Janeth Mahawanga ametembelea Kituo cha Watoto Yatima cha New Faraja Orphanage Center

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,850
928
MHE. JANETH MAHAWANGA ATOA ELIMU KUPINGA UKATILI WA WATOTO NEW FARAJA ORPHANAGE CENTER​

Mbunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dar Es Salaam na Mwanzilishi wa Taasisi ya Tisha Mama Foundation, Mhe. Janeth Elias Mahawanga na Taasisi ya Ejaz Bhalloo Foundation pamoja na Jeshi la Polisi kutembelea Kituo cha kulea Watoto Yatima cha "New Faraja Orphanage Center" kilichopo Mburahati kwà ajili ya kutoa futari na elimu kuhusiana na ukatili kwa watoto.

Mhe. Mahawanga kwa kushirikiana na wafanyabiashara na taasisi tofauti wamezungumza na watoto juu ya umuhimu wa kujiamini na kutoa taarifa pindi wanapoona dalili za kufanyiwa ukatili hususani wa kingono na kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao ili kuhakikisha kwa pamoja wanajikinga.

Aidha, Mhe. Mahawanga amewapongeza wote ambao wameguswa na Jambo hilo la kiimani la kutoa sadaka hususani kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuwaomba wadau kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Namshukuru sana Mkurugenzi wa Taasisi ya Ejaz Bhallo na tutaendelea kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha dhamira ya kupinga ukatili dhidi ya watoto inafanikiwa.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-03-28 at 21.52.25.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-28 at 21.52.25.jpeg
    100.6 KB · Views: 10
  • WhatsApp Image 2023-03-28 at 21.52.24(3).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-28 at 21.52.24(3).jpeg
    77.1 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2023-03-28 at 21.52.24(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-28 at 21.52.24(2).jpeg
    107.4 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2023-03-28 at 21.52.24(7).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-28 at 21.52.24(7).jpeg
    74.9 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2023-03-28 at 21.52.24(8).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-28 at 21.52.24(8).jpeg
    85 KB · Views: 10
Back
Top Bottom