Mbunge: SGR itajengwa kwa miaka 81

Mbunge wa Handeni Mjini CCM, Reuben Kwagilwa, ameishauri Wizara ya Fedha na Mipango, waangalie namna ya kufadhili miradi mikubwa kwa mfumo wa dhamana ya miundombinu ‘infrastructure bond’ ili kuiwezesha Serikali kutoa huduma za wananchi kila siku.

Amesema isipofanya hivyo mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa wa SGR utachukua miaka 81 kukamilika kwakuwa mpaka sasa hata kilometa 300 bado hazijakamilika.

Kwagilwa ametoa ushauri huo jana bungeni wakati akichangia mjadala wa mpango wa tatu wa maendeleo wa kitaifa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021/22 - 2025/26,

“Standard Gage Railway tunayoijenga ukijumlisha zile njia tunazotakiwa kujenga ni kilomita 4886 hapo naongelea zile njia tu, siongelei mahala ambapo reli huwa zinapishana. mpaka sasa tumeshajenga kipande kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kilometa 300 na tunaendelea kipande cha Morogoro Makutupora kilometa 422 lakini tuko upande mwingine wa Isaka na Mwanza kilometa kilometa 249,

Kwa namna tunavyohudumia mradi huo kama tukiendelea kwa mfumo huo tutajenga kwa miaka 81 kwa nchi nzima ikiwa miaka mitano tumejenga kwa kilameta 300 na kilometa zilizosalia tutazijenga kwa miaka 81 hii katika nchi ambayo inapambana kujenga uchumi kasi hiyo haikubaliki na imegharimu Sh11 trilioni ambazo ni ‘hido investiment’ kwa sababu hatutaanza kutumia leo.,”amesema

Ameongeza “Serikali inatakiwa kujifunza na kuondokana na mfumo wa kizamani wa kufadhili miradi mikubwa kwa sababu inajipa pressure kubwa halafu inashindwa kupeleka huduma za kila siku kwa wananchi wake” amesema
Kama wapo private sectors ambao wangependa kuwekeza kwenye huu mradi sioni kama ni vibaya wakipewa ila kwa conditions faidishi kwa kila upande.
 
Sio kwa ubaya kibinadamu mwenye chake akifa shida hutokea sana...hii miradi mikubwa ilikuwa ya mwendazake alijua nje ndani na afanye nn ili ikamilike...unfortunately hayupo so kelele kama hizi lazima zitokee mwenye mlango wake kapotea na funguo so lazima hizi blahblah ziwepo...Mzee alikiri sisi ni matajiri ni kiongozi gan mwingine wa hadhi yake alishakiri hayo?
 
Pamoja na kuficha hasara(Kama Ni kweli, maana haya yamefikiriwa na akili yako kwa msaada wa CAG binadamu),
Lakini kazi aliyoifanyia taifa hili watanzania na afrika nzima tumeiona..

Kumbuka: “the devil is in the details”. Kwenye miradi ya maendeleo ya nchi hakuna kitu kama “kuona kwa macho”. Wapiga propaganda wa Magufuli walijenga hiyo hoja vichwani mwa Watanzania wengi eti “kazi zake tunaziona”. That’s all hogwash.

Kwanza, hakuna aliyediriki kuonyesha vipaumbele vya kweli vya kitaifa kulingana na mahitaji na fedha zilizopo. Pili, Magufuli alizima uwazi kwenye miradi na uhuru wa kujadili chochote kuhusu mustakabali wa taifa. Sasa hapo nani alikuwa akijua kama tunapata thamani ya pesa yetu au tunafisidiwa kiasi gani?

Sasa ndio CAG aliyemuajiri mwenyewe toka TANROADS ameanza kuanika wizi uliokuwa ukiendelea chini ya utawala ule. Macho gani yangeweza kuona hizo “kazi zake” za kutuibia?
 
Sio wewe umelaaniwa?
Magufuli ana laana kwa sababu hii ndiyo legacy aliyoacha:

1.Kuondoka duniani wakati hahitajiki.

2.Kuteka wapinzani wake kama akina Azory Gwanda.

3.Kutesa wapinzani wake kwa kuwaweka ndani kila siku.

4.Kuua wapinzani wake na wakosoaji wake kama akina Ben saanane na kuwapiga wapinzani wake risasi kama ilivyokuwa kwa Tindu Lissu.

5.Kuua uhuru wa vyombo vya habari.

