Miaka inakimbia sana, majuzi tu hapa 2010 Dr. Slaa alisababisha ushindi wa JK kushuka kwa asilimia 20+, miaka mitatu ama minne baadae chadema walikua juu sana, sana, walianza kukubalika mpaka vijijini ambako ndo haswa kuna wapiga kura, walikubalika sana. Ilikua ukikosa kuhudhuria rallies zao unajihisi kama umekikosea heshima chama. kisha boooooom 2015, mwenyekiti mbowe akafanya maamuzi magumu, akacheza kamari ambayo binafsi ndo ilinifanya niwatoe chadema moyoni na siasa kwa ujumla. Nilijisikia kuwachukia na kuwadharau sana. Na naamini kila kinachowatokea leo na kesho ni aftermath ya uamuzi wa kipumbavu sana aliofanya mbowe back in 2015. Ile ndo ilikua turning point, binafsi naamini kama historians wataamua kuweka kumbukumbu za chadema kwa usahihi, tarehe ya kuzaliwa siijui lakini tarehe sahihi kilipokufa chama ni tarehe ambayo kilikubali kumpokea lowassa na kuua misingi yote ya kuanzishwa kwake.