Mbunge Ndaisaba Ruhoro - Uzeni Kahawa kwa Bei Iliyopo Ili Kuepuka Hasara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942

MBUNGE NDAISABA RUHORO - UZENI KAHAWA KWA BEI ILIYOPO ILI KUEPUKA HASARA

Wakulima wa kahawa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamemtwisha Mbunge wao zigo la kuwasaidia kutatua tatizo la kuporomoka kwa bei ya Kahawa kutoka Tsh. 3,020 ya awali hadi Tsh.1,900.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kigina Julai 22, 2023 na kuhutubiwa na Mbunge wa Ngara, Ndaisaba Ruhoro, baadhi ya wakulima wamedai kuporomoka kwa bei ya kahawa kunawapa hofu ya kupata hasara kutokana na gharama kubwa ya uzalishaji kulinganisha na bei iliyoko sokoni.

“Wakati bei ya kahawa aina ya Arabica imeshuka sokoni kutoka Tsh. 3,020 ya awali hadi Tsh.1,900, gharama zingine za maisha ikiwemo mahitaji ya familia na pembejeo za kilimo zinazidi kupanda. Serikali lazima itafute namna ya kutusaidia wakulima," amesema Ramadhan Abdul mkulima wa kahawa kutoka kijiji cha Kigina

Amesema wakulima wanatambua jitihada za kutafuta soko na bei nzuri zinazofanywa na chama cha ushirika cha Ngara Farmers cooperative Society, ni vema Serikali na wadau wengine kusaidia kutatua tatizo hilo kwa faida na maslahi ya wakulima na Taifa kwa ujumla.

Mkulima mwingine, Justus Rwechungura amepongeza jitihada za Serikali za kusambaza pembejeo za kilimo kwa wakulima, lakini akashauri juhudi hizo zihusishe utafutaji na uhakika wa soko la mazao ya kilimo ndani na nje ya nchi.

"Hakutakuwa na faida kwa Taifa kuongeza uzalishaji sekta ya kilimo bila uwepo wa soko la uhakika na lenye bei nzuri," amesema Justus

Akizungumzia kuporomoka kwa bei ya kahawa, Mbunge Ruhoro amewashauri wakulima kuuza mazao yao kwa bei iliyopo ili kuepuka hasara zaidi iwapo bei itaendelea kushuka kwenye soko la dunia.

"Soko la kahawa yetu inategemea pia soko la dunia ambalo hivi sasa limekumbwa na mtikisiko wa kiuchumi kutokana na sababu kadhaa ikiwemo vita vya Urusi na Ukraine," amefafanua Ruhoro

Amesema kutokana na ukweli huo, kuna hatari ya bei ya bidhaa ikiwemo za kilimo kuendelea kuporomoka katika soko la dunia; hivyo kuwashauri wakulima kuuza kahawa yao kabla bei haijashuka zaidi.
 

Attachments

  • kahawa-picha.jpg
    kahawa-picha.jpg
    112 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-07-26 at 00.44.47.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-26 at 00.44.47.jpeg
    46.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-07-26 at 00.44.46(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-26 at 00.44.46(2).jpeg
    65.4 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-07-26 at 00.44.46(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-26 at 00.44.46(1).jpeg
    64.2 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-07-26 at 00.44.46.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-26 at 00.44.46.jpeg
    61.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-07-26 at 00.44.44(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-26 at 00.44.44(1).jpeg
    65.5 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-07-26 at 00.44.44.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-26 at 00.44.44.jpeg
    69.1 KB · Views: 4
Back
Top Bottom