CHADEMA na Msigwa tulivyo fanya na wala si dhambi kisiasa.

Na hii dhana ya kuamini wana Iringa waliichagua CHADEMA kwa sababu ya wanachuo siyo ya kweli hata kidogo ingawa ki ukweli na wao wana mchango wao. Mwaka 1995 hapa Iringa kulikuwa hakuna CHuo Kikuu chochote kile lakini wana Iringa waliichagua NCCR-Mageuzi na Mbunge wake Mfwala Magoha Kibaassa. Hata wananchi wa kawaida ambao si wanachuo wanao uwezo wa kuchambua mambo na kufanya maamuzi sahihi ya kubadili viongozi. Sijui takwimu zinakuonyesha wasomi walikuwa wangapi kwenye uchaguzi wa Mwaka 2010 au ni asilimia ngapi ya wana Iringa Mjini wote.

Naujua na kuuthamini sana mchango wa wasomi katika kuleta mabadiliko ya kweli kwenye jamii yoyote ile, lakini sitaki mchango wao huo uwe ni kifungo kwa wengine. Kwa nini tusimhamasishe Msigwa kutembelea watu wake wote badala yake tuna specify kwa wasomi wa kwenye Contena la RUCO ambayo ni sehemu ya kunywea Pombe?

Wasomi waje na vitu Creative na Tangible kwa ajili ya manufaa ya watu wa Iringa halafu hapo ndipo tutaona mchango wao na tofauti yao na wananchi wasio wasomi ,na siyo kumshinikiza Mbunge awafuate kwenye Grocery zinazouza Pombe.

Iringa Mjini kuna Kata 16 na kote huko kuna watu na wanashawishiana wenyewe kwa wenyewe kufanya mabadiliko.

Watu kama ninyi ndiyo mnaoleta heshima katika jukwaa hili si lolote bali hoja zilizoenda shule. Good.
 
sijui kwa nini umejiita Ipogolo. Lakini ni nini kimekutuma uanze kuzungumzia uchaguzi ambao uko mbele kwa miaka minne kuanzia sasa. Chiku ana haki ya kugombea kama atakuwa hai na bado mwanachama wa CHADEMA. Kuna kitu kinaitwa SWOT kwenye kila uchambuzi anaoufanya mtu. Yaani Strength, Weakness, Opportunity na Threat. Zitumie hizo ili uweze kutuambia Udhaifu, Uimara, Fursa na Hatari za hao wote wawili kwenye kugombea ubunge mwaka 2015.

kwa nini unaamini kwamba Chiku ndiye "akijipanga" vizuri atakibakiza kiti cha Ubunge mikononi mwa CHADEMA na siyo Msigwa? Hebu tufanye kazi za kuwatumikia wananchi kuliko kushabikia watu.
jina alinipa mzee Msimbilla kama unamfahamu. Angalia thread inayomtaja bi Chiku abwao akienda kufungua matawi kalenga. Mchungaji ni Mwenyekiti wa Cdm iringa (m) uwepo wake kule ungevuta hisia chanya za wanaotaka kujiunga na chama kwa maana ya Wamemuona Mwenyekiti wa Iringa mjini. Pia Tunasema kuwa mjini watu wameshapata mwamko wa elimu ya uraia iweje gangiloka kwa watu wenye uelewa wa masuala mengi CDM ishindwe sio kupoteza maana hatukuwa tunatetea KATA. Yanayosemwa na watu tusiyapuuze. monika Mbega watu walisema hatumpi kura CCM wakadhani utani. haya IRINGA ITAJENGWA NA SISI WENYEWE. MIAKA MINNE MBELE BILA KUJIPANGA SASA NI KAZI BURE. KWA NINI TUNAAMUA KUFUNGUA MATAWI KWA AJILI YA 2015/ TUNAKWENDA MBELE HATUA 3 TUNARUDI NYUMA HATUA 4
 
...hapana, elewemi CCM ni "WEZI" wakati nyie mnahangaika kusema wameshinda kumbe wenzenu walishaiba, mie siamini CCM kama wameshindwa kiukweli, naomba MSIGWA aje hapa atudokeze au kama kuna mtu wa Iringa.
msigwa hawezi kuja hapa. labda ajitoke dubious msigwa.
 
jina alinipa mzee Msimbilla kama unamfahamu. Angalia thread inayomtaja bi Chiku abwao akienda kufungua matawi kalenga. Mchungaji ni Mwenyekiti wa Cdm iringa (m) uwepo wake kule ungevuta hisia chanya za wanaotaka kujiunga na chama kwa maana ya Wamemuona Mwenyekiti wa Iringa mjini.

