Mbunge na Madiwani Iringa Mjini, wasaidieni Madereva wa Bajaji

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,318
2,000
Vijana hawa wananyanyasika sana na polisi pamoja na mkuu wa wilaya.

Kila siku lazima wakamatwe au kupigwa mabomu ya machozi bila sababu za msingi.

RPC aliapa kuwanyoosha/kulipa kisasi kwa sababu walimzomea mkuu wa wilaya
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,041
2,000
Pole zao vijana, ila hawahawa bodaboda na bajaj ndio walipambana sana kuhakikisha wapinzani hawachukui na kurudisha fomu kwa amani, wakawa mawakala bandia wa vyama vishiriki vya CCM. Sasa waliowapambania (mbunge na madiwani) wametulia kimya kama hawaoni vile manyanyaso yao. Wamekuwa kama toilet paper, ikitumika haina maana tena, wajipambanie tu wenyewe na pia hili liwe somo kwao.

Yaani pamoja na ofisi zao kupakwa rangi ya CCM, bado wanapata taabu😄😄
 
latentspace

Member
Apr 14, 2020
12
75
Pole zao vijana, ila hawahawa bodaboda na bajaj ndio walipambana sana kuhakikisha wapinzani hawachukui na kurudisha fomu kwa amani, wakawa mawakala bandia wa vyama vishiriki vya CCM. Sasa waliowapambania (mbunge na madiwani) wametulia kimya kama hawaoni vile manyanyaso yao. Wamekuwa kama toilet paper, ikitumika haina maana tena, wajipambanie tu wenyewe na pia hili liwe somo kwao.

Yaani pamoja na ofisi zao kupakwa rangi ya CCM, bado wanapata taabu
Tatizo ni kuwa na viongozi wenye mgongano wa Kimaslahi. mkuu wa wilaya ya Iringa Mjini Mh Kasesela anamiliki coaster zaidi ya nne na ndiye aliyeshinikiza bajaji zisipite barabara za rami na analitumia jeshi la polisi kwa maslahi yake.
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,041
2,000
Tatizo ni kuwa na viongozi wenye mgongano wa Kimaslahi. mkuu wa wilaya ya Iringa Mjini Mh Kasesela anamiliki coaster zaidi ya nne na ndiye aliyeshinikiza bajaji zisipite barabara za rami na analitumia jeshi la polisi kwa maslahi yake.
Mwambieni aache ujinga, zama zimebadilika. Sehemu nyingi mikoani ruti ni fupi, madaladala yanaondoka, auze na kununua bajaj au ayapeleke vijijini hayo mabasi. Asibishane na nyakati
 
Quavohucho

JF-Expert Member
Aug 30, 2020
354
1,000
Jana kijiwe cha mashine tatu ilikuwa so poa
Pigwa sana mabomu ya machozi,
Shida ni kwamba kuna mgongano wa kimasirahi

DC ana ubia na coasters kaza town, na kuna kiongozi mmja Ali facilitate mikopo ya bajaji bado haijamripa
 
SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,318
2,000
Tatizo ni kuwa na viongozi wenye mgongano wa Kimaslahi. mkuu wa wilaya ya Iringa Mjini Mh Kasesela anamiliki coaster zaidi ya nne na ndiye aliyeshinikiza bajaji zisipite barabara za rami na analitumia jeshi la polisi kwa maslahi yake.
Jamaa ni katili sana huyu DC.
 
SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,318
2,000
Jana kijiwe cha mashine tatu ilikuwa so poa
Pigwa sana mabomu ya machozi,
Shida ni kwamba kuna mgongano wa kimasirahi

DC ana ubia na coasters kaza town, na kuna kiongozi mmja Ali facilitate mikopo ya bajaji bado haijamripa
Duh hatari sana.
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,041
2,000
Iringa mjini shida ni madiwani, wengi uelewa wao ni mdogo sana na wengi ni walamba viatu kwa hiyo wanashindwa kusimamia haki ikiwa waminya haki ni hao wanaowalamba viatu lakini pia wanashindwa kusimamia haki kwa kuwa hawaelewi mambo (elimu ndogo). Mkurugenzi wa Manispaa anapiga mahela hapo madiwani wao wapo tu wametoa macho hakuna hatua wanazochukua, Bustani ya Manispaa (gardeni) imebinafsishwa kijanja janja hata mikataba haionekani madiwani wapo tu wanachekacheka. Mikataba inaghushiwa na hela zinapigwa madiwani wapo tu. Kuwategemea watu kama hao wawasaidie wananchi ni kujidanganya. Waanze kwanza kutekeleza maagizo ya CAG
Screen Shot 2021-04-12 at 10.22.41 AM.png
Screen Shot 2021-04-12 at 8.49.42 AM.png
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,041
2,000
Jana kijiwe cha mashine tatu ilikuwa so poa
Pigwa sana mabomu ya machozi,
Shida ni kwamba kuna mgongano wa kimasirahi

DC ana ubia na coasters kaza town, na kuna kiongozi mmja Ali facilitate mikopo ya bajaji bado haijamripa
Hapo bado ishu ya wamachinga, nao uchaguzi umeshaisha sasa wataondolewa mji uwe safi.
 
kasanga70

Senior Member
Oct 19, 2015
140
250
Yaani mm ndio nashindwaga kuelewa hapa tu. Hivi Kila siku viongozi kutwa kushindana na wananchi wanao fanya kazi halali na wanalipa Kodi yaani Kila siku utaratibu mpya unatoka sheeeet...
 
SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,318
2,000
Yaani mm ndio nashindwaga kuelewa hapa tu. Hivi Kila siku viongozi kutwa kushindana na wananchi wanao fanya kazi halali na wanalipa Kodi yaani Kila siku utaratibu mpya unatoka sheeeet...
Iringa uongozi umeoza.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
44,574
2,000
Vijana hawa wananyanyasika sana na polisi pamoja na mkuu wa wilaya.

Kila siku lazima wakamatwe au kupigwa mabomu ya machozi bila sababu za msingi.

RPC aliapa kuwanyoosha/kulipa kisasi kwa sababu walimzomea mkuu wa wilaya
Ni wapuuzi hao maana Msigwa alikuwa anawatetea wakarubuniwa na CCM
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
44,574
2,000
Yaani mm ndio nashindwaga kuelewa hapa tu. Hivi Kila siku viongozi kutwa kushindana na wananchi wanao fanya kazi halali na wanalipa Kodi yaani Kila siku utaratibu mpya unatoka sheeeet...
Hii nchi inaishi kwa maagizo ya wakubwa na siyo sheria na taratibu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom