CHADEMA watamkumbukaje Bi. Anna Komu?

CHADEMA watamkumbukaje Bi. Anna Komu?

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
703
Reaction score
1,143
Moja ya Taarifa za kusikitisha leo ni kifo cha Bi Anna Komu, kada wa CHADEMA kwa zaidi ya miongo 3.

Anna Komu alishika nyazifa mbalimbali za ngazi za juu kabisa ikiwemo ujumbe wa bodi ya udhamini ndani ya CHADEMA kwa nyakati tofauti.

Hata hivyo mwaka jana kwa kushirikia na Said Issa walikiburuza chama chao mahakamani wakidai mgawanyo sawa wa mali kesi iliyopelekea CHADEMA kuzuiwa kufanya shughuli zake za kisiasa.

Kama hiyo haitoshi mwishoni mwa mwaka jana waliwasilisha maombi madogo kuomba amri ya mahakama ya kukamatwa kwa viongozi wote wakuu wa CHADEMA.

Soma Pia: Anna Maulidah Komu Afariki Dunia

Swali linakuja, Je, CHADEMA watashiriki msiba huu kwa namna gani? Je, watamuenzi na kumkumbuka kama kada wao wa muda mrefu? Au watampotezea?
 
Watamuombea kwa Mungu kadri ya imani yake na alipwe kadri ya matendo yake hapa duniani...
 
Mwanamapinduzi and a true daughter of Africa she will be remembered!
 
Huyu pia alikua Ccm kabla ya kwenda chadema je CCM wanamkubuka kwa lipi?
 
Mwenyezi Mungu amlaze pema jabali la siasa za upinzani Anna Komu.
Amen
 
Huyu pia alikua Ccm kabla ya kwenda chadema je CCM wanamkubuka kwa lipi?
CCM hawawezi kuwa na baya naye tena! Mwaka jana aliwafanyia kazi nzuri sana ya kuivuruga CHADEMA. Kama kuna alilowakosea, nadhani watakuwa wameshamsamehe.
 
Moja ya Taarifa za kusikitisha leo ni kifo cha Bi Anna Komu, kada wa CHADEMA kwa zaidi ya miongo 3.

Anna Komu alishika nyazifa mbalimbali za ngazi za juu kabisa ikiwemo ujumbe wa bodi ya udhamini ndani ya CHADEMA kwa nyakati tofauti.

Hata hivyo mwaka jana kwa kushirikia na Said Issa walikiburuza chama chao mahakamani wakidai mgawanyo sawa wa mali kesi iliyopelekea CHADEMA kuzuiwa kufanya shughuli zake za kisiasa.

Kama hiyo haitoshi mwishoni mwa mwaka jana waliwasilisha maombi madogo kuomba amri ya mahakama ya kukamatwa kwa viongozi wote wakuu wa CHADEMA.

Soma Pia: Anna Maulidah Komu Afariki Dunia

Swali linakuja, Je, CHADEMA watashiriki msiba huu kwa namna gani? Je, watamuenzi na kumkumbuka kama kada wao wa muda mrefu? Au watampotezea?
Atakumbukwa kama mhujumu haki kwa tz wote ,moto wa milele umuunguze ,
 
Back
Top Bottom