Pia Tunasema kuwa mjini watu wameshapata mwamko wa elimu ya uraia iweje gangiloka kwa watu wenye uelewa wa masuala mengi CDM ishindwe sio kupoteza maana hatukuwa tunatetea KATA. Yanayosemwa na watu tusiyapuuze.

Monika Mbega watu walisema hatumpi kura CCM wakadhani utani. haya IRINGA ITAJENGWA NA SISI WENYEWE. MIAKA MINNE MBELE BILA KUJIPANGA SASA NI KAZI BURE. KWA NINI TUNAAMUA KUFUNGUA MATAWI KWA AJILI YA 2015/ TUNAKWENDA MBELE HATUA 3 TUNARUDI NYUMA HATUA 4

Nakubaliana na maoni yako lakini tatizo langu nataka kujua mantiki yake. Msigwa kweli angekwenda angevuta watu wengi zaidi kutokana na kufahamika kwake, lakini si viongozi wote wa CHADEMA walikwenda kwenye ufunguzi huo wa mataw,i kwa nini ni Msigwa tuu alengwe kwa kutokwenda kwenye ufunguzi huo wa matawi Tagamenda?

Marekani kuna vyama vya Republican na Democrat. Na Marekani kuna wasomi wengi zaidi kuliko huku na hali bora zaidi za maisha kuliko hapa kwetu Iringa. Wao hubadilisha vyama au usimamia kwenye chama kimoja kwa sababu ya umaskini au ujinga wao? Mtu kuipenda Republican au Democrat kunasababishwa na ujinga na umaskini wa wamarekani hao?

Ninachomaanisha ndugu yangu mpambanaji mwenzangu ni kwamba hatutakuwa sahihi tukidhani usomi na uelewa wa watu wa Gangilonga unaondoa watu watakaoiunga mkono CCM. Sisi kama chama ni lazima tuweke mizizi kwenye nyoyo za watu ili wawe wanachama wetu watakaopambana na wanachama wa CCM kwani hao ni lazima wawepo tupende au tusipende. kwa zaidi ya miaka 2000 dini ya Kikristo na Kiislamu zimekuwa zikipambana kutokomeza watenda dhamb duniani,i lakini mpaka leo wapo wamejazana na hizi dini nazo zipo na zina wafuasi wa kutosha.

Kama lengo ni kushinda uchaguzi wa Iringa Mjini mwaka 2015, basi Msigwa ahamasishwe kufungua matawi Iringa Mjini na si Tagamenda ambako ni Iringa Vijijini tena ni Jimbo la Kalenga. Kwenye msafara wa kwenda kufungua matawi Tagamenda viongozi wa Iringa vijijini kasoro mwenyekiti wao ambaye ni mgonjwa walikuwepo pamoja na wale wa Jimbo la Kalenga.
 
Kila kheri CHADEMA na Msigwa na yeye mwenyewe atasema mambo haya kama yupo hapa JF basi aje
 
nDUGU, HATUNA SABABU yakupinga au kukosoa kila jambo, kama ukweli upo basi tujitahidi kulifanyia kazi ili kuongeza kasi kukubalika.Tukubali pia viongozi wa CDM wote ni binadamu wanaweza kubweteka ila ukweli bado safari ni ndefu sana. Hivyo taarifa za kiutendaji ni muhimu sana kwa kila ngazi.Wanahitaji pia kutoa vipimo vya utendaji kwa kila mbuge,diwadi na mwenyekiti mwenye dhamana. Wasibweteke kamwe na hawana budi kukubali taarifa na uwezo wa waliopewa dhamana na wananchi.
kuna kitu kimoja ni lazima tukielewe. Mhe. Msigwa hakushinda uchanguzi kwa sababu alipendwa au kwamba wananchi wa Iringa waliipenda CDM, la hasha. Tulimchangua Msigwa kwa sababu CCM walituudhi kumkata Mwakalebela. Msigwa alipata kura za chuki. Kwa hiyo strategy ya kwanza Mhe. Msigwa alipashwa kuwin nyoyo za watu na kuwahibitishia kwamba wananchi wa Iringa hawakufana makosa kumchagua. Ni kweli mhe. Msigwa n mchangiaji makini bungeni. Tatizo lake n moja na ni dogo sana, mhe. Msigwa anashughulika zaidi na maswala ya kitaifa kuliko maswala ya kitaifa kuliko maswala ya Iringa mjini. Plse, rev. Msigwa change. Haya ninayaoyaandika hapa nimekwisha mweleza Msigwa. I hope atayafanyia kazi. Other wise, mie ninamwombea afya njema, maisha marefu na 2015 arudi tena mjengoni.
 
