Mbunge Sanga ahoji matumizi ya mkopo wa Bilioni 350 Bajeti Wizara ya Ardhi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MHE. SANGA AHOJI MATUMIZI YA MKOPO WA BILLION 350 BAJETI YA WIZARA YA ARDHI

Mbunge wa Jimbo la Makete Festo Sanga ameishauri Serikali kuacha kutenga fedha za dharula badala yake fedha hizo za dharula zielekezwe katika kutekeleza miradi

Sanga ameyasema hayo Bungeni wakati akichangia hoja kwenye bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi ya mwaka wa fedha 2023/2024

Mhe. Sanga amesema kuwa Serikali inapoweka fedha za dharula ni kama wanamashaka wakati kuna uhitaji wa fedha kwenye tume ya mipango kuhakikisha maeneo mengi ya ardhi yanapimwa

"Kwenye Mkopo huu kuna Billion 46.8 zimeelekezwa kwenye Uratibu, uendeshaji na dharula. Kwanini tuweke fedha zote hizi hap? Eneo la Upimaji tumetenga chini ya Billion 10, Je tunadhamira ya dhati kumsadia Mh Rais kutatua migogoro ya ardhi nchini?.

Rais alikopa 1.3 Trillion na alitumia kiasi cha 5 Billion tu kusimamia miradi yote ikakamilika, kwann mkopo huu utengewe 46.8 Billion?.

Namuomba Mh Waziri atupe majibu, hata vikao vya harusi vilishaacha kuweka hela ya dharula kwasababu kwa jicho la ndani fedha ya dharula haijawahi kubaki lazima iliwe.

 
Back
Top Bottom