Mbunge Selasini apata ajali mbaya! Akimbizwa hospitali, watatu wafa papo hapo akiwamo mamake

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Mbunge wa Rombo, Mhe. Joseph Selasini kapata ajali mbaya sana muda si mrefu.

Ajali hiyo imemtokea akiwa safarini toka Arusha kwenda Rombo na ni eneo la Bomang'ombe mjini.

Watu watatu akiwemo mamake mzazi wamekufa papo hapo.

Mhe. Selasini amepekimbizwa Hospitali ya wilaya ya Hai pale Bomang'ombe; hali yake si nzuri.

Ni kweli. Mbunge Joseph Selasini kapata ajali eneo la Bomang'ombe Mjini, karibu na pale wanapouza nyanya...

Gurudumu moja la mbele la gari alilokuwa akisafiria lilipasuka. Gari likaacha njia
likaangukia darajani. Kwa wale wanaofahamu eneo hilo kuna daraja maarufu linaitwa Daraja la Mjapani.

Alikuwa akitokea Arusha kumtoa baba yake hospitalini. Yeye na Baba yake wamesalimika. Walikuwa wamefunga mikanda. Ndiyo iliyowasaidia. Wengine watatu, mama yake, shangazi yake na mama mwingine, wamekufa pale pale.

Mbunge anaendelea vizuri. Amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Hai, Anaongea na anatembea. Magari mawili ya Ambulence ndio yamefika, watahamishiwa KCMC kwa uchunguzi zaidi.

Tumaini Makene,
Kurugenzi ya Habari - CHADEMA
 
Inasikitisha sana. Pole sana mbunge wetu Mungu akupe nguvu upone haraka.
Na Mungu awalaze marehemu wote mahala pema peponi amina..
 
pole mbunge wangu ...lakini hivi kwanini mnapenda kuzurura bana..hivi hamna ipad muwe mnakaa mnasoma vitu na kuplot stratergies za kutatua matatizo ya wananchi ...aghhh
 
Mbunge wa Rombo, Mhe. Joseph Selasini kapata ajali mbaya sana muda si mrefu.

Ajali hiyo imemtokea akiwa safarini toka Arusha kwenda Rombo na ni eneo la Bomang'ombe mjini.

Watu watatu akiwemo mamake mzazi wamekufa papo hapo.

Mhe. Selasini amepekimbizwa Hospitali ya wilaya ya Hai pale Bomang'ombe; hali yake si nzuri.
namtakia kila la heri.
 
Hizi ni bad newz kwa familia ya wanamageuzi nchini kote, lakini yote tuna mwachia Mungu na pole wafiwa wote majeruhi na mh. Mungu awaponye haraka.
 
Nimechat naye mchana huu jamani. Uwii. Mungu amjaalie uponaji na afya pia Awapumzshe kwa Amani waliofariki.
 
Duh jamani! Pole sana Mh Selasini kwa ajali na pole sana kwa kuwapoteza wapendwa wako ikiwa ni pamoja na Mama Mzazi. R.I.P Wote waliofariki and get well soon Mh Selasini
 
Back
Top Bottom