Mimi kama Kiongozi wa CHADEMA Mkoa wa Iringa nataka kuweka wazi kwamba ni mapema mno kumpima Msigwa utendaji kazi wake kwa kipindi cha miezi kumi na moja tu.

Kwanza yeye alipoingia madarakani alikuta Mbunge aliyemtangulia kachukua mafaili yote ya Ofisi na kuondoka nayo nyumbani kwake.Ikumbukwe kwamba mbunge huyo, Monika Mbega (CCM) alikuwa ni Mbunge wa Iringa mjini tangu mwaka 2000 hadi 2010. Kwa maana nyingine ni kwamba Mbega ameondoka na taarifa rasmi za Ofisi ya mbunge wa Iringa Mjini za kipindi cha miaka 10.

Hivi Msigwa anaweza kujua ni miradi mingapi ilikuwa inasimamiwa na Ofisi ya Mbunge kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita bila ya kuwa na kumbukumbu za kiofisi ambazo Monica Mbega ameondoka nazo? Kwa mfano ni vikundi vingapi vya uzalishaji mali vilifadhiliwa na ofisi ya mbunge na vilifadhiliwa kwa kiasi gani cha fedha.

Watoto na watu wengine walio kwenye mazingira magumu wamesaidiwaje na Mbunge aliyepita na wako kwenye hatua ipi. Mbega aliwasiliana na ofisi ngapi kwa niaba ya watu wa Iringa na aliwasiliana na ofisi hizo kwa lengo lipi. Hoja yangu hapa ni kwamba kabla ya kumbebesha mzigo mkubwa Msigwa ni lazima kwanza tumsaidie kupata nyaraka hizo muhimu za kiofisi ili aweze kuchapa kazi kiufanisi.

Ni kweli kwamba Msigwa ni mwenyekiti wa Iringa Mjini, lakini swala la Uchaguzi wa kata hizi za Gangilonga na Kitanzini ambazo tulipoteza tulifanya mkosa ya kiufundi kwenye kuchagua wagombea na jinsi tulivyoendesha kampeni zetu. Hakuna wa kumlaumu katika hili, kwani wote kwa pamoja tuliipoanza kampeni tuliamini kwamba tutashinda lakini hali ya mambo baadaye haikuwa upande wetu.

kushindwa kwetu kulitokana na makosa ya kiufundi ambayo hatudhani kama huko tuendako tutayarudia tena. Kitu pekee ninachokiona ni kwamba watu wengi wanafikiri kwa kupambana na Msigwa itakuwa ni rahisi kwao kuwa wagombea wa CHADEMA kwenye nafasi ya Ubunge hapa Iringa Mjini mwaka 2015.

Ushauri wangu kwao badala ya kuanzisha kampeni za kupakana matope na kujifagilia basi tumsaidie Msigwa ili ikifika mwaka 2015 wana Iringa Mjini waone tofauti kati ya mbunge wa CCM na wa CHADEMA. Tunaye diwani mmoja Bwana Nyalusi yeye naye aonyeshe kwenye kata yake ya Mvinjeni jinsi ya kuendesha utawala bora ili mwaka 2015 tuwe na cha kuwaonyesha wananchi.

Aisee naona wewe ni kiongozi!
 
Katika sehem ambayo inanipa mashaka sana kwa kuwepo na kuendelea kuwepo uongozi wa CHADEMA ni manispaa ya Iringa.
Pamoja na kufanyika uchaguzi mdogo wa madiwani kata ya Kitanzini na Gangilonga CDM hawakupata ushindi ingawa alikuja Mbowe na Joseph Sugu na wakati wa uchaguzi Msigwa alikuwepo lakini bado CDM ilitoka kapa.
Mtazamo wangu ni kwamba CDM inaweza kupoteza jimbo by 2015 kama hali itabaki hivi.

Nini kifanyike ili tubakize jimbo?
 
kuna kitu kimoja ni lazima tukielewe. Mhe. Msigwa hakushinda uchanguzi kwa sababu alipendwa au kwamba wananchi wa Iringa waliipenda CDM, la hasha. Tulimchangua Msigwa kwa sababu CCM walituudhi kumkata Mwakalebela. Msigwa alipata kura za chuki. Kwa hiyo strategy ya kwanza Mhe. Msigwa alipashwa kuwin nyoyo za watu na kuwahibitishia kwamba wananchi wa Iringa hawakufana makosa kumchagua. Ni kweli mhe. Msigwa n mchangiaji makini bungeni. Tatizo lake n moja na ni dogo sana, mhe. Msigwa anashughulika zaidi na maswala ya kitaifa kuliko maswala ya kitaifa kuliko maswala ya Iringa mjini. Plse, rev. Msigwa change. Haya ninayaoyaandika hapa nimekwisha mweleza Msigwa. I hope atayafanyia kazi. Other wise, mie ninamwombea afya njema, maisha marefu na 2015 arudi tena mjengoni.


