Mbunge: SGR itajengwa kwa miaka 81

Mbunge wa Handeni Mjini CCM, Reuben Kwagilwa, ameishauri Wizara ya Fedha na Mipango, waangalie namna ya kufadhili miradi mikubwa kwa mfumo wa dhamana ya miundombinu ‘infrastructure bond’ ili kuiwezesha Serikali kutoa huduma za wananchi kila siku.

Amesema isipofanya hivyo mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa wa SGR utachukua miaka 81 kukamilika kwakuwa mpaka sasa hata kilometa 300 bado hazijakamilika.

Kwagilwa ametoa ushauri huo jana bungeni wakati akichangia mjadala wa mpango wa tatu wa maendeleo wa kitaifa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021/22 - 2025/26,

“Standard Gage Railway tunayoijenga ukijumlisha zile njia tunazotakiwa kujenga ni kilomita 4886 hapo naongelea zile njia tu, siongelei mahala ambapo reli huwa zinapishana. mpaka sasa tumeshajenga kipande kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kilometa 300 na tunaendelea kipande cha Morogoro Makutupora kilometa 422 lakini tuko upande mwingine wa Isaka na Mwanza kilometa kilometa 249,

Kwa namna tunavyohudumia mradi huo kama tukiendelea kwa mfumo huo tutajenga kwa miaka 81 kwa nchi nzima ikiwa miaka mitano tumejenga kwa kilameta 300 na kilometa zilizosalia tutazijenga kwa miaka 81 hii katika nchi ambayo inapambana kujenga uchumi kasi hiyo haikubaliki na imegharimu Sh11 trilioni ambazo ni ‘hido investiment’ kwa sababu hatutaanza kutumia leo.,”amesema

Ameongeza “Serikali inatakiwa kujifunza na kuondokana na mfumo wa kizamani wa kufadhili miradi mikubwa kwa sababu inajipa pressure kubwa halafu inashindwa kupeleka huduma za kila siku kwa wananchi wake” amesema
Huduma ipi iliyoshindwa kupelekwa?

Huyu naye ni mjinga mjinga
 
mfumo mwingine ni wa kushirikisha sekta binafsi kumiliki hiyo reli TRC waweza uza hisa mfano kwa halmashauri na makampuni binafsi ya ndani na kwa watanzania au waweza tumia mfumo wa build and operate ila wasipewe watu wa nje.Iwe kwa watanzania tu

Bakheresa Uganda mbona kashika reli hata hapa anaweza
 
Magufuli alikuwa na laana!
Angekuwepo Magufuli huo huo mradi ungekamilika kwa muda mfupi .Ardhi ya Dar mpaka morogoro ina changamoto nyingi kwanza ni mchanga ardhi yake sio ngumu pili ni mito mingi na ardhi tope nyingi lakini ukitoka morogoro ukiingia Dodoma kwenda mbele ardhi ngumu unaenda spidi ya kufa mtu kujenga
Huyo mbunge hayuko sahihi hakuangalia hali ya ardhi alipofanya hizo calculations anafikiri ardhi zote ziko sawa na kipande hicho cha morogoro na Dar

Magufuli alikomaa waanze kwanza sehemu korofi kipande cha Dar na Morogoro akijua wakimaliza hicho huko mbele itakuwa spidi kali ya ujenzi
 
AngekuwepoMagufuli huo huo mradi ungekamilika kwa muda mfupi .Ardhi ya Dar mpaka morogoro ina changamoto nyingi kwanza ni mchanga ardhi yake sio ngumu pili ni mito mingi na ardhi tope nyingi lakini ukitoka morogoro ukiingia Dodoma kwenda mbele ardhi ngumu unaenda spidi ya kufa mtu kujenga
Huyo mbunge hayuko sahihi hakuangalia hali ya ardhi alipofanya hizo calculations anafikiri ardhi zote ziko sawa na kipande hicho cha morogoro na Dar

Magufuli alikomaa waanze kwanza sehemu korofi kipande cha Dar na Morogoro akijua wakimaliza hicho huko mbele itakuwa spudi kali ya ujenzi
Sasa angekuwepo Magufuli mradi ungekamilika kwa muda mfupi kivipi wakati Magufuli alikuwa ni fisadi,mwizi na mzembe wa kusimamia rasilimali za uma?Umesoma ripoti ya CAG?Umeona jinsi alivyokuwa anaficha hasara ambayo ATCL ilikuwa inatengeneza na kutangazia uma kuwa ATCL inatengeneza faida lukuki?
 
Mbunge wa Handeni Mjini CCM, Reuben Kwagilwa, ameishauri Wizara ya Fedha na Mipango, waangalie namna ya kufadhili miradi mikubwa kwa mfumo wa dhamana ya miundombinu ‘infrastructure bond’ ili kuiwezesha Serikali kutoa huduma za wananchi kila siku.

Amesema isipofanya hivyo mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa wa SGR utachukua miaka 81 kukamilika kwakuwa mpaka sasa hata kilometa 300 bado hazijakamilika.

Kwagilwa ametoa ushauri huo jana bungeni wakati akichangia mjadala wa mpango wa tatu wa maendeleo wa kitaifa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021/22 - 2025/26,

“Standard Gage Railway tunayoijenga ukijumlisha zile njia tunazotakiwa kujenga ni kilomita 4886 hapo naongelea zile njia tu, siongelei mahala ambapo reli huwa zinapishana. mpaka sasa tumeshajenga kipande kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kilometa 300 na tunaendelea kipande cha Morogoro Makutupora kilometa 422 lakini tuko upande mwingine wa Isaka na Mwanza kilometa kilometa 249,

Kwa namna tunavyohudumia mradi huo kama tukiendelea kwa mfumo huo tutajenga kwa miaka 81 kwa nchi nzima ikiwa miaka mitano tumejenga kwa kilameta 300 na kilometa zilizosalia tutazijenga kwa miaka 81 hii katika nchi ambayo inapambana kujenga uchumi kasi hiyo haikubaliki na imegharimu Sh11 trilioni ambazo ni ‘hido investiment’ kwa sababu hatutaanza kutumia leo.,”amesema

Ameongeza “Serikali inatakiwa kujifunza na kuondokana na mfumo wa kizamani wa kufadhili miradi mikubwa kwa sababu inajipa pressure kubwa halafu inashindwa kupeleka huduma za kila siku kwa wananchi wake” amesema
Nipeni "Reuben Kwagilwa" awe mbunge wenu hapa Handeni mjini.
 
Back
Top Bottom