Frank Ishengoma
Member
- Oct 8, 2023
- 37
- 18
MbungeABOOD AZINDUA KIKUNDI CHA WANAWAKE WAJANE KATA YA MKUNDI SAMBAMBA NA KUSHIRIKI IBADA YA MISA STESHENI SDA CHURCH-KATA YA KINGOLWIRA TAREHE 28.10.2023.
UZINDUZI WA CHAMA CHA WANAWAKE WAJANE KATA YA MKUNDI
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdulaziz M.Abood amezindua Rasmi Chama cha Wanawake Wajane Kata ya Mkundi katika hafla iliyofanyika Katani humo ikihudhuliwa na Wanawake Wajane zaidi ya mia mbili (200+), Viongozi wa Mkoa wa Chama cha Wanawake Wajane wakiongozwa na Mwenyekiti wao wa chama cha wanawake wajane Mkoa Ndugu Doroth Mwamsiku, Mratibu kutoka Taifa chama cha wanawake wajane Ndugu Daniel Simfukwe, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Mkundi pamoja na Serikali.
Hafla hiyo imetawaliwa na shangwe, vigeregere nderemo na vifijo baada ya Mhe Mbunge kuwasili katika Ukumbi huo na kupokelewa kwa bashasha na shamlashamla kubwa.
Akihutubia hadhara hiyo Mhe. Mbunge amewapongeza Wanawake Wajane Kata ya Mkundi kwa kuunda Umoja wao wa kikundi Cha Faraja na kufanikiwa kupata faida ya shilingi laki nane (800,000/-) kupitia kuzungusha Sukari ambayo imetokana na kuchangishana 1,000 kila wiki na hii imefanyika ndani ya miezi minne tu tangu kuundwa kwa Umoja huo, vilevile Mhe Mbunge akamshuru Rais Mhe. Dkt Samia kwa kuendelea kuwajali kwa kishindo Wanawake hasa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu, kuwatengenezea Miundombinu wezeshi kwa ajili ya kuimarisha ujasiliamali wao n.k.
KUKABIDHI HUNDI
Mhe. Mbunge akapata nafasi ya kukabidhi Hundi ya tsh 1,000,000/- kwa kikundi cha wanawake Wajane cha Faraja Mkundi ili kiasi hicho cha fedha kisaidie kuongeza chachu ya kukua kwa Mitaji na kukuza Uchumi wa Wanaumoja na Jamii kwa ujumla huku akiwatia Moyo wajane hao kuwa kila kitu kinawezekana na hawana budi kupambana na kushirikiana kwa juhudi zaidi, akishukuru Bi Doroth Mwasiku amemshukuru Mhe Mbunge kwa kukubali kuwa Mlezi wao Wilaya ya Morogoro Mjini sambamba na kukipatia shilingi milioni moja kikundi wa Faraja Mkundi.
KUSHIRIKI IBADA YA MISA STESHENI SDA CHURCH KATA YA KINGOLWIRA.
Vile vile Mhe Mbunge akatembelea na kushiriki Ibada ya Misa ya Kanisa la Kisabato katika Kanisa la Stesheni SDA Church lililopo Kata ya Kingolwira ikihudhuliwa na Wachungaji mbalimbali pamoja na Waumini wapatao zaidi ya 190.
Sambamba na hilo Mhe. Mbunge akajionea hatua iliyofikiwa ya Ujenzi wa Kanisa hilo na Kuchangia Hundi ya Shilingi 1,000,000/-ili kukamilisha ujenzi wa Kanisa hilo.
Karibuni sana