Hayo ndiyo maneno.
 
Nini kifanyike ili tubakize jimbo?
Kwanza kwa nini tuna hofu ya kupoteza Jimbo?

Hofu hii ya kupoteza Jimbo inajengwa na wana CCM kwa kusema kwamba wametuazima jimbo na mwaka 2015 watalichukua. Sasa miongoni mwetu ile hofu imeshawaingia na kuonekana kama ni jambo la kweli. Mimi sioni kama kweli Mwakalebela ni bora zaidi kuliko Msigwa na siamini kwamba CHADEMA mwaka 2015 tutategemea huruma za CCM kushinda. Kwa vyovyote itakavyokuwa tutakuwa Imara zaidi kuliko wao.
 
Taarifa zote zilizotolewa humu jamvini watu wanazo, na tatizo linalotutafuna watanzania tulio wengi ndugu zangu ni "UNAFIKI". lakini mimi itoshe tu kusema kuwa wapo baadhi ya wanasiasa wa CDM mwenendo wao wa kiutendaji sio mzuri na unaweza kuhatarisha ushindi wa baadae. watu saizi wanawaza CDM iongeze wabunge, madiwani na wenyeviti wa mitaa/vitongoji na si kufikiria kurudi nyumba. Kulikuwa na taarifa ya diwani wa Sinza C kujisahau na kuendekeza anasa, mi natoka sinza nimefanya utafiti siku mbili na kubaini bila chembe ya shaka kuwa ni kweli diwani huyo anahatarisha ushindi wa CDM. kila mwana sinza anamlalamikia. sasa uongozi wa chadema uchukue tahadhari sana juu ya hilo, watengeneze mfumo wa kufuatilia taarifa za kila kiongozi wa kisiasa na utendaji wake, wasioneane aibu yatawafika ya CCM, mambo ya huyu mwenzetu.
 
Katika sehem ambayo inanipa mashaka sana kwa kuwepo na kuendelea kuwepo uongozi wa CHADEMA ni manispaa ya Iringa.
Pamoja na kufanyika uchaguzi mdogo wa madiwani kata ya Kitanzini na Gangilonga CDM hawakupata ushindi ingawa alikuja Mbowe na Joseph Sugu na wakati wa uchaguzi Msigwa alikuwepo lakini bado CDM ilitoka kapa.
Mtazamo wangu ni kwamba CDM inaweza kupoteza jimbo by 2015 kama hali itabaki hivi.
msigwa anatuwakilisha vilivyo bungeni
 
Lazima tuwekane sawa hapa bila kudanganyana au kuficha ukweli. Uchaguzi wa Kitanzini na Gangilonga ni mojawapo wa kipimo cha kupima kama CDM na Mbunge wananchi wamewaelewa na kuwakubali sawa sawa.
Pili tunaposema chama kinabidi kijijenge vizuri ni pamoja na kuwa na viongozi kuanzia chini mabalozi,wenyekiti wa mitaa,madiwani kwani hawa ni watu muhimu kuweza kueneza idea na sera za chama pamoja na kuongeza wanachama ambao ni mtaji mkubwa wa chama.Kwahiyo tukibeza mawazo ya kuwa na uongozi kuanzia chini basi tujue mabadiriko ya kweli yatabaki kwenye makablasha tu.
Mwisho nadhani post hii imekuja wakati mbadala sasa la muhim ni kwamba CDM tunabidi kuongeza nguvu siyo siri hata hao madiwani waweza badirika na kuwa wenzetu wapenda mabadiriko. CCM 2015 wanamleta JESCA diwani mpya wa Kitanzini.
 
Katika sehem ambayo inanipa mashaka sana kwa kuwepo na kuendelea kuwepo uongozi wa CHADEMA ni manispaa ya Iringa.
Pamoja na kufanyika uchaguzi mdogo wa madiwani kata ya Kitanzini na Gangilonga CDM hawakupata ushindi ingawa alikuja Mbowe na Joseph Sugu na wakati wa uchaguzi Msigwa alikuwepo lakini bado CDM ilitoka kapa.
Mtazamo wangu ni kwamba CDM inaweza kupoteza jimbo by 2015 kama hali itabaki hivi.
Sina uhakika kama 2015 kama CCM bado itakuwepo? 2012 wanauchaguzi wao wa ndani, na kwa hali inavyoonekana watavurugana hadi kupelekea umauti au umahututi wa CCM. Na kwa sasa ni wazi CCM ikiwa mahututi na mwenzie CUF hali itakuwa hiyohiyo.
 
Back
Top Bottom