Mbunge Shibuda wa Chadema amerudi CCM?

Mbunge Shibuda wa Chadema amerudi CCM?

Huenda kuna makubaliano ya CCM na CDM kubadilishana EL na Shibuda, kama usajili wa wachezaji wa soka unavyofanyika
 
Mbona maelezo chini ya hiyo picha yanasema "Mbunge wa CCM John Shibuda"? sasa tunajiuliza nini hapa?
Asante kwa kutonya kosa hilo, labda nitoe utetezi dhaifu kwamba key board iliteleza ingawa si kwaida kuteleza kwa kiwango hicho labda zaidi ni lile tatizo la"double check or to over look my post before posting." Isomeke: Mbunge wa Chadema John Shibuda.
 
mkuu mbona unadhana hivo.... kuna tatizo la kumsalimia RAIS WA TANZANIA

...hakuna tatizo kama 'RAIS WA TANZANIA', ila kwa mambo ya chama na wahusika wakiwa ni wa chama husika....!! Mi sijui mkuu.
 
Unajaribu kutuaminisha kuwa siasa ni UADUI? If YES you are at the wrong place. Here is for Great THINKERS not speculators!!
 
watu wenye akili ndogo ndio hawamuelewi Shibuda

Shibuda ni 'free minded person'
yuko 'care free'

hayuko serious na chochote

yuko 'a bit comedian.'
ndio maana alikuwa anampinga Mkapa waziwazi hadi akataka kugombea urais
mwaka 2000 huku kila mtu 'akibaki mdomo wazi'

Shibuda alipaswa kuwa mbunge wa bila chama,angegombea kama mgombea binafsi
ndio angeeleweka......tatizo sheria za demokrasia ya tz haziruhusu wagombea binafsi...

na watu ambao hawajakomaa kisiasa ndani ya CHADEMA watazidi tu kukosa nae raha...hamtamuelewa...
 
Shibuda ni snitch tu, anatafuta nini kwenye vikao vya magamba..kama sio unafiki na uchochezi.
 
Moyo wa Shibuda upo CCM kama ilivyo kwa asilimia kubwa ya wabunge wa CDM. Wametumia CDM kupata chance ya kuingia bungeni baada ya kukosa nafasi hiyo ndani ya CCM

Kwa busara ya kawaida tu alicyofanya kinatoa tafsiri ya wazi ambayo tunatege sikio yanayojilia kikaoni Dodoma
 
KIKWETE ni Rais wanchi na Shibuda ni Mbunge wa jimbo la Maswa, wakisalimiana kuna ubaya gani, au kupeana mkono kunambadilisha kuwa CCM? Some times when you have nothing to say in your mind usilazimisha kuzungumza ulilonalo katika masaburi yako.
We kweli kenge mumaji, Kikwete kaja kwa shughuli za kichama, na anakutana na makada wote ndani ya NEC na halm kuu,hata mkuu wa mkoa na wilaya hakuwepo hapo,halafu hushangazwi na uwepo wa shibuda ktk tukio hilo.Huna uwezo wa ku analyze wala ku-reason, unakuja na matusi jukwaani,angalia utapigwa mtungo wewe.
 
Mimi naona sawa tu kwa huyu chalii wa siasa za bongo, angefanya hivyo kamanda Tundu Lissu ningesikitika. "MSHALE NYUMBANI KWAO NI PORINI"
 
hiyo jana **** wewe

Pole Madcheda, hii picha ima masaa tu tangu ichukuliwe pale dodoma jana wakati wa kikao cha wabunge wa CCM. Usitegemee kupata hapa hapa JF tu, jaribu kuwa mpembuzi na utakutana na picha hizo katika vyombo vingine vya habari. Kumbuka hapa JF ni live na vyombo vingine utakapopata picha hii tayari unajua kilichojilia, magazeti yanabaki kunuliwa na wenzangu wasio na digital media.
 
Mlimpa ticket ya Chademu kwa sababu mlikuwa desperate na viti vya ubunge ili proportionality ya POSHO i-balance, sasa mnalalamika nini?
 
Mlimpa ticket ya Chademu kwa sababu mlikuwa desperate na viti vya ubunge ili proportionality ya POSHO i-balance, sasa mnalalamika nini?

umeongea la maana
Shibuda huyu ndo yule yule...aliekuwa ccm

hajabadilika kitu......sasa wao wanataka awe 'mwanaharakati'...ghafla
kwa kuwa tu 'yupo CHADEMA'
 
Sioni tatizo kwa Shibuda kumlaki mwenyekiti wa ccm, tatizo langu ni kwa ccm inayojidai ni imara kumtegemea mtu kama Shibuda ili awape mbinu ya kupambana na CHADEMA! ccm=tragedy!
 
Back
Top Bottom