6.Kuua uhuru wa kujieleza kwa wananchi kama vile kufungia mitandao ya kijamii kama twitter na kukamata wanaotumia mitandao mingine kumkosoa.

7.Kuiba kura kwa kutumia Polisi,jeshi,TISS pamoja na tume ya uchaguzi.

8.Kuua biashara za watu kupitia sera mbovu za uchumi.

9.Kudanganya katika takwimu za ukuaji wa uchumi wa nchi.

10.Kuweka mihimili yote mitatu mfukoni mwake,yaani mhimili wa urais,bunge na mahakama.

11.Kuua uchumi wa nchi kupitia sheria mbovu za uwekezaji.

12.Kuua watu kwa Corona kupitia leadership negligence.

13.Kuhakikisha kuwa akina Ben Saanane na Azory Gwanda walikipata cha mtema kuni.

14.Ukabila kwa kuhamishia rasilimali nyingi za nchi katika wilaya ya Chato na kujaza wasukuma serikalini.

15 Ukanda kwa kupeleka SGR mwanza wakati siyo economic viable zone.

16.Ubaguzi wa rangi kwa kuwakandia wanawake weusi.Imagine mtu anafanya ubaguzi wa rangi karne ya 21!Is this not insane?

17.Kugandamiza demokrasia kwa kukataza vyama vya upinzani kufanya siasa wakati CCM kufanya siasa ni ruksa.

18.Kunyanyasa malaika-watoto wa kike wasirudi shule wakipata mimba.

19.Ufisadi wa kutisha kwa kufanya miradi mikubwa bila budget kupita bungeni.

20.Wizi wa kutisha wa mali ya uma kupitia kampuni yake ya Mayanga constructions LTD.Mfano uwanja wa Chato umetengenezwa na kampuni hii bila tenda kuitwa.

21.Kubambikizia kesi za kuhujumu uchumi wapinzani wake nchi nzima na kuwatupa korokoroni bila dhamana.

22.Kugushi report ya CAG ya hasara za mabilion za ndege za ATCL na kuilazimisha ATCL watoe gawio fake kwa serekali.

23.Kupora utajiri halali na wa jasho wa matajiri wa Tanzania kwa kuwabambikizia kesi fake za kuhujumu uchumi na kuwalazimisha wakiri makosa ya uwongo kisha kuwafilisi mali zao.

24.Ufisadi na wizi wa kutisha kama ulivyoibuliwa na CAG mara baada ya dikteta kufa.
 
Angekuwepo Magufuli huo huo mradi ungekamilika kwa muda mfupi .Ardhi ya Dar mpaka morogoro ina changamoto nyingi kwanza ni mchanga ardhi yake sio ngumu pili ni mito mingi na ardhi tope nyingi lakini ukitoka morogoro ukiingia Dodoma kwenda mbele ardhi ngumu unaenda spidi ya kufa mtu kujenga
Huyo mbunge hayuko sahihi hakuangalia hali ya ardhi alipofanya hizo calculations anafikiri ardhi zote ziko sawa na kipande hicho cha morogoro na Dar

Magufuli alikomaa waanze kwanza sehemu korofi kipande cha Dar na Morogoro akijua wakimaliza hicho huko mbele itakuwa spidi kali ya ujenzi
Mkuu, Km202 main way zilizokamilika ni 150km zimekamilika na kati ya 95km za side way hamna hata moja iliyokamilika hapa nazingumzia railway infrastructure bado sijasema kuhusu electrification infrastructure na telecommunications infrastructure na line facilities nyingine. Mradi ulitakiwa kuisha tangu 2019 Leo ni 2021 na huyo mwenda zake alikuwa na analifahamu mhandisi mshauri anaendelea kulipwa maana mkataba ulikuwa ni lump sum miaka mitatu bado pesa nyingine za management kwa shirika la reli hizi zote ni kodi za watanzania. Hakuna wakuongea maana kule amejaza wasukuma wenzie kwaanzia mkurugenzi mpaka manager mradi.
 
Serikali haikuwahi kumkamata mtuhumiwa yeyote wala kumpeleka mtuhumiwa yeyote mahakamani kuhusiana na mauaji haya kitu ambacho kinajenga na kutoa ushahidi wa mazingira kuwa mhusika alikuwa ni serikali ya Magufuli.
Serikali au jeshi la police mkuu wangu? Tusichanganye mambo bro.... Hizi kesi zipo police na zinashughulikiwa na police, apa labda mkuu wa jeshi Saimoni Siro ndo atatujibu haya ila iyo evidence hakuna sehemu imemtaja magu!!! Magu alikuwa ni mkuu wa nchi lakini anawasaidizi wake sasa issue zingine zinaishia kwa wakuu wa idara jamaa angu!!!! Wanaokufa ni wengi nakupotea hao ni unaowajua wewe lakini tukisema kesi zote magu ndo muhusika sio sawa brother
 
Mbunge wa Handeni Mjini CCM, Reuben Kwagilwa, ameishauri Wizara ya Fedha na Mipango, waangalie namna ya kufadhili miradi mikubwa kwa mfumo wa dhamana ya miundombinu ‘infrastructure bond’ ili kuiwezesha Serikali kutoa huduma za wananchi kila siku.

Amesema isipofanya hivyo mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa wa SGR utachukua miaka 81 kukamilika kwakuwa mpaka sasa hata kilometa 300 bado hazijakamilika.

Kwagilwa ametoa ushauri huo jana bungeni wakati akichangia mjadala wa mpango wa tatu wa maendeleo wa kitaifa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021/22 - 2025/26,

“Standard Gage Railway tunayoijenga ukijumlisha zile njia tunazotakiwa kujenga ni kilomita 4886 hapo naongelea zile njia tu, siongelei mahala ambapo reli huwa zinapishana. mpaka sasa tumeshajenga kipande kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kilometa 300 na tunaendelea kipande cha Morogoro Makutupora kilometa 422 lakini tuko upande mwingine wa Isaka na Mwanza kilometa kilometa 249,

Kwa namna tunavyohudumia mradi huo kama tukiendelea kwa mfumo huo tutajenga kwa miaka 81 kwa nchi nzima ikiwa miaka mitano tumejenga kwa kilameta 300 na kilometa zilizosalia tutazijenga kwa miaka 81 hii katika nchi ambayo inapambana kujenga uchumi kasi hiyo haikubaliki na imegharimu Sh11 trilioni ambazo ni ‘hido investiment’ kwa sababu hatutaanza kutumia leo.,”amesema

Ameongeza “Serikali inatakiwa kujifunza na kuondokana na mfumo wa kizamani wa kufadhili miradi mikubwa kwa sababu inajipa pressure kubwa halafu inashindwa kupeleka huduma za kila siku kwa wananchi wake” amesema
Kwahiyo tukachukue mkopo China, halafu tushindwe kulipa halafu wanauchukuamradi ksma walivyofanya Zambia, sio?
 
Cha ajabu awamu iliopita kabla ya magufuli ccm ilikuwa imezama ,,magufuli akafanya jitihada zake ccm ikakaa kwenye reli yani ilifika kipindi ukivaa tisheti ya ccm unaonekana waajabu nakuzomewa juu.
Naona tutarudi kule
Ccm haikufikishi popote hapa tunajadili mauozo yaliyoibuliwa na CAG ambayo aliyekuwa anatuaminisha kuwa nyuma tulipigwa na sasa yeye mtetezi anatutetea hatuoni, kificho bado kipo na maisha yamezidi kuwa magumu zaidi na sio swala la uchama maana hizo ni kodi zetu Watanzania
 
Hivi hawa ni wale wabunge wapiga makofi au wameazimwa nchi jirani? Siamini kuanzia mpaka NDUGAI wote wamemgeuka Magufuli. Unafiki mbaya sana. Mbona hamkushauri alipokuwa hai? Ooops nimesahau na Ubunge mtu angevuliwa na kufilisiwa🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
mfumo mwingine ni wa kushirikisha sekta binafsi kumiliki hiyo reli TRC waweza uza hisa mfano kwa halmashauri na makampuni binafsi ya ndani na kwa watanzania au waweza tumia mfumo wa build and operate ila wasipewe watu wa nje.Iwe kwa watanzania tu

Bakheresa Uganda mbona kashika reli hata hapa anaweza
Wewe unaweza kuuza hisa kwa mkeo tummiliki wote? Kwani mkitumia akili kabla ya kupost mnapungukiwa na nini?
Kuna vitu ni nyeti mno jamani, hasa nishati na usafirishaji, ni nyeti sana!!!
 
Nami nina wasiwasi sana na uhai wa miradi ya kimkakati maana Hayati hatukujua anatoa wapi hela za kuifadhili, alidai tu ANAWABANA MAFISADI sasa ameenda si wananchi wala viongozi tupo njiapanda tunaifanyaje hii makitu yake!
 
Back
Top